Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,988
Ndugu wanaJF,
Nimelazimika kuanzisha thread hii kwa lengo moja tu la kutoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji wa jina la mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema unaofanywa na kundi la masalia kwa sababu maalum.
Mwishoni mwa mwaka jana TUNTEMEKE aliwahi kuibuka na madai kama haya kwamba John Heche anatumia cheti cha ndugu yake, na kwamba hakuwahi kusoma chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) cha mwanza. Leo tena katika thread iliyoanzishwa na mwanamasalia aliyetimuliwa Chadema bi. Juliana Shonza amejitahidi sana kutumia jina la Wegesa Charles Suguta ama Wegesa Suguta.
Bila shaka ameamua kufanya hivyo kama muendelezo wa tuhuma walizozianzisha kundi la masalia kwa kutumia ID yao ya kundi ya Tuntemeke kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Hili kundi la PM7 linataka kumuonyesha John Heche kwamba naye amegushi jina kama walivyo baadhi ya viongozi wakubwa huko ccm (wafadhili wao). Mathalani imetajwa mara kadhaa kwamba miongoni mwa watu wanaotumia majina ya kugushi huko ccm ni pamoja na Naibu katibu mkuu bara Bw. Mwigulu Nchemba (Lameck Madelu?) na Dr. HKigwangalla (Saidi Bagaile?) ambao wanadaiwa kutumia majina ya bandia.
Sasa nirudi kwenye hoja ya msingi. Kawaida sisi wakurya hata kama umezaliwa mjini ama katika mazingira ya mbali na nyumbani/kijijini lazima unapewa jina la kikurya, kwahiyo kwa wakurya wengi wanakuwa na majina mawili ama matatu lakini yote yakiwa ya mtu mmoja.
Kwa mfano mwalimu Nyerere, majina yake ni Julius Kambarage Nyerere(Julius jina la kikristo). Kuna mwanae Charles Makongoro Nyerere (Charles jina la kikristo), kuna Dr. James Mnanka Wanyancha-mwenyekiti wa Road Fund (James jina la kikristo), Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (Ernest jina la kikristo), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (George jina la kikristo. Nadhani kwa kutaja hao wachache mnaweza kuona scenario ya majina ya kikurya, naamini kuna makabila mengine yenye utamaduni kama wa kwetu.
Sasa nije kwa John Heche Suguta:
Jina lake la kikurya ni Wegesa na baba yake mzazi anaitwa Heche Suguta. Wegesa Heche Suguta jina lake la kikristo ni John, ndipo sasa unapata John Heche Suguta. Jina la kikristo la baba yake John Heche (Heche Suguta) ni Charles, ndipo sasa unapata Charles Heche Suguta.
Katika vyeti vyake vya shule John Heche anatumia jina la Wegesa Charles Suguta (Wegesa Suguta). Aliandikishwa shule kwa jina la Kikurya na akaendelea kulitumia katika harakati zake zote za kishule. Ndugu zake na John Heche ni pamoja na Bw.Manchare Heche Suguta (Mwanasheria NEMC), Chacha Heche Suguta (M/Kiti Bavicha Tarime) na Mome Heche Suguta (Tarime) kwa kutaja wachache ambao angalau wanafahamika na watu wengi.
Nimalizie kwa kuwajulisha masalia kwamba kama mnadhani mnaweza kumchafua Bw. John Heche kwa staili ya majina basi nawashauri msahau kwakuwa watu wote waliokua nae toka utotoni Tarime, shuleni alikosoma sekondari ya Bulima (O level), Musoma Alliance (A level), Bunda TTC na hatimaye SAUT Mwanza wanamfahamu sana John Heche kwa majina yote mawili.
John Heche aligombea na kushinda kiti cha udiwani Tarime mjini mwaka 2008 katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Chacha Wangwe, kwa kumshinda mbabe wa Tarime Bw. Peter Zakaria. Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu augustino (SAUT) Mwanza. Kama angelikuwa anatumia majina ya bandia ama majina ya mtu mwingine bila shaka hilo lisingejificha wakati wa kampeni za uchaguzi.
Baada ya kusema hayo nadhani nime-clear doubts zilizokuwa zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya watu hapa JF.
Nawatakia jioni njema.

Kuhusiana na majina ya heche kama moja ya shutma za mtoto wa kigogo na baharia muendesha majungu soma huu ufafanuzi wa kaka yeke John Heche.
"John Heche ni mdogo wangu kwanza naomba niweke wazi hilo...Sisi baba yetu alikua na wanawake 7 kati ya hao watoto tuko 42 wote wa baba mmoja ni marehem sasa( Mungu amweke pema) .
Mzee alikua anaitwa CHARLES HECHE SUGUTA...sasa ukiangalia hapo jina CHARLES ni la baba na pia HECHE Ni jina lingine la mzee, Jina la John la ukoo ni WEGESA na hilo JOHN ni la ubatizo,,sasa kwenye vyeti na shuleni alikua anatumia WEGESA CHARLES ambae CHARLES NI jina la mzee kama ilivyo pia HECHE,,,its not an issue kabisa ni ushauri wangu kwa vijana wa cdm wakue wajadili masuala ya Kitaifa ya kusaidia nchi sio kurukaruka kama njiwa na kusema vitu vya ajabu...jina hilo ni sahihi na la kwetu kabisa anayebisha aende Tarime aulize mzee HECHE/IMEKUBALIKA watu wanamjua baba yetu majina yote hayo ni yetu..na hilo John Heche.
Wegesa Charlese yote ni majina ya ukooVs haya ya ubatizo lakini yote ya mtu mmoja simple...Suala lingne kuna mtu wa hao jamaa anasema eti wadogo zetu wanasomeshwa na Mbunge hilo sio kweli ni UONGO na UZUSHI mtupu sisi kama familia tunasomesha wale vijana wetu wote walioko vyuoni na secondary kwa kipato halali tulicho nacho".
Manchare Charles Heche Suguta.