Student visa hutolewa kwa mwanafunzi aliyepata udahiri katika chuo chochote kilichoko nje ya nchi kwa mara ya kwanza iwe kwa kupata scholarship au kwa gharama zako mwenyewe,au mwanafunzi aliyeko chuoni kwa ufadhili wa makampuni au wazazi wake. Kwa wale wanaobahatika kupata scholarships za serikali mchakato wake hadi hatua ya kuipata hiyo student visa huratibiwa na wizara ya elimu.
Kwa watu binafsi hatua ni zile zile za kuomba nafasi katika chuo kilichoko nje ya nchi kwa kutumia vigezo vya chuo husika na kulipia ada zote za masomo ikiwa ni pamoja na gharama zingine muhimu kama malazi, chakula na usafiri. Mambo yote hayo yanapimwa na mamlaka husika kwa kuangalia uzito wa akaunti zako za benki, Kama pesa zipo na unaweza kufanya malipo basi student visa ni ya kwako hadi simestra hiyo hadi utakapotakiwa kuongeza muda.