UDOSO yaanza kusaka wanafunzi machangudoa

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,000
[h=2] [/h] Debora Sanja, Dodoma


SERIKALI ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO), imeanza uchunguzi ili kuwabaini wanafunzi wa chuo hicho, ambao wanajihusisha na biashara ya ngono. Viongozi hao wamefikia hatua hiyo kufuatia taarifa iliyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari wiki iliyopita kuwa, baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wanajiuza.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa UDOSO, Yunge Paul alisema, tayari kazi hiyo imeanza na watakaobainika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Alisema wanafunzi hao, wanashusha heshima ya chuo hicho kikubwa na kama taasisi ambayo imebeba wasomi wengi.

Alisema taarifa ya kashfa ya ngono, iliyoripotiwa na vyombo vya habari imesononesha nchi nzima ikiwemo uongozi wa chuo, wazazi na wanafunzi.

“Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kwa kweli, imesononesha nchi nzima ikiwemo UDOM yenyewe, wanafunzi wakiwemo wanafunzi wakina dada,” alisema.

Alisema taarifa hiyo, haikutoa uzito na ushahidi wa kutosha kuwa wanafunzi wa chuo hicho wanajiuza na wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali za starehe mjini Dodoma.

“Tunaomba vyombo vya habari, vilivyotoa taarifa hiyo warekebishe, ili kurudisha heshima na imani kwa Chuo Kikuu cha Dodoma,” alisema Yunge.

Alisema wakati taarifa hiyo, inatolewa katika vyombo vya habari mji wa Dodoma ulikuwa na watu wengi na kuwa inawezekana walioonekana kufanya vitendo hivyo sio wanafunzi wa chuo hicho.

“Mwanafunzi wa UDOM, anajulikana kwa kitambulisho chake na inawezekana mtu yeyote akajitambulisha anatoka katika chuo hiki kama ushahidi wa wanafunzi upo tuletewe,” alisema.
 

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
965
500
Matatizo ya wanafunzi ni geniune kabisa,watoto wanatoka huko mikoani hawana kitu lakini wakiwa wananjozi kwaajili ya maisha yao, wanapewa mikopo nusunusu,wengine hakuna mikopo then wanaopewa mikopo ni wale wenye uwezo.So ili watoto wafanye kilichowapeleka Vyuoni ni pamoja kuwapa stahili zao kwa usawa.Wapewe mikopo kwa asilimia mia wote then waanze uchunguzi wao ili kubaini wanaojiuza na ndipo wawachukulie hatua za kinidhamu kwa wale watakaobainika vinginevyo ni uonevu.
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,217
2,000
Sheria zinasemaje?
Kuna sheria inayozuia mtu kufanya umalaya?

utajuaje mtu anajiuza? kwa kuvaa? kwenda club?
 

mwita ke mwita

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
7,763
2,000
UDOSO hawana mamlaka kikatiba kusaka malaya mitaani na wenyewe huenda kuna malaya sasa watasakaje malaya, wenyewe washughulikie BOOM na wanafunzi kusoma vizuri
 

Sabry001

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,064
1,195
Hv kwani dodoma wanafunzi waliopo ni wa UDOM tu? Why mnakichafua chuo chetu kwa taarifa zisizo na uhakika bhana? Kila ubaya mwawatupia udom, vilaza wao, wadini wao sasa mmehamia kwenye ukahaba jamani! Ingekuwa vyema wanahabari mjifunze kutoa taarifa accurate kupunguza mkanganyiko miongoni mwa jamii. Penye wengi kuna mengi hvo sitaweza kataa uwepo wa makahaba huku dodoma au udom bt next time waonyesheni nyuso zao, id zao km wanazo na sio kupiga picha miguu ya watu wamevaa vimini tena walio ktk burudan zao, club au sherehe afu mnawaita wa UDOM! Huo ni ukanjanja ktk reporting!
 

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,301
2,000
Watuachie vipoozeo vyetu bana wasiwaguse siye madomo zege roho zetu kwatu
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
13,304
2,000
Wengi tumepitia Vyuoni siamini km kuna Mwanafunzi wa UDOM ana paper jumatatu asubuhi atathubutu kulala na na mtu kwa sh 500/ halafu asubuhi apande daladala ya 500/ hadi Education kuwahi paper
Nina wasiwasi na mtoa Mada wa Star tv hawajui wanachuo au alikataliwa na vyangudoa waliopo hapa Mjini akaamua kuwatosa au alinyang'anywa Disco
Kwa nini asiwatoe live kwani Picha tulizoziona sio za Kumbi za Disco za Dodoma angefunguka zaidi, waacheni hao watoto wana stress zao baada ya migomo ya mara kwa mara mnawaanzishia nyingine
 
  • Thanks
Reactions: Mto

Nyakipambo

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
435
0
Kweli UDOM bado ni chuo cha kata. Mtu mzima unataka kumpangia autumiaje mwili wake? Pumbaf kabisa hawa hawana kazi ya kufanya
 

Also me

Member
Aug 17, 2011
67
70
hata kama ni kwl, xwal la kujiuliza ni kwamba swala la watoto wa kike kujiuza dodoma limeanza wiki jana au lilikuwepo kabla, na nyie UDOSO achen kujichukulien umaaaruf mmeshindwa kushughulikia matatizo mangapi ya msingi ya wanafunzi katika chuo chenu?!......... hadi muweze hili ambalo haliwahuxu au ndo kutafuta publicity?!.........
 

kbosho

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
13,018
2,000
Mbona wanajulkana...na wanakoshda c mastr pub, cafe latino, free point na ktuo kikuwa loyal vllage na unq pub!....na wateja wakubwa ni wafanya biashara, walimu tena wa udom, wafanyakaz wa LAPF,CRDB,NMB,VODA,TGO,CCM, na wagen wanao kuja kwenye mikutano dodoma! Vdada vyenye ni vdogo vdogo af vzur ajabu
 
  • Thanks
Reactions: Mto

kbosho

JF-Expert Member
Jun 4, 2012
13,018
2,000
Mbona wanajulkana...na wanakoshda c mastr pub, cafe latino, free point na ktuo kikuwa loyal vllage na unq pub!....na wateja wakubwa ni wafanya biashara, walimu tena wa udom, wafanyakaz wa LAPF,CRDB,NMB,VODA,TGO,CCM, na wagen wanao kuja kwenye mikutano dodoma! Vdada vyenye ni vdogo vdogo af vzur ajabu....
 

Mjanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
1,239
1,225
Hivi kazi za Msingi za UDOSO ni zipi?? magamba walishawaingilia tayari hawa!
Chuo Kikuu siyo mahala pa kukurupuka na kutoa kauli zisizo na mashiko kama hizo!
Lazima ikumbukwe wale ni wananzuoni na siyo wanafunzi, vilevile wote wameshafikisha
umri wa miaka 18 au zaidi-umri ambao kila mmoja wao anaaminika kuwa mkomavu
kiakili,kimawazo na kimwili, hivyo maamuzi yoyote wayafanyayo yanakuwa yamefikiriwa
vizuri! naamini hakuna anayerubuniwa ili akajiuze!
UDOSO, DARUSO na wengine wanapaswa kusimamia haki na maslahi ya wenzao ili
waweze kusoma na kutimiza ndoto zao katika mazingira rafiki, haya mengine wawaachie wanasiasa!
 

BUMIJA

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
4,445
2,000
Maana ya chuo kikuu nini??UDOM Kuna parade?Mnagongewa kengele?Kila mtu kilichompeleka anakijua:::::Mambo ya kujiuza yalianza Zamani ndo mnajua leo;;;;vyuo vingi wanajiseli:::usbnyeze
 

Imany John

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
2,921
2,000
kunatofauti gani na kusema UDOSO imeanza kuulizia rangi ya mkaa.
Je nikweli hawaijui?
 

salosalo

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
584
500
wanawasaka ili wakisha kuwabaini kila mmoja awe anawachapa nao kwa muda wake. Najua wamejuta kwa kusema alah! tunahangaika kwenda mbbali wakati wako haphapaaribu!!!
 

Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
15,034
2,000
Eeeh Mungu! Loan board nao wanachangia, wahamisha mikopo wote bado! Wale wapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom