Badala ya kushindana nani zaidi, ni bora mkaunganisha nguvu kutatua matatizo yanayowahusu wote kama mikopo. Kumbuka ukikaa karibu na ua waridi utanukia, lakini hautakuwa ua waridi. Hata ungekuwa uko Harvard au MIT, bila jitihada binafsi ni kazi bure, kama vile kuishi karibu na sinagogi-si lazima uwe Kuhani.