MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Mtu anayeshindwa kubainisha udhaifu uliosemwa na CAG ni wa aina gani, uwezo wake wa kusimamia sheria,taratibu na kanuni za bunge utatoka wapi?Mimi sijawahi kuona SPIKA mwenye uelewa wa hivi. Wabunge wa CCM walienda kishabiki zaidi, ni mara 100 zaidi spika angekua dada TULIA AKSON au ANDREW CHENGE na sio huyu mzee.
CAG ameulizwa swali na Mtangazaji Anold Kayanda vipi mbona mmetoa ripoti nyingi halafu hatuoni hatu zikichukuliwa? Mzee wa watu akasema kua kama hatua hazichukuliwi ni udhaifu wa bunge, yeye kafuatwa na mwanahabari na wala hajamwita, sasa kwa kauli hiyo kadhalilisha vipi taifa?. Yeye makosa yake ni yepi? Sasa huyu spika badala ya kutazama ujumbe ahangaike nao, yeye anahangaika na mtu ambaye kisheria kwanza hagusiki. Kwanza CAG sio Prof Assad bali ni taasisi.
Wabunge wa CCM wana kila sababu ya kulaumiwa kwa kumchagua huyu mzee, ni bora hata angekua mzee Chenge.Angalau huyu anaelewa na anajua kuchanganua mambo.
Bunge lishughulike na ripoti za CAG liache kujihami kwa udhaifu wake.Kama sio dhaifu ziko wapi 1.5t? Zilitumikaje?