UDSM yang'aka Prof. Kabudi kutajwa orodha ya wenye vyeti vyenye utata. Yataka watoa orodha waulizwe

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
Habari wanaJF,

Mamlaka za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) imesema taarifa za Waziri wa sheria Profesa Palamagama Kabudi kuwa na vyeti vyenye utata sio sahihi, imetawataka wale waliohusika kufanya uchunguzi na kuotoa orodha ya majina hayo waulizwe tatizo nini mpaka Mwalimu huyo nguli wa Sheria mwenye heshima kedekede akumbwe na kashfa hiyo.

Pia Makamu Mkuu wa chuo cha UDSM (Taaluma) Prof. Luoga ashangaa na yeye jina lake kutajwa katika orodha ya vyeti feki.

Profesa Kabudi aliwahi kuwa Dean wa Shule ya Sheria pale UDSM, Aidha kwa sasa Profesa Kabudi ni Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Habari wanaJF,

Mamlaka za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) imesema taarifa za Waziri wa sheria Profesa Palamagama Kabudi kuwa na vyeti vyenye utata sio sahihi, imetawataka wale waliohusika kufanya uchunguzi na kuotoa orodha ya majina hayo waulizwe tatizo nini mpaka Mwalimu huyo nguli wa Sheria mwenye heshima kedekede akumbwe na kashfa hiyo.

Profesa Kabudi aliwahi kuwa Dean wa Shule ya Sheria pale UDSM, Aidha kwa sasa Profesa Kabudi ni Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wanashangaa nini, inawezekana kabisa. That was the order of the day in the era of Kikwete, Mwinyi and Mkapa; and possiblly in Nyerere era . Inawezekana alibugi form 4, akaiba cheti, akaenda form six akatambua makosa yake akasoma kwa bidii, na sasa ni Profesa!
 
kama alipotakiwa kuwasilisha cheti fulani na hakufanya hivyo, wahakiki waseme nini? mbona sie tunamtaka Bashite ajieleze mwenyewe ila huyu eti wahakiki ndio waeleze
Kabudi hajapeleka cheti feki au chenye utata. Yupo kwenye orodha ya ambao walipeleka vyeti pungufu. mimi sijui kama wahitimu wote walipita njia zinazofanana. Kuna wale waliopitia certificate bila secondary, kuna wa diploma bila form six na kuna wale wa direct entry yaani form 4 na six halafu university. Sasa sijui kabudi kapitia njia gani.
 
Tatizo Kuna watu wanachanganya..

Wanadhani Ukitoka 4m4 ukaenda Certificate > Diploma > Degree etc .. eti una cheti feki..hapa ndio tatizo..

All in all waache kupiga kelele, Aoneshe Vyeti Yaishe..
Au na yeye aende Kanisani akalie na aseme anamuachia Mungu..
 
Apeleke cheti husika kioneshwe tuelewe ukweli,tena yeye ana bahati wengine hata hawatasikilizwa.
 
Wanashangaa nini, inawezekana kabisa. That was the order of the day. Inawezekana alibugi form 4, akaiba cheti, akaenda form six akatambua makosa yake akasoma kwa bidii, na sasa ni Profesa!
duh we kilaza kweli, hana cheti feki....elewa maada

chako ulikichonga stationary gani, maana mnajianika humu
 
Wanashangaa nini, inawezekana kabisa. That was the order of the day. Inawezekana alibugi form 4, akaiba cheti, akaenda form six akatambua makosa yake akasoma kwa bidii, na sasa ni Profesa!
Hilo linaweza kuwa kweli, mara nyingi watu waliopitia njia hizo hawafanyi makosa kama wakibapata nafasi nyingine, huwa wanahakikisha hawafanyi makosa tena. Hebu angalia hata majina yake yalivyo mengi....Palamagamba Aidan John Mwalusambo Kabudi.
 
Habari wanaJF,

Mamlaka za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) imesema taarifa za Waziri wa sheria Profesa Palamagama Kabudi kuwa na vyeti vyenye utata sio sahihi, imetawataka wale waliohusika kufanya uchunguzi na kuotoa orodha ya majina hayo waulizwe tatizo nini mpaka Mwalimu huyo nguli wa Sheria mwenye heshima kedekede akumbwe na kashfa hiyo.

Profesa Kabudi aliwahi kuwa Dean wa Shule ya Sheria pale UDSM, Aidha kwa sasa Profesa Kabudi ni Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hapo patamu kweli.
Mungu hamfichi mnafiki! Kama Rais Magufuli na Serikali yake watamwondoa Prof. Kabudi kwenye Orodha ya vyeti veyenye utata(Incomplete) basi zoezi hili lifutwe kabisa maana halina maana, limejaa upendeleo na unyanyasaji kwa watu wa chini tu. Serikali isitake kuwadanganya Watanzania kwa mwavuli wa Kisiasa.

Hivi huyu Kabudi Palamagamba asingelikuwa ameteuliwa kwenye Ubunge na baadaye kupewa Uwaziri ina maana Chuo Kikuu UDSM wangelikanusha kuwa sio sahihi kwa Prof kuwa kwenye orodha? Hii maana yake nini kuwafanya Mabashite au Wateule wa JPM kuwa ni magenius wanapoteuliwa???

Serikali ikiri kuwa zoezi hili kwa ujumla limepoteza mwelekeo, halina weledi, ni la kionevu, kibaguzi na linaenda kuligharimu Taifa mabilioni ya fedha kwa njia moja au nyingine.
Muda utanena.
 
Back
Top Bottom