UDSM wekeni majina ya usahili kwenye website yenu

Nov 6, 2015
46
18
Baadhi ya vyuo kama SUA,UDOM sasa hivi wanaweka majina ya usahili(interview) ya nafasi mbali mbali za kazi kwenye tovuti(website) yao,tabia ya kutumia njia ya kupiga simu kuwa ndio njia pekee inakatisha tamaa waombaji wa nafasi hizo.
 
Daah! Kweli sasa unapiga simu saa 10 jioni then ni siku mbili unatakiwa uwe kwenye usaili.Imagine mtu yupo Kigoma au Bukoba.Lakini ndiyo hivyo mtaka cha uvunguni sharti ainame.Nipo Dillema hapa Nafikaje hiyo Interview usafiri wenyewe pembezoni ni majanga
 
mkuu wamesha kuita?
 
Kwa taarifa za uhakika ni kwamba walishawaita watu waliokizi vigezo na leo j3 ndo wanawafanyia interviews
 
Pia chuo cha MUHAS kilitangaza hizi academic positions, vipi nao walishaita watu kwenye usaili? Mwenye taarifa
 
Hivi kwa nn wakiita wasiwatalifu vijana kuwa hujapata ili vijana mtafute pengine
AU hata kuweka majina kwenye website yao.

Yani kuna baadhi ya vyuo/taasisi hata kuita watu kwenye interview ni siri sasa sijui kama hata hiyo haki hua inatendeka au laa.

IFIKE WAKATI TANZANIA TUBADILISHE MIFUMO YA KIZAMANI
Pongezi kwa SUA,UDOM Kwa kwenda na wakati
 
Je waliopata wameshaitwa au la? Kama unafahamu lolote tujuzane kidogo
Nilichokua nimeambiwa na chanzo cha uhakika ni kwamba mchakato mzima wa interview na kuitwa kazini ulitakiwa kuisha ndani ya mwezi wa tisa, kwasababu chuo kilikuwa kimepewa kibali cha kuajiri ambacho kilikua kinaisha tar 30 mwezi wa 9. Kwahiyo kama ni ajira watakuwa tayar washapewa tangu mwishon mwa mwezi uliopita
 
Duuuh! Kumbe wameshaita watu kazini,itakuwa style yao ileile ya kuwapigia simu nadhani.Nilishiriki usaili lakini naona kimyaaa,hope nimeshafyekelewa mbaali.
 
Daah! Kweli sasa unapiga simu saa 10 jioni then ni siku mbili unatakiwa uwe kwenye usaili.Imagine mtu yupo Kigoma au Bukoba.Lakini ndiyo hivyo mtaka cha uvunguni sharti ainame.Nipo Dillema hapa Nafikaje hiyo Interview usafiri wenyewe pembezoni ni majanga
Sasa si bora hivyo, na mtu unapigiwa simu upo porini au mashambani mtandao hupatikani, unaendelea kusubiri unaamua kuuliza kwenye magroup ya whatsapp au jf unaambiwa mbona jana ndo wamefanya, na kumbe ingekuwa kwenye mtandao kila siku asubuhi na jioni unapitia inakuwa kama dozi vile.
 
Natanguliza kuomba msamaha kwa wanjamvi wote katika uzi huu.
Awali wakati kazi zinatangazwa na mchakato mzima wa interview nilikuwa nawasiliana na mmoja wa wahusika katika zile ajira, na mpaka mwisho aliniambia kuwa washapata watu na watawaita kabla ya September kuisha, hivyo nikajua wamesha waita.
But wiki 2 zilizo pita nilikuwa pale udsm na nikakutana na yule mwalim na akanieleza kuwa
ISSUE YA KUITA WATU KAZINI BADO ILA ITAFANYIKA WAKATI WOWOTE.
Hivyo nitumie nafasi hii kuwaomba radhi watu wote ambao niliwakatish tamaa sana, niwaambie kwamba haya ni makosa ya kibinadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo watu wameshaanza kuitwa?
 
Back
Top Bottom