Itakumbukwa wakati Mheshiwa Rais anawaapisha wakuu wa mikoa, aliagiza Ma RC hao kuwashughulikia watendaji ili wawatii, hii ni pamoja na kuwaweka ndani kwa saa 48 ikibidi.
Je ni wakati gani RC anaweza kuamuru mtu kuwekwa ndani na kwa makosa yapi? Au anaweza kuamua tu kuwa mweke fulani ndani pasipo sababu ya msingi? Ikiwa ndivo je nini tafsiri ya utawala bora?
La pili linalofanana na hilo ni pale Mheshimiwa Rais alipooagiza vijana wote wanaocheza pool mida ya mchana kukamatwa na kupelekwa mashambani kwenda kulima ni wazo zuri na naamini litatekelezwa kwa haraka sana, lakini katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inampa mtu uhuru wa kutembea na kwenda mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili mradi asivunje sheria. Ikiwa hawa vijana watakamtwa na kukataa kwenda huko mashambani watakuwa wamekiuka kifungu gani cha sheria ambacho pengine kitasababishwa wafunguliwe mashtaka? Au watashitakiwa kwa sheria ya uzururaji? NAJIULIZA TU.