Udsm na kufukuzwa kwa wanafunzi 2000 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udsm na kufukuzwa kwa wanafunzi 2000

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Matemu, Jan 10, 2009.

 1. Matemu

  Matemu Member

  #1
  Jan 10, 2009
  Joined: Nov 29, 2007
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  UDSM NA KUFUKUZWA KWA WANAFUNZI 2000
  Utawala wa chuo kikuu cha UDSM kimetoa tamko la kuwafutia udahili wanafunzi wapatao 2000 kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu.Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Makamu mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia masuala ya Taaluma na Utafiti Prof.MABOKO hakufafanua kinagaubaga ni utovu upi wa nidhamu ambao umepelekea wanafunzi hao kutimuliwa chuoni.
  Hata hivyo si lengo langu kujadili tamko hilo bali ni kuangalia namna Utawala wa chuo kikuu UDSM kinavyotoa matamko mengi kisiasa zaidi kuliko kiutendaji.KWA NINI NASEMA KISIASA KULIKO KIUTENDAJI?

  1,Katika mgomo wa mwaka jana WAZIRI WA ELIMU Prof.Magembe alitangaza kuwafuti udahili wanafunzi wapatao 300 kwa kile kile wanachodai siku zote Utovu wa nidhamu.Hata hivyo agizo hilo halikutekelezeka kwa sababu ambazo hatukuelezwa na kuishia kusipojulikana.

  2,Siku zote Uongozi wa chuo unapotangaza kufukuza wanafunzi chuoni ama kuwafutia udahili ni kwa nini hawatangazi majina yao hadharani badala yake huishia na matamko tu ya tumewafukuza? Maboko ama Magembe wanatakiwa kuwa na majina kwanza halafu ndiyo watoe hayo matamko yao BADALA YA KUONGEA TU NA KUWAWEKA WANAFUNZI ROHO JUU NA WAZAZI WAO KWA UJUMLA.

  Ikumbukwe kuwa wanafunzi 2000 kwa chuo cha UDSM ni karibia asilimia 13% ya wanafunzi wote hivyo si jambo la mzaha la kuongea tu bila kutaja majina yao.KWA USHAURI TU KAMA WANATAKA KUTISHA WANAFUNZI NI BORA WAKATUMIA NJIA NYINGINE ZAIDI KULIKO HII YA MATAMKO YA KUFUKUZA WANAFUNZI.
   
  Last edited by a moderator: Jan 12, 2009
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Jan 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Na jana taasisi ya ustawi wa jamii umesitisha mahafali ya wanafunzi pale ghafla watu walikuwa wamejiandaa na nini
   
 3. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,262
  Likes Received: 4,236
  Trophy Points: 280
  Shy hebu tuhabarisha zaidi hapo ustawi kulikuwa na jamaa wa mwaka wa 3 Advanced Diploma waligoma wakitaka wapewe degree ,walizuia mahafali tangu mwaka jana ikahairishwa hadi mwaka huu na wao chuo kiliwaambia watafanya mitihani yao ya Advance Diploma mwaka huu
  Ni jamaa walifungua kesi mahakamani
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Bado wana chance ya kwenda mahakamani!
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Jan 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mahakamani walishindwa hao wanafunzi kama mnavyojua hiyo advanced diploma imafutwa kwahiyo wao walikuwa wanataka wapewe degree kwa sababu hiyo advaced imefutwa
   
 6. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Attached Files:

  Last edited: Jan 17, 2009
Loading...