udsm wacharuka na kibonde...

Efraim kibonde ni mtanzania, ana uhuru wa kutoa maoni yake, wanafunzi wa udsm ni watanzania wana uhuru wa kutoa maoni yao, hatutajali ni maoni gani na yanamlenga nani isipokuwa maoni hayo yataashiria uvunjifu wa amani.........kushnei.

Awe ana gentleman division au div 1 hapa siyo hoja tunataka kujua mantiki ya hoja iliyopo na madhira yanayotokana na hayo.

Tuchape kazi wananchi mwacheni efraim na mdumange wake na udsm wakomae na wa kwao..... Tukiona side yenye mdumange wenye manufaa ya umma, let's join hand with them without shame
 
Who is Kibonde in Tz? Tumkumbuke kwa lipi? UDSM, mpuuze mtu huyu! Thats all I can say.
 
Hivi hawa wasomi walisikiaje hizi comments za Kibonde, au waliambiwa? manake siamini wasomi kama wale wanakaa kusikiliza kile kipindi cha Kibonde!!! Mtu yeyote anaye-tune radio kusikiliza kipindi cha JAHAZI au KIBONDE SHOW lazima ana walakini katika ubongo wake!! Nlisikiliza/kuangalia hivyo vipindi once kidogo nitapike...sijawahi sikiliza tena ! Vile vipindi ni vya wajinga!
 
anajidai anajua kila kitu huyu kibonde, mi simpendiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mnaosikiliza ujinga wa huyo Kibonde hebu tudokezeni amesema nini kilichowatibua wanafunzi wa Udsm. Sisi wengine hatu-tune kabisa hiyo radio.
 
wasomi ,wasomi,someni ili taifa liendeleeeeeeeeee,kila mtu ananjia zake za kutafuta kipato
ukishikilia la mwenzako,utakufa njaa!
tuwe wabunifu jamani,tuachane na kibonde.:clap2:
 
wasomi wa nchi za nje wanaspend muda wao kwenye research na ugunduzi.wasomi wa mlimani wanaspend muda wao kumdiscuss mropokaji kibonde,kuangalia pcha za ngono,man u na aseno,kukariri vitin/pamphlets na lecture notes,.HATUNA JIPYA NDO MAANA TUNAPATA MUDA WA KUDISCUSS KIBONDE.
 
Kaka nijuavyo mimi ukiwa na D mbili basi unakuwa na div 4 ya points 28 na nadhani ndio ya mwisho na ikiwa utapata D moja basi unakuwa na points 29 na unapata Div 0 sasa ikiwa ni kweli ana points 33 basi ana ziro na kama akiwa na D mbili atakuwa amepata Div 4

Nadhani wewe ndugu yangu kama una cheti ca f4 basi umenunua au umechonga! Umetia aibu sana kwenye elimu yetu!
 
wasomi ,wasomi,someni ili taifa liendeleeeeeeeeee,kila mtu ananjia zake za kutafuta kipato
ukishikilia la mwenzako,utakufa njaa!
tuwe wabunifu jamani,tuachane na kibonde.:clap2:
Anatakiwa Kibonde amind his own business ndio watu hawatamjadili lakini akiwa kimbelembele kwa kila kitu ndio maana watu wanamchukia

Angalia hapa
https://www.jamiiforums.com/tanzani...-kila-kitu-tafuta-wataalamu-wakusaidie-9.html
icon1.png
Uchaguzi 2010: Kibonde usijifanye kujua kila kitu, tafuta wataalamu wakusaidie


Katika kipindi cha Jahazi cha tar 31/8/2010 mtangazaji Kibonde amejifanya kuwa mtetezi wa JK na CCM kwa kuliponda pingamizi ya Dr Slaa na CHADEMA kuhusu JK kukiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Kwa bahati mbaya sana katika kutekeleza jukumu hilo Kibonde alizidi kudhihirisha umbumbumbu wake hadharani pale alipodai kuwa "Rais anayo mamlaka ya kuagiza matumizi ya fedha za Serikali atakavyo"

Kwa maoni yangu Kibonde ana ufahamu mdogo sana wa kitu kinachoitwa Separation of Powers between the State (Serikali), Legislature (Bunge) and Judiciary (Mahakama). Hajo ya CHADEMA katika sakata hili ni mgombea wa CCM Jakaya Kikwete na Serikali yake ni kufanya matumizi ya fedha za umma kwa kukiuka Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali. Kwa mujibu wa Katiba Bunge ndio lenye jukumu la kuidhinisha makusanyo na matumizi ya fedha za Serikali.

Kutokea mawaka 2006 TUCTA iliwasilisha madai ya nyongeza za mishahara kwa watumishi wa Serikali kufikia kima cha chini cha Shs 315,000/=.

Kutokea mwaka 2006 JK na Serikali yake hawakuchukua hatua zozote kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa maana ya kupeleka ombi kwa bunge la kufanya matumizi ya ya ziada katika kulipa mishahara ya watumishi. Hivyo Bunge la 2006, 2007, 2008, 2009 na hata la 2010 Kikwete na Serikali yake walishindwa kuwasilisha ombi hilo.

Wakati Serikali ya JK ilishindwa kuwasilisha ombi la kuongeza mishahara ya watumishi wake wanyoinge. Inadaiwa katika kipindi hicho iliwaongezea mishahara na marupurupu za viongozi waandamizi wa Serikali wakiwemo Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Majaji n.k na pia kulipa malimbikizo ya nyongeza hiyo. Kama tutakumbuka vizuri wabunge wenye jukumu la kupitisha matumizi ya Serikali walipoona vigogo wenzao Serikalini wamejiongezea mishahara na marupurupu; wabunge nao wakawasilisha mapendekezo ya kuongezewa mishahara na marpurupu na wakapata.

Ni kwanini CCM , Kikwete na Serikali yake waliamua kuwadharau wafanyakazi kwa miaka minnne kutoka mwaka 2006, na kuendelea kuwadharau hata pale walipotishia kugoma mwi 2010? Jibu walifanya hivyo kwa kuwa walijua TUCTA inaongea peke yake, haina asasi ingine ya kuisaidia hivyo Serikali itaweze kutumia vitisho kuzima jeuri ya TUCTA na Mgaya.

Kuteuliwa kwa Dr Slaa kuwa mgombea Urais wa CHADEMA kulikuja kama mshituko kwa CCM JK na watanzania walio wengi. Na hoja yake ya kwanza wakati anafanya mikutano ya kutafuta wadhamini katika mikoa mbali mbali ilikuwa kutamka wazi wazi kuwa anazihitaji kura za wafanyakazi zilizokataliwa na mgombea wa CCM Jakaya Kikwete katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salam Mei 2010, na akachapisha fulana zenye ujumbe huo.

TUCTA ilipoona imepata msemaji wa kusaidiana naye katika kudai haki za wafanyakazi zilizokuwa zikipigwa danadana kutokea 2006, haikubweteka ikatoa tamko kwa wanachama wake kuwa wampatie kura mgombea anayeonyesha kuhitaji kura za wafanyakazi, kwa kuwa haiwezekani "ukampatia pilau mtu asiyeihitaji".

Ni kutokana na pressure hizi za kuanza kwa Kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2010 CCM, Kikwete na Serikali yake wakasalimu amri na kutoa nyongeza ya mishahara kutoka Shs 135,000/= kufika Shs 235,000/= kimya kimya. TUCTA, CHADEMA na wadau wengine wakataka kufahamishwa ni nini kinaendelea ndipo Rais akajitokeza katika mikutano ya Kampeni za CCM mkoani Mwanza kudai kuwa Serikali yake inawajali sana wafanyakazi na tayari imewaongezea mishahara.

Sasa Kibonde atuambie katika mtirirko huu wa matukio, ni kweli CCM ya leo na JK wanawajali wafanyakazi? Walikuwa wapi kwa miaka minne kuwapatia wafanyakazi nyongeza hiyo?

Hoja kubwa ya Dr Slaa na CHADEMA sio wafanyakazi kuongezewa mishahara, bali wafanyakzi kutumika kama busati la kusafisha miguu na kukumbukwa baada ua upepo wa kisiasa kuwa mbaya kwa CCM na mgombea wake Jakaya Kikwete. Tujiulize kwa mtirirko uliotajwa hapo juu, iwapo vyama vya siasa vingesimamisha watu wasio makini kama Dr Slaa katika nafasi ya Urais, nyongeza ya mishahara iliyokuwa ikipigwa danadana kwa miaka minne kutoka 2006 na iliyotolewa wakati wa kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu ingepatikana?

Sambamba na hilo Dr Slaa na CHADEMA wanahaji kitendo cha Rais na Serikali yake kukikuka Kanuni na Taratibu za Fedha za Serikali. Ni ukiukwaji huu uliosababisha kuwepo kwa Kashafa ya EPA, Meremeta, Tangold, n.k.

Naomba wana JF wanaofahamu mipaka ya Rais kuagiza matumizi ya fedha za umma wakati usiokuwa wa dharura (emergency) bila ya kupata idhini ya bunge watusaidie kumhabarisha Kibonde kupitia hapa
 
Great. I salute you for clear and " no doubt" explanation.....may be jamaa kasomea Uganda ambako hatujui ukokotoaji wao upoje. Sasa ni ajabu kulinganisha Council mbili katika mataifa mawili tofauti......Challenge them and Educate them too. I like your approach.
 
Back
Top Bottom