UDSM: Mgomo unaokuja nani alaumiwe?

WAZUSHI TU!!!!!! wala watu wanaosoma mwaka wa kwanza na mwaka 1-4(llb) hawawezi kumalizia semester?? au wanatafuta supp na C kwa kupoteza muda!!!
kuna wanaotafuta sababu za kudisco, hela haitoshi sawa, lakini hili hawakuliona toka mapema? Hawa ni wasomi wanaosukumwa na njaa, mafuta ya taa yakipanda bei hawaoni, mauaji ya raia kwao siyo tatizo, kuhusu katiba mpya hakuna anayeuliza kinachoendelea
 
aah kizazi kipya cha migomo. kusoma msome bure na kero kwa taifa tena. masuala hayo ni ya kuzungumzika na siyo lazima wafanye mgomo, kwani hapo vinala wataumia
 
Spika umeongea hoja madhubuti,ila sasa mgomo kwa muda huu si muafaka kabisaaa,ingawa bodi wamewazingua,lakini kama mtachelewa field chuo kitawajibika,nakumbuka wakati nasoma tulikumbana na kadhia ya kuchelewa field,hapohapo udsm lakini wao ndio hasa waliowajibika........Suala la pili,kama watachelewesha nauli basi msiondoke kwenye vyumba,tuliwahi kufanya hiyo kitu,na utambue kuwa hela ile huwa ni kwa NAULI na kujikimu tu........
Mwishoni mwa semester iliyopita ulitokea mgomoUDSM, kilio kikiwa ni "Kupungukiwa" hela za kujikimu.WanachuoWali poozwa kwa kuahidiwa kuongezewa kiwango cha hela kwani gharama zaMaisha ni kweli zimepanda (tumesikia pia bungeni sijui ni kwa kiasi gani)!Kutuliza hali ya wakati ule,uongozi wa chuo uliamuaKutoa coupon kwa wanachuo ili angalau wapate mlo (hawakuangalia tatizo la nauli kwaWanachuo wanao ishi hostel na gharama zinginezo tofauti na kula). Hela walizo kopeshwa kwa style ya coupon zililipwa kwa kukatwa katika hela walizo wekewa mwanzoniMwa semester ya pili,hapa,tatizo bado lilirudi pale pale,kwa kulipa deni kwa hiyohautegemei hela zilizo baki baada ya kulipa deni zimfikishe mwisho wa semester ya mwisho. Kawaida hela ya field (Practical Training) hutolewa kabla ya kuanza kwa mitihani ya kumaliza mwaka.Lakini mwaka huu,bodi ya mkopo (HESLB) inataka itoe hela baada ya mitihani kumalizika.(Kwanini kubadili utaratibu bila taarifa rasmi tena kibabe hivi?)Ikimbukwe pia kwamba,wapo wanachuo wanao wahi kumaliza mitihani hivo kuondoka mapema,…Na pia,mitihani inaisha rasmi tarehe22.07.2011 na field inaanza rasmi tarehe25.07.2011,..yaani kunaSiku mbili tu kati ya kumaliza mitihani na kuanza field,….amazing.Kwa mtu anae kwenda kufanya field mwanza,kigoma,kagera,mara etc atafika lini huko?Na pia ataamini vipi kwamba atakua amepata hela hiyo tarehe 23 july,na atumie usafiri gani wa haraka,kwa kiwango kidogo cha hela anazopata kuwahi kigoma awahi field ukizingatia kwamba ukichelewa hata siku moja tu umejiondolea kiasi flani cha maksi?Ni nini kinaifanya serikali kupitia bodi iamini kwamba hela ambazo hazikutosha semester iliyopitazinatosha semester hii ukizingatia kwamba hela hizo hizo zilikatwa deni la coupon la semester iliyo pita? Kwa kifupi,hela ya field pamoja na kwamba inawasaidia wale walio wahi kumaliza mtihani kuondoka mapema,ina saidia pia kuwapa support wale ambao wameishiwa hela katika mda mbaya kama huu wa kuingia katiaka mitihani ambapo mtu hahitaji stress za vipi atakula leo.Jana tumeenda bodi ya mkopo hawa kutusikiliza,leo tumetaka kufanya kikao cha bunge tumenyimwaVenue,utawala wanajua kabisa kwamba tunataka kubariki mgomo,lakini hawa saidii kituKutunyima venue,maana tunaipisha tu siku ya leo kama sikukuu na kesho kama wanachuo hawajapewaHaki yao basi na tubariki mgomo kupitia revolutionary square,…Hadi hapo kesho,tunasubiri kudai haki.Waziri *soma pia: Home
 
Na wewe si ulikuwa unalaumu grades za nauli au umesahau????njaa haikugusi????
kuna wanaotafuta sababu za kudisco, hela haitoshi sawa, lakini hili hawakuliona toka mapema? Hawa ni wasomi wanaosukumwa na njaa, mafuta ya taa yakipanda bei hawaoni, mauaji ya raia kwao siyo tatizo, kuhusu katiba mpya hakuna anayeuliza kinachoendelea
 
kuna wanaotafuta sababu za kudisco, hela haitoshi sawa, lakini hili hawakuliona toka mapema? Hawa ni wasomi wanaosukumwa na njaa, mafuta ya taa yakipanda bei hawaoni, mauaji ya raia kwao siyo tatizo, kuhusu katiba mpya hakuna anayeuliza kinachoendelea
Hakuna watu wanaonikera kama watu hawa wahamasisha migomo wasiokuwa na akili! Nina wasiwasi sana na elimu yao wanayoipata! Wao wanachoangalia ni masilahi binafsi (kama wabunge wa ccm), hawawezi kupambana kwa ajili ya watz waliowengi ambao wanaishi vijijini wakitegemea mafuta yao kuwasha vibatari wakati huo serikali inapandisha bei ya hayo mafuta. Hawagomei wachimbaji wa uranium yetu kule dodoma ambayo inatupatia only USD 5m per year wakati huo wawekezaji wakichukua about USD 200m per year! Huu ni ujinga kwa hawa wasomi wanaotumia miguu kufikiria badala ya kutumia akili. Swali hapa ni je, kwenye mkataba waliosaini hawa wanachuo na bodi ya mkopo uliainisha kutolewa kwa pesa wiki mbili kabla ya kufunga chuo!? 'SHAME ON YOU STRIKE ORGANIZER'
 
hapo umenena madai yapo ila hayana mashiko kwa wakti huu.nlipenda sana mgomo ila kwa hili nsingekubali
kuna wanaotafuta sababu za kudisco, hela haitoshi sawa, lakini hili hawakuliona toka mapema? Hawa ni wasomi wanaosukumwa na njaa, mafuta ya taa yakipanda bei hawaoni, mauaji ya raia kwao siyo tatizo, kuhusu katiba mpya hakuna anayeuliza kinachoendelea
 
Na wewe si ulikuwa unalaumu grades za nauli au umesahau????njaa haikugusi????
kwa hiyo njaa ikinigusa natakiwa kugoma? Hii bado hailalishi grades katika nauli,, vilevile sijawa kilaza wa kufikia hatua ya kusahau ninachokiandika.
 
ile ela ya coupon kumbe ilikuwa ni mkopo. basi inabidi wawape coupon tena, safari hii iwe bure.
 
Hahahahaaaaaa......tena mwaka wa 3 wanapaswa waje walipe watakapofata TRANSCRIPT maana wao ndo wanamaliza,au walipie wakati wa MAHAFALI
ile ela ya coupon kumbe ilikuwa ni mkopo. basi inabidi wawape coupon tena, safari hii iwe bure.
 
Wadau kuna kila dalili UDSM wanaweza kuanzisha mgomo na maandamano kuanzia sasa,kwa sasa wanachuo wapo eneo la revolution square wanapeana modalities.CHANZO cha mgomo ni kutotolewa kwa pesa ya field,ambapo wanafunzi wanatarajia kufunga chuo kwa muda wa wiki mbili zijazo lakini mpaka sasa bodi ya mikopo hawajatoa pesa hizo.
Kweli kuongoza nchi ya watu wenye njaa, ambao mifukoni jua linawaka, ni kazi kwelikweli. Wanaweza hata ku chabo watoto wako wanakula nini. Lo! JK una kibarua kigumu.
 
UDOM wamegoma baada ya kudanganywa kupewa hela ya field ila serikali kwa kuwatimua kwenda nyumbani so nawaomba ndugu zangu msishindane na magamba plz.
 
speaker ongea na wenzako na mkae kitako mfikirie vizuri sio kukurupuka tuu oooooooooooh tunagoma.hao bodi ya mikopo hawajakataa kuwapeni hela, subirini muda ufike muone kama hamtapewa, muwe mnastrike kwa vitu kama;
1 kupandishwa kodi mafuta ya taa ( sababu ndo kule kijijini kwetu tunayatumia kwa asilimia mia moja)
2. mchakato wa kaitiba mpya.
3 . kushuka kwa thamani ya sarafu yetu.
4 mauaji ya raia kule mwanza,arusha na mbeya.
5. kumtaka waziri mkuu (pinda),spika wa bunge(bkiroboto) nepi, na mapacha watatu( el, ra.ac) jk wajiuzuru.wakipishe chama chao kijivue gamba vizuri
6 zahanati kule kushimundu hakuna na vijiji vingine vyote.
na mengine mengi ambayo unaweza kuorodhesha mpaka modem ikaisha voucher.
ilo sula mnalotaka kugomea limekaa kiubinafsi zaidi na sio kwa watanzania wote.

behave basi.
 
Hakuna watu wanaonikera kama watu hawa wahamasisha migomo wasiokuwa na akili! Nina wasiwasi sana na elimu yao wanayoipata! Wao wanachoangalia ni masilahi binafsi (kama wabunge wa ccm), hawawezi kupambana kwa ajili ya watz waliowengi ambao wanaishi vijijini wakitegemea mafuta yao kuwasha vibatari wakati huo serikali inapandisha bei ya hayo mafuta. Hawagomei wachimbaji wa uranium yetu kule dodoma ambayo inatupatia only USD 5m per year wakati huo wawekezaji wakichukua about USD 200m per year! Huu ni ujinga kwa hawa wasomi wanaotumia miguu kufikiria badala ya kutumia akili. Swali hapa ni je, kwenye mkataba waliosaini hawa wanachuo na bodi ya mkopo uliainisha kutolewa kwa pesa wiki mbili kabla ya kufunga chuo!? 'SHAME ON YOU STRIKE ORGANIZER'
Yea, tell them, these are the scholars we are to rely on. Well, their academic background and also their intellect must be questionable !
 
Back
Top Bottom