Itzmusacmb
JF-Expert Member
- Jun 22, 2016
- 1,531
- 1,133
Wakuu nipo maeneo ya Yombo Sigara mkabara na Airport hapa Dar es salaam kuna wingu zito la moto ndani ya uwanja wa ndege kama mnavyoona, aliyekuwepo maeneo hayo ajaribu kutupa maelezo.
=======
UFAFANUZI:
JamiiForums imefuatilia na kubainisha kuwa TAA wanafanya emergency drill na hivyo watu wasiwe na hofu na hali hii.
======
Hii sio ajali,wala hakuna ndege iliyodondoka.
Zoezi hili linaitwa "Emergency Drill".
"Emergency Drill" ni "igizo" la ajali au tukio la ghafla (la kutengenezwa),inaweza kuwa igizo la moto,ndege kudondoka,meli kuungua au eneo la mgodi kulipuka.
Hii ni moja ya hatua ya kupima utayari wa kukabiliana na majanga ktk sehemu za kazi na hasa zile zinazofuata "Safety Manuals" kwa kiwango kikubwa kama viwanja vya ndege,migodini,bandari na viwandani.
Zoezi hili hufanywa walau mara moja kila baada ya miaka mitatu,ili kupima uweledi na utayari wa vyombo vya uokoaji kama Zimamoto,msalaba mwekundu,hospital nk.
Miezi kadhaa iliyopita kuna "emergency drill" ilifanyika bandari ya Dsm,waliwasha makontena na kuigiza kama ajali ya moto kupima kiwango cha utayari wa uzimaji wa moto na uokoaji.
Mwaka wa jana Wachimbaji wa gesi kisiwa cha Songosongo waliandaa zoezi la kupima utayari wa "Flying Doctors-Air Ambulance",walitoa taarifa ya ajali ya mfanyakazi kuvunjika kiuno akiwa kazini,walitaka kupima ndege waliyoingia nayo mkataba wa uokozi itatumia muda gani kutoka Dsm kwenda Songosongo.
Ilitumia dakika 21 tu toka Dsm to Songosongo,wakalipa na gharama as if it was a real scenario.
Hii si Tanzania,ni duniani kote.Maana kuna watu wanaweza wakaibuka wakasema ni matumizi mabaya ya pesa.There is no compromise to principles and practices of safety!!
Japo kama kawaida,wazee wa kuongeza sifuri mwisho,huu ndio mwanya!!Unaweza kukuta gharama za nguo za "moulage team" imeongezwa sifuri mbili na "Training" ya "moulage team" watu wana visifuri kadhaa.
barafu