Ufafanuzi crane za JNHPP, Januari Makamba alikuwa sahihi mnaopinga someni hapa

Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,863
3,193
Mhandisi Christopher Bitesigirwe Mratibu wa Mradi wa JNHPP. Nimekuwa pale kwenye mradi kwa muda wa zaidi ya mwaka na ni Mtaalamu wa Mitambo. Kuna aina nyingi ya crane na kila crane inatengenezwa kwa kazi maalum. Kuna crane zinazotembea (movable cranes) na crane zinazofungwa mahali (immovable cranes).

Crane itakayofungwa pale kwenye handaki la kuchepusha mto (diversion tunnel) ambayo ni immovable crane imetengenezwa pamoja na gate la kufunga handaki la kuchepusha mto.

Lile gate lina vipande 14 ambavyo vina uzito wa tani 26 kila kimoja. Na vitaunganishwa vipande 7 kwa kila nusu gate lenye uzito wa tani 182. Hivyo crane itakayotumika kufunga gate kwa jina la kitaalamu inaitwa hoisting mechanism ambayo itakuwa inabeba vipande vya gates kwa ajili ya kuviunganisha na kushikilia. Baada ya kufunga gate, litamwagwa zege la kuimarisha gate hilo ambalo litakaa pale wakati wote (permanently).

Kwa kuwa crane hiyo imetengenezwa mahususi kwa kazi ya kuziba handaki la kuchepusha mto, baada ya kazi hiyo kukamilika crane hiyo haitakuwa na kazi tena.

Crane hiyo tunayoiongelea bado haijafika nchini na itakapofika ndio tunaweza kuanza kazi ya kuziba handaki la kuchepusha mto (diversion tunnel).
 
Nape Nnauye aliteleza, January Makamba akajikwaa. Nani ni nani?

Nape Nnauye aliposimama mbele ya bunge na kuhoji matumizi ya mkopo wa Dola bilioni 9 uliokopwa na serikali ya awamu ya tano, Wabunge baadhi waliduwaa na wengine wakagonga meza, walikubali? Hatujui, walikataa? Hatujui?

Aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete aliwahi kusema kwamba, "Mwenezi wangu akisimama kwenye jukwaa huwa sijui anaenda kusema nini! Na hatabiriki katika anachoenda kukisema. Hapa Kikwete alikiri kwamba Katibu Mwenezi wake wa chama (Nape) huwa hatabiriki katika maongezi yake.

Ni kweli, Nape aliwahi kusema mengi yenye kutia mashaka na hata yenye ukakasi ila akayafanya yaonekane ya kawaida mbele yake. Mmesahau goli la Mkono?

Leo Nape anahoji matumizi ya mkopo wa Dola bilioni 9. Na kutaka uchunguzi ufanyike wa matumizi ya hizo Dola bilioni 9. Inachekesha lakini pengine hajui anachokisema. Uchunguzi hauishii kwenye makaratasi ya kandarasi na matumizi pekee. Aliyekuwa Waziri wa fedha katika awamu ya tano ni Dr Philip Mpango ambaye ni makamu wa Rais wa sasa, anataka huyu akatoe ushahidi wa matumizi yake mbele ya jopo la wachunguzi? Kwa kifupi Waziri wa fedha ndiye anaeandaa proposal zote za mikopo kulingana na uhitaji na hata msaada wowote ule lazima upitie kwake.

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Awamu ya tano ni Kasim Majaliwa, ndo huyuhuyu wa sasa, huyu ndo msimamizi wa shughuli zote za serikali, anajua nje ndani kuhusu hii mikopo, je Nape anataka Majaliwa nae akakae kwenye hiki kikaango Cha mahojiano ya mikopo ya Dola bilioni 9?

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Awamu ya tano ndo huyu Rais wa sasa, huyu alishiriki kwenye vikao na mijadala inayohusu mikopo hii, je anataka na Rais akahojiwe juu ya mikopo hii?

Kuna muda chuki zinaathiri uwezo wa kufikiria! Wataalamu wa afya ya akili wanasema hivi "ukiihifadhi chuki moyoni, sio tu itakunyima Uhuru wa mawazo bali itakudumaza akili, lakini pia inaweza kukusababishia afya ya kimwili"

Nape akubali kwamba awamu ya tano imepita, imemaliza kazi yake, WATANZANIA wanajua na dunia inajua kuwa awamu ile haikuwa awamu ya majaribio. Ilikuwa awamu ya "Hapa kazi tu" na kazi ilionekana na kufanyika. Nimkumbushe Nape kwamba tukianza kuchunguzana chunguzana hatutaishia katika awamu ile pekee, tutafikia makaburi katika awamu pendwa kwake pia. Na pengine tunaweza kuanza kuihoji hata awamu hii kabla ya kumaliza hata mwaka mmoja madarakani.

Lakini tunaweza kubariki uchunguzi hata katika namna ya goli lile la Mkono ikiwa lilitumika ama halikutumika na waliohakikisha ushindi huo unapatikana. Ukianza kila nyama ya mtu kamwe huwezi kuacha.

Kama ilivyo kwa Nape, January nae akajikwaa pale pale alipoteleza Nape, yeye akasema mradi wa ujenzi wa Bwawa la Mwalimu NYERERE lilicheleweshwa kwa zaidi ya siku 400 😂😂 siku 400 ni mwaka na mwezi mmoja, sijajua anazungumzia mradi upi huo.

Akaja na ngonjera kwamba hakuna cranes za kunyanyua uzito wa TANI 26 nchini hadi nje ya nchi, akasahau kwamba hizohizo material zilishushwa bandarini, lakini pia akasahau kuwa kwenye mradi wenyewe hizo cranes zipo. Niseme tu kwamba kwenye mradi wapo ndugu zetu huko wanafanya kazi, alipojichanganya akasema hazipo, ma_opareta wa hizo cranes wameduwaa.

Lakini pia hata zisingekuwepo, hizo cranes zinakodishwa na makampuni kadhaa hapa nchini. January ameendeleza alipoishia Nape. January ameshindwa kutuambia ni KWANINI Kuna mgao wa umeme hivi Sasa, ameshindwa kutuambia WATANZANIA ni kwa sababu gani nchi imeweza kulala kwenye Giza kwa masaa 24 bila umeme katika baadhi ya mikoa na tatizo hilo limesababishwa na nini.

Nape aelewe kwamba wanaoipinga awaku ya tano ni mabwanyenye na sio WATANZANIA masikini. Watanzania wa kipato Cha kati na Cha chini hawako tayari kusikia awamu ya tano ikisemwa vibaya.

Lakini pia serikali ya awamu ya tano ielewe kwamba wananchi wanaoisemea mazuri awamu ya tano ni kwa sababu ya hawahawa VIONGOZI kuisema vibaya awamu ya tano. Kwa hiyo wamejikuta wanavutana na wananchi bila kujua kuwa sababu ya mvutano ni wao wenyewe. Awamu hii ikiacha kuinanga awamu iliyopita, hutosikia mtu akiisema vibaya awamu ya sasa, vinginevyo kitaumana kila siku.

Usiku mwema.
Abdoulquarim Malisa
 
Tatizo ni lugha iliyotumika kufanya "articulation" imekosa vionjo sahihi. Endapo January angemwagika kuhusu masuala haya ya kitaalamu, basi angeepusha mijadala inayoendelea kuhusu jambo hili.
Ndio maana tunaelimisha watu wanatumia conflict zao kuchafua image ya serikali
 
Hiyo crane itatengenezwa kwa kazi hiyo tu. Ikishamaliza hiyo kazi, inakuwa chuma chakavu.


Ndio maana watu tunahoji; kwanini zisitumike crane hizi za kawaida kufanya kazi hiyo???, inashindikana vipi???--- hapo ninaomba kuelimishwa zaidi mkuu.
 
Nape alisema mikopo hiyo, na matumizi yake, hakukuwa na uwazi.

Nadhani anamaanisha Makamu wa Rais wa wakati huo, Waziri wa fedha wa wakati huo, Waziri Mkuu wa wakati huo na Bunge la wakati huo, hawakushirikisha. Kila kitu kilifanywa na Rais na mpwaa wake ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha.
 
Ndio maana watu tunahoji; kwanini zisitumike crane hizi za kawaida kufanya kazi hiyo???, inashindikana vipi???--- hapo ninaomba kuelimishwa zaidi mkuu.
Umeambiwa hizo clain ni permanent sio za kukodi jifunze kusoma
 
Tatizo ni lugha iliyotumika kufanya "articulation" imekosa vionjo sahihi. Endapo January angemwagika kuhusu masuala haya ya kitaalamu, basi angeepusha mijadala inayoendelea kuhusu jambo hili.
Ni kweli kabisa.
Ndio maana narudia kusema huyu si mtu sahihi kwenye hiyo nafasi...na hii inafanya kuzidi kuamini uwepo wake pale ni kwa kitu fulani...ila muda ni mwalimu mzuri ila tutakuwa tumeshachelewa...
 
Ndio maana watu tunahoji; kwanini zisitumike crane hizi za kawaida kufanya kazi hiyo???, inashindikana vipi???--- hapo ninaomba kuelimishwa zaidi mkuu.
Nadhani mhandisi amefafanua sana. Kwa uelewa wangu ni kuwa hizi crane za kawaida zipo kwa matumizi ya kawaida. Kuna baadhi ya kazi, hizi crane za kawaida haziwezi kufanya. Fikiria kwa mfano crane ambayo inatakiwa inyanyue kitu kwenye height ya mita 40, hizi crane za kawaida haziwezi. Mkono wake utakuwa mfupi lakini pia itaishiwa nguvu.
 
Back
Top Bottom