Ufafanuzi kuhus fao la kujitoa mifuko ya jamii ushahidi huu hapa

howard

Senior Member
Feb 21, 2011
188
28
UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.


Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.


1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.



2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.


Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.


Wenu.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii
source: wavuti.com
 
tunashukuru kwa ufafanuzi wenu mzuri. Jambo jingine linatusumbua ni kuhusu wanachama kubadili mifuko, kuna athari zozote?
 
Nashukuru kwa ufafanuzi, swala ambalo sijaliona hapa mfano mwanachama anafariki je ndugu zake wataruhusiwa kuchukua mafao yake au watasubiri mpaka umri wa kustaafu, au sheria imesemaje kuhusu hili.
 
Hapo ndo jk unapofanya u hr manager wangu uwe mgumu..nani ataishi na kusubiri miaka 55?hivi mko serious kweli nyie watu au
 
wizi mtupu mmewekeza ktk miradi isiyo na faida sasa mnataka kuzuia hela zetu ili muendelee kujikimu hakuna chochote na hatutaki siasa katika hela zetu. Msituletee hizo habari hatuwaelewi
 
Katika hili wafanyakazi wakikaa kimya nitasema kweli bongo kazi ipo, suppose ukafa kabla ya miaka 55 je wanaobaki wanapewa chao au wanasubiria kwanza? haya mambo magumu ndio maana mimi niliamua kujipa ajira yangu mwenyewe pumbavu na wakati naacha kazi nilichukua mpunga wa maana kama withdrawal benefits
 
walipasa waangalie life span ya mtanzania ni miaka mingapi wanaweza kuwa wameiga kutoka mataifa mengine ambayo life span ni miaka 70 na kuendelea uzoefu unaonyesha watu wengi wakiacha kazi au kuachishwa hawachukui muda wanaaga dunia pia kuna taasisi ambazo wanastaafu chini ya umri huo
 
Hawajawatendea haki wafanyakazi wa kima cha chini wanaolipwa elfu 85 kwa mwezi.Mtu huyu atanufaikaje nahiyo mikopo ya nyumba ingali yeye kwa mwezi anakatwa 10% nssf/ppf ni 8500 plus ya mwajiri inakuwa 17,000 kwa mwezi unadhani itampasa achangie miaka mingapi walau aweze kukopeshwa nyumba ya 10m.
Ndiyo ile anakwenda anaambia pesa zako hazijajitosheleza wewe kuweza kukopeshwa.
Ama kweli hii nchi imekosa watetezi kabisa.
 
upuuzi mtupu, utafanyaje assumption kuwa unaondoa fao hilo ili mfanyakazi aweze kukopa nyumba?

Unajua hitaji la mfanyakazi????
Au wanadhani kila mfanyakazi anahitaji mkopop wa nyumba??????

Si waseme tu kuwa wamefilisika????
 
mimi hapo cjawaelewa kabisa naona wanataka kuibia tu wao hizo hela wanakaa nazo muda mrefu na kuzifanyia miradi ambayo sisi wafanyakazi hatuna faida nayo kwanza hiyo mikopo ya nyumba inacomplications kibao wamiwekea conditions ngumu oo uwe na hati miliki ya kiwanja hiyo hati kuja kuipata mbinde naje wale wafanyakazi ambao wanafanya kazi kwa mikataba inakuwaje mkataba wake ukiisha na asiweze kupata kazi tena huyu mafao yake yanakuwaje atasubiri mpaka maka hiyo 55? naomba nieleweshwe kidogo hapo
 
Na je sheria hiyo imeweka kinga kwa wanachama dhidi ya uwekezaji wa mifuko ya jamii? Maamuzi ya uwekezaji fedha za mfuko ni ya nani?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Pesa yangu wachukue bila hiari na masharti makali waniwekee.., hii ni haki kweli? Mie wakati wananilazimisha kujiunga haya ya fao la kujitoa hayakuwa wazi! Hawa watu wanatumia akiba zetu kwa faida ya wachache (kuwekeza na kukopeshana wao kwa wao). Sijaona/sikia Mtanzania wa kawaida amefaidiaka zaidi ya kupata usumbufu usiokifani inapofikia wakati wa kudai mafao.
IF IT WAS MY CHOICE makato ya mafao yangu wangenipatia niyahifadhi mwenyewe!!
 
Katika hili wafanyakazi wakikaa kimya nitasema kweli bongo kazi ipo, suppose ukafa kabla ya miaka 55 je wanaobaki wanapewa chao au wanasubiria kwanza? haya mambo magumu ndio maana mimi niliamua kujipa ajira yangu mwenyewe pumbavu na wakati naacha kazi nilichukua mpunga wa maana kama withdrawal benefits
Mkuu hapo kwenye 'red" sema pole pole wasije wakakusikia wakaamu kukutungia sheria na wewe uliyeamua kujiajiri. Yaani vichwa vya wa-TZ vimejaa maji ya madafu. Eti kumwezesha mwanachama kukuopa nyumba?! Utafikiri uwezo wa kuzijenga hizo nyumba wanao! Yaani zunguka yote wao wameona mkopo mzuri ni nyumba tu. Na aliyesaini hiyo naye ni DHAIFU mara dufu!
 
kwanza watupe pesa yetu ndipo tubadili mkataba maana hatukukubaliana kulipana uzeeni.Ningeshauri wanasheria wajitokeze ili kuipeleka mifuko hii ya ifadhi ya jamii mahakamani maana wanavunja mkataba wa kujitoa bila kuwashirikisha walioingia nao mkataba.
 
Tik Tok Tik Tok...nasikia hii ngoma imerudi tena uwanjani!
 
Tik Tok Tik Tok...nasikia hii ngoma imerudi tena uwanjani!
Hawa jamaa nadhani wanatuona tuna kauzezeta vichwani vileeeee.Yaani badala ya kutupatia pesa yetu tukajikwamua kwa kuitumia kama mitaji wao wanataka tufe waifaidi.Sitaki hata kusikia hiki kitu masikioni mwangu maana nasikia hasira inanivuka mipaka juu ya unyama huu wanaolazimisha kutufanyia.
wenye ukweli wa hili la kutaka kutunyima pesa yetu toka mifuko ya jamii watwambie tafadhari ili tukaidai haki yetu.Wastssfu wenyewe wananyanyasika kila siku na wengine kufa bila kufaidi pesa yao then hawa wanataka na sisi tuunganishwe katika kapu moja.Pesa yetu ya NSSF imejenga daraja la Mwl.Nyerere na bado tunalipishwa ada ya kulitumia kweliiiiiiiiiiiii.Nyumba nijenge mimi bado nidaiwe kodi ya kulala.
 
  • Thanks
Reactions: 911
Aisee. Hapo ole wenu muandamane yake washa washa yanawahusu.
 
Aisee. Hapo ole wenu muandamane yake washa washa yanawahusu.
Hahahaaaaaaaaaa... wasomi tuna wana njia nyingi za kudai haki..hasa ukitilia maanani kuwa haki haipotei bali yaweza kuchelewa tu.
 
Back
Top Bottom