Je atapata kozi hii UDSM?

Nimekupata mkuu, ninachosema ni kuwa kwa sababu wameandika relevant diplomas na hawakuzitaja basi ni wao watakaoamua, na lolote laweza kutokea. Wakitupa mrejesho ingesaidia sana baada ya 02.10.2017. Bila kuwa prejudiced-UDSM lazima wataangalia content ya economics kwenye hizo diploma na mtu yeyote ambae yuko kwenye hizi higher education institutions atakuhakikishia hilo. Utaona miaka ya nyuma wanachukua zaidi EGM.

Asante kwa kunielewa...

Kwa case ya form six leavers ni sahihi sana kuchukua watu wa EGM kwa maana konachoenda kusomwa ni uchumi kilimo, hakuna combination mbadala kwa kweli juu ya hili.

Ila kuhusu diploma, huwa wanachukua aina kama hiyo ya diploma kwa ajili ya kozi za kilimo biashara (am talking from experience na ikifika tarehe 2 October nitakuja na ushahidi ili kuweka kumbukumbu sawa), UDSM huwa wanaandika aina za diploma za wachaguliwa, mwaka Jana kuna vijana wamemaliza animal health and production Chuo cha mifugo Mpwapwa na walichaguliwa kwa kozi hiyo (japokua kuna maswahibu yaliwakuta na hawakujiunga na Chuo).

Na kwa mfumo wa mwaka Jana wa uombaji, ulikua ukiichagua hiyo kozi na ukatanabaisha kwamba wewe ni equivalent applicant ilikua inakuletea orodha ya "relevant diplomas" ambapo zote zilikua ni za kilimo na inaeleza kwamba ukiwa na diploma let say ya animal production utapewa first priority, diploma ya agriculture general utapewa second priority n.k.

Siku njema
 
Hata kwa idadi tu, wanaomaliza diploma na kuingia vyuo vikuu huwa wanakua wachache ukilinganisha na wale wa kidato cha sita. Ninaamini hakuna bahati katika hili, ni vigrzo na ushindani ndio vinaamua.
mwaka Jana katika kozi ya actuarial diploma walichukuliwa wawili tu, vipi ata kwa upande wa kozi nyingine wale wanaotoka diploma ngumu kupata unakuta kozi inataka watu 200. lakin 150 walichukuliwa form six leavers.
 
Amani iwe nanyi waungwana,kuna mshkaji wangu ameapply apo UDSM course ya BSC IN AGRICULTURAL AND NATURAL RESOURCES ECONOMY AND BUSINESS,O LEVEL alipata MATH C,GEOGRAPHY C,CHEMISTRY C,BIOS D,ENGLISH C,na yeye alisoma DIPLOMA IN ANIMAL HEALTH AND PRODUCTION na kupata GPA ya 4.3.Ivi anaweza akapata kweli mana anawasiwasi saana,
Huyo rafiki ako hawezi kuuliza mpaka umuulizie wewe!? Si useme tu kuwa muhusika ni wewe!
 
Huyo rafiki ako hawezi kuuliza mpaka umuulizie wewe!? Si useme tu kuwa muhusika ni wewe!
Sio kila mtu yupo jf mkuu,alafu maisha yanatofautiana sana so si kila mtu anaweza tumia simu itakayomfanya aweze kujoin umu,pia mtu anaweza kukuliza wewe kitu lakin usiwe na majibu ya kutosha so unaweza uliza hata umu jf iliupate majibu then umjibu ili atosheke,pia naami iki kitu kitakua kimewanufaisha wengi ambao labda walitaka kujua diploma ya animal healthy ina relate vipi na iyo degree,mwisho kila mtu anaweza kuwa muhusika kulingana na nafasi yake kama wewe ulivyo uvaa uhusika wakutoa aina ya jibu uloandika apo.
 
Relevance ya hiyo diploma na diploma nyingine za kilimo kwa kozi ya Agricultural Economics haitokani sana na "How much of a knowledge of Economics is in those diploma courses". Bali inatokana na " hawa (wenye hizo diploma) ndio wenye kilimo chao, kwahiyo tuwaendeleze kimaarifa ili hicho kilimo chao kifanywe kibiashara na kiuchumi", na ndio maana ukiangalia hiyo kozi inatolewa kwenye Chuo cha kilimo (Bsc. AEA pale SUA) na hiyo ya UDSM (Bsc. ANEB) iko chini ya college ya kilimo, vinginevyo ingekuwa chini ya shule ya biashara (UDBS).

Lakini ukiangalia contents za hiyo kozi (Agricultural Economics) utagundua kwamba ni kozi ya uchumi zaidi kuliko ambavyo ni kozi ya kilimo. (It is much economic and less agricultural). Kwahiyo kimantiki, kuhoji hiyo Relevance ya mtu wa diploma ya mifugo (nadhani dhidi ya mtu wa diploma ya uchumi na biashara) unakua uko sahihi kwa namna fulani.
Lakini nikukumbushe tu kwamba kozi za shahada za uchumi kwa ujumla kwa hao wenye diploma za uchumi zimejaa tele huko Mzumbe, UDSM(UDBS), CBE, IFM, na kwingineko. Kuwadahili hawa kwenye Agricultural Economics dhidi ya wanakilimo wenyewe ni sawa lakini si sawa kwa maana ya kwamba "it is right but not fair". Itakuwa ni kama "unawaleta wataalam wa uchumi kwenye kilimo" badala ya "kuleta utaalam (kuwapa utaalam wa uchumi) watu wa kilimo".

Sasa nikujibu hili swali lako;

Je, kwenye Diploma in animal health and production kuna contents za uchumi na biashara ?

Kwa sababu shughuli ya ufugaji ni shughuli ya kiuchumi, na ni biashara pia, hao wenye hiyo diploma huwa wanafundishwa baadhi ya masomo yenye muelekeo wa uchumi na biashara. Nakumbuka kwa uchache wanasoma "Principles of Production Economics and Marketing" na "Livestock Enterprise Establishment and Management".

Suala la kumudu au kutokumudu litatokana na jitihada za mhusika, yote kwa yote Oktoba 2 itaamua.

Kwa lolote karibu.
Mkuu ahsante kwa mchango wako na ushuri wako pia,mrejesho ni kama ifuatavyo,jamaa amechaguliwa vyuo viwili UDSM course hiyo ya BSC IN AGRICULTURAL AND NATURAL RESOURCES ECONOMY AND BUSINESS na SUA course hiyo BSC IN AGRICULTURAL ECONOMY AND AGRIBUSINESS, so anatakiwa kuconfirm,so kwa kuzingatia ubora wa course,wigo mpana wa kujiajiri au kuajiliwa baada yakuhitimu ni chuo kipi angeenda apo?
 
Back
Top Bottom