Ufafanuzi kwa anayejua......

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,068
2,000
Kitambo kidogo kiasi cha wiki mbili sasa nimekuwa nikitumiwa picture hizi za mdudu huyu na hata nikipita pita kwenye mitandao ya kijamii nimekuwa nikikutana nazo sana zikiwa na tahadhari kwamba ni mdudu hatari sana kwa binaadamu,naomba wataalamu walifafanue hili kweli mdudu huyu ni hatari kiasi cha kusababisha kifo?
hawa wawili wanadaiwa kuathiriwa na sumu yao
nawasilisha.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,979
2,000
Ngojea tuwasubiri waliong'atwa zaidi Mkuu waje watiririke na waserereke vizuri kwani wengine huku tulipo Mdudu au Wadudu wanaotusumbua sana na tunawaogopa mno ni wale wa HIV ( Wadudu Virusi ) ambao baadae humsababisha Mtu Kuugua Ugonjwa mbaya uitwao Dally Kimoko au UKIMWI.
 
R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,159
2,000
Mkuu hizo ni dhana tu za kutiana uoga na hazina ukweli na haijathibitishwa popote na serikali kama kuna hatari ya kwa hiyo kiumbe.

Kwa kitaalamu huyo kiumbe anaitwa spalgis epius hapo akiwa kwenye stage ya pupa kabla ya kuwa kipepeo kamili na huwa wanatumika kama predator ( of scale insects) kwa wadudu waharibifu wanakula eidha hizo mbogamboga au mapapai.

Kwa taarifa zaidi unaweza uka google na kupata taarifa zake kamili ila hana athari kama zinavyosemwa na huyo aliyetuma . 

middle east

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
1,205
2,000
Acheni uoga ....majuzi profesa wa pale sua alitoa ufafanuzi mbele ya media ...hiyo ni hatua ya ukuaji ni buu kama sijakosea ....alisema hana madhara .....wanaitaga metamorphosis kama kumbukumbu za bioz zinakamata vema
 
Selekwa

JF-Expert Member
Jul 7, 2013
728
500
Mkuu hizo ni dhana tu za kutiana uoga na hazina ukweli na haijathibitishwa popote na serikali kama kuna hatari ya kwa hiyo kiumbe.

Kwa kitaalamu huyo kiumbe anaitwa spalgis epius hapo akiwa kwenye stage ya pupa kabla ya kuwa kipepeo kamili na huwa wanatumika kama predator ( of scale insects) kwa wadudu waharibifu wanakula eidha hizo mbogamboga au mapapai.

Kwa taarifa zaidi unaweza uka google na kupata taarifa zake kamili ila hana athari kama zinavyosemwa na huyo aliyetuma .hiki ndicho kitu watanzania wengi tunakikosa,hata kutumia elimu ya darasa la tatu au la nne kama sikosei...Big up mkuu
 
Selekwa

JF-Expert Member
Jul 7, 2013
728
500
Kitambo kidogo kiasi cha wiki mbili sasa nimekuwa nikitumiwa picture hizi za mdudu huyu na hata nikipita pita kwenye mitandao ya kijamii nimekuwa nikikutana nazo sana zikiwa na tahadhari kwamba ni mdudu hatari sana kwa binaadamu,naomba wataalamu walifafanue hili kweli mdudu huyu ni hatari kiasi cha kusababisha kifo?
hawa wawili wanadaiwa kuathiriwa na sumu yao
nawasilisha.
Hawa watu mbona wanakuwa kama wana Stevens Johson syndrome,wanatakapotumia anti histamine mbona hali inaimalika bila shida unless kama shida itakuwa much severe.
 
Hunyu

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
4,789
2,000
Nahisi kuna upotoshaji mkubwa kwenye hili jambo.

Tunaomba serikali na wataalamu wafanyr kazi yao ili tufahamu maana naamini si mdudu mgeni
 
Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,068
2,000
Mkuu hizo ni dhana tu za kutiana uoga na hazina ukweli na haijathibitishwa popote na serikali kama kuna hatari ya kwa hiyo kiumbe.

Kwa kitaalamu huyo kiumbe anaitwa spalgis epius hapo akiwa kwenye stage ya pupa kabla ya kuwa kipepeo kamili na huwa wanatumika kama predator ( of scale insects) kwa wadudu waharibifu wanakula eidha hizo mbogamboga au mapapai.

Kwa taarifa zaidi unaweza uka google na kupata taarifa zake kamili ila hana athari kama zinavyosemwa na huyo aliyetuma .Shukrani chief @RMbuna,hapa sasa nimeelewa.
 
Zambotti

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,640
2,000
Amezua taharuki sana, kiasi watu hatuna raha na ulaji wa mboga za majani. isije kuwa kama propaganda za dengue
 
Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,068
2,000
Amezua taharuki sana, kiasi watu hatuna raha na ulaji wa mboga za majani. isije kuwa kama propaganda za dengue
Yaani kila mtu mtaani anamzungumzia anavyojua yeye,kinachotisha zaidi wengine wanasema ana sumu kali kama ya nyoka.ila hapa naamini wataalam watatutoa mashaka.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom