Tanroads wana lawama ndogo sana pale. Pamoja na shimo eneo lenyewe ni straight kwa zaidi ya kilometa moja na nusu. Akili ya kawaida inagoma kabisa kuwalaum TANROADS. Ukiangalia hadi Dereva wa Basi afe ujue jamaa wa Lorry alikuja line yake tena kwa ghafla, vinginevyo dereva ninavyowajua asingekubali uso kwa uso angeamua hata kulipindusha kuliko uso kwa uso. Naamini either dereva wa lorry alisinzia au alihama ghafla wakat wako jiran na basi. Mfano wake ni umbali kati ya Fire na Pale Magomeni, eneo liko clear hamna hata kona! Kwa wanaofaham wanaweza kufafanua kile nikisemacho. Ni lorry pale ndo tatizo. Bahati nzuri nimepita pale na nmeona hali ilivyo, shimo siyo sababu hasa!