nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Na Heckton Chuwa, Moshi
SIKU chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) kutangaza maandamano ya nchi nzima kupinga mchakato unaoendelea wa muswada wa katiba nchini, kundi moja la wasilamu limeonya uamuzi huo usifanyike Dar es Salaam kwa madai ya kwamba una agenda ya kumngoa Rais Jakaya Kikwete ikulu.
Onyo hilo limetolewa na Amir wa Vijana wa Kiislamu, Shekhe Shaban Mapeyo, wakati akihutubia kongamano la waislamu lililofanyika mjini Moshi, mkoani
Kilimanjaro, jana.
CHADEMA wamekuja na agenda mbalimbali wakidai ni za kisiasa na wengi tumeamini hivyo, ukweli ni kwamba wana agenda ya siri wao na maajenti wao tangu mwanzo kwa njia mbaalimbali kama vile Dowans na sasa wameikomalia hii ya katiba mpya, hili waislamu tusilikubali wakija huko mikoani wakataeni.
"Sisi Dar es Salaam tunawasubiri watakutana na nguvu za wenye historia ya Tanzania, alisema Shekhe Mapeyo huku akishangiliwa na umati wa waliohudhuria kongamano hilo.
Alisema agenda ya katiba inayotumiwa na CHADEMA kwa madai ya kutumia nguvu za umma ni danganya toto, lengo halisi ni kumngo Rais Kikwete ikulu na kwamba waislamu watapambana kwa hali na mali kuzuia uovu huo kwa niaba ya Watanzania wote.
Shekhe Mapeyo alisema kuwa waislamu wamekuwa wakinyamaza kwa kila jambo wakati ajenda zikiibuliwa na vyama mbalimbali vya siasa lakini kwa sasa wameamua kusimama kidete baada ya kuona CHADEMA wamekuja na ajenda ya kutaka 'kuhatarisha amani ya nchi'.
Sheikh Mapeyo alisema, Meseji zimesambazwa zinazohamasisha watu wajiandae kumngoa Mujahidina Ikulu na sisi tunajiuliza Rais Kikwete ni Mujahidina tangu lini? Maana sisi tunachojua ni kiongozi wa wananchi wa Tanzania anayefanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa, alisema Sheikh Mapeyo.
Kuhusu madai ya CHADEMA kuwa wanahangaikia katiba mpya kwa niaba ya Watanzania wote, Sheikh Mapeyo alisema kuwa huo ni uzushi kutokana na jinsi viongozi wa chama hicho wanavyotaka katiba hiyo ipatikane kwa haraka tena ndani ya miezi sita tu.
Jamani mchakato wa kutafuta katiba mpya si mwepesi na wa haraka tena kwa miezi sita tu kama wanavyotaka wenzetu hawa, nia yao hii ni hatari kutokana na umuhimu wa katiba ya nchi; katiba inayopatikana kwa muda wa miezi sita ni ya nchi ya watu waliochanganyikiwa, kunahitajika umakini wa hali ya juu kwenye swala kama hili, alisema.
Kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ya CHADEMA iliyonadiwa na mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa mwaka jana, chama hicho kilipanga kuanzisha mchakato wa kuandaa katiba mpya ndani ya siku 100 (siku 100).