Udini wapenyezwa madai ya katiba; Maandamano yasifanyike Dar madai ni agenda ya kumng'a Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udini wapenyezwa madai ya katiba; Maandamano yasifanyike Dar madai ni agenda ya kumng'a Rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Heckton Chuwa, Moshi

  SIKU chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) kutangaza maandamano ya nchi nzima kupinga mchakato unaoendelea wa muswada wa katiba nchini, kundi moja la wasilamu limeonya uamuzi huo usifanyike Dar es Salaam kwa madai ya kwamba una agenda ya kumng’oa Rais Jakaya Kikwete ikulu.

  Onyo hilo limetolewa na Amir wa Vijana wa Kiislamu, Shekhe Shaban Mapeyo, wakati akihutubia kongamano la waislamu lililofanyika mjini Moshi, mkoani
  Kilimanjaro, jana.

  “CHADEMA wamekuja na agenda mbalimbali wakidai ni za kisiasa na wengi tumeamini hivyo, ukweli ni kwamba wana agenda ya siri wao na maajenti wao tangu mwanzo kwa njia mbaalimbali kama vile Dowans na sasa wameikomalia hii ya katiba mpya, hili waislamu tusilikubali wakija huko mikoani wakataeni.

  "Sisi Dar es Salaam tunawasubiri watakutana na nguvu za wenye historia ya Tanzania,” alisema Shekhe Mapeyo huku akishangiliwa na umati wa waliohudhuria kongamano hilo.

  Alisema agenda ya katiba inayotumiwa na CHADEMA kwa madai ya kutumia nguvu za umma ni danganya toto, lengo halisi ni kumng’o Rais Kikwete ikulu na kwamba waislamu watapambana kwa hali na mali kuzuia uovu huo kwa niaba ya Watanzania wote.

  Shekhe Mapeyo alisema kuwa waislamu wamekuwa wakinyamaza kwa kila jambo wakati ajenda zikiibuliwa na vyama mbalimbali vya siasa lakini kwa sasa wameamua kusimama kidete baada ya kuona CHADEMA wamekuja na ajenda ya kutaka 'kuhatarisha amani ya nchi'.

  Sheikh Mapeyo alisema, “Meseji zimesambazwa zinazohamasisha watu wajiandae kumng’oa Mujahidina Ikulu na sisi tunajiuliza Rais Kikwete ni Mujahidina tangu lini? Maana sisi tunachojua ni kiongozi wa wananchi wa Tanzania anayefanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa,” alisema Sheikh Mapeyo.

  Kuhusu madai ya CHADEMA kuwa wanahangaikia katiba mpya kwa niaba ya Watanzania wote, Sheikh Mapeyo alisema kuwa huo ni uzushi kutokana na jinsi viongozi wa chama hicho wanavyotaka katiba hiyo ipatikane kwa haraka tena ndani ya miezi sita tu.

  “Jamani mchakato wa kutafuta katiba mpya si mwepesi na wa haraka tena kwa miezi sita tu kama wanavyotaka wenzetu hawa, nia yao hii ni hatari kutokana na umuhimu wa katiba ya nchi; katiba inayopatikana kwa muda wa miezi sita ni ya nchi ya watu waliochanganyikiwa, kunahitajika umakini wa hali ya juu kwenye swala kama hili,” alisema.

  Kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi ya CHADEMA iliyonadiwa na mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa mwaka jana, chama hicho kilipanga kuanzisha mchakato wa kuandaa katiba mpya ndani ya siku 100 (siku 100).
   
 2. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hivi maimam wa zanzibar wanaona matamko ya wenzao wa bara?
   
 3. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wakati mwingine watu huwa wanatafuta tu wengine waseme! hapa waislamu tukiambia shule na uelewa wetu ni mdogo! tutasema tumetukanwa! Kwa mawazo kama haya mtu akiambia mawazo yake ni ya shule ya kata, atawezaje sema ametukanwa!
   
 4. k

  kibokogiziba Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nina wasiwasi unaposema waislamu tukiambiwa "kwani muislamu hawezi kumkosoa mwenzie jamvini " kama hapa kasome pia dini ujue waislamu wanatumia njia gani kuambizana mambo yao. Nahisi umeongea kama mamluki anaewasilisha kundi. hata mwislamu akikosea vipi haambiwi makosa jamvini, kasome sira ya mtume SAW vinginevyo tumiwa salama
   
 5. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tafadhali mwanaharakati wa kiislamu Prof.Safari tushauri tumekosea wapi? mpaka tupewe kauli hizi nchi hii inahitaji amani hivyo lazima tuheshimiane vinginevyo hivi vikundi vya ccm ndani ya misikiti vitatuponza...........
   
 6. w

  warea JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe kikwete ni rais wa waislam tu! Hakuna mkristu CCM? Kwa hiyo kuipinga CCM ni kuupinga uislamu? Inawezakana maana mwenyewe katulia kama mtungi, amewaachia maimam wapambane na CDM - kwa matamko na sasa wapambane mtaani kwa mapanga!

  Nani anaweza kuwakemea watu wanaochochea machafuko ya kidini kama si rais na mawaziri husika?
   
 7. m

  magiri Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  serikali kwa makusudi ianze kutoa onyo kwa wanaojiita waislamu. nasema wanaojiita kwa sababu waislamu na uislamu wa kweli hata nasi tunaufahamu. haiwezekani watu waache kutumia haki yao ya kidemokrasia eti kwa sababu ya tishio la wanaoojiita waislamu. kama maandamano wanayoyapinga si halali kuna vyombo vya kisheria vinavyohusika na hayo. wao ni nani hata wazuie maandamano? ni polisi, mahakama au ? labda mimi nitoe ufumbuzi wa matatizo ya hao wanaojipa cheo cha uislamu. kama wanadhani kukosoa serikali ni kupinga hicho wanachoita uislamu wajue kabisa kwamba hii siyo nchi ya kiislaam na serikali iliyoko madarakani si ya kidini kabisa. wajuepia kwamba rais wanayedhani wanamtetea sote tunajua kwamba haongozi msikiti hata asipingwe na labda kukosolewa pale inapobidi. na kama wanafikiri kwamba huyo ni sheikh asiyesitahili kupingwa, basi wamshauri ajiudhuru madaraka yake waone kama tutamfuata kumpinga kwenye msikiti watakaomfungulia. tunakerwa na watu wanaotaka kutumia udini kama kinga ya kutaka tusiwasahihishe na ikibidi kuwapinga viongozi wazembe na mafisadi. lugha ya kujifanya vidume na walinzi wa serikali acheni. nyie ni nani hata muwe walinzi wa serikali? kwa sisi tunaoelewa uislamu huo siyo uislamu bali mnatumiwa na watu wenye ajenda yao hasa ya kutaka kuzima vuguvugu la watanzania juu ya kuiwajibisha serikali ambayo ipo ili kuwatumikia. hivi hao mnaotaka kuwazuia wasiandamane nao wakisema hawawatambue ninyi nao wakajibu, hamjaatarisha amani? jk hawezi kuwatumia ninyi hata kama hataki hayo maandamano. si ana majeshi yake na vyombo vinavyoilinda serikali? nyie ni nani? acheni kutumiwa.
   
 8. shemasi

  shemasi Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  udini sio mzuri na utaliangamiza taifa letu kama hatutakuwa makini.
  Roho hii si njema na yatakiwa kukemewa sana
   
 9. EZZ CHEZZ

  EZZ CHEZZ Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hivi hizo ajenda za chadema za siri ni zipi?kwa nini zifahamike kwa ccm na mashehe tu?hao wanapoongea hayo maneno hayo huwa wanazi un-install kwanza akili zaoanyway,ngoja niendelee na mambo mengine ya msingi
   
 10. E

  Egyptian Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo kuna wa2 hawafikiri japo ni wasomi na wana maGPA makali lakini vilaza.Wanajisifu kuwa niwasomi lakini hizo GPA niza kutazamia.M2 wa namna hii hafikili ila bendera fuata upepo.Waislam kuzungumza hayo ya agenda za cdm hatujakurupuka system yote tunaijua! Pangeni mnachopanga tutajua 2.Hatuzungumzi bila ushahidi.Nendeni kwanza mkarejee nyaraka zenu na ndio mkanushe.
   
 11. V

  Vam Member

  #11
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu kibaya sana kama kuwa masikini wa akili,fikra na mawazo endelevu.Utatumika kwa kila jambo la kipuuzi na la kifedhuri,utatoa matamko ya ovyo kama ZUZU ili mradi uhararishe Ujinga wako mbele ya macho na masikio ya wajinga wenzako.Fikiria kwanza kabla ya kuzungumza ujinga na upuuzi wako mbele ya kadamnasi ya Watu,hata kama ni Wajinga wenzako.Siyo kila jambo unalitolea Tamko

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 12. M

  Mmbwanga Member

  #12
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani Wakristo waliopo CCM na serikalini wasimame wamwambie Bosi wao mkakati huu sio kila mtu ana akili kwa hiyo ataupuuza. CHADEMA ndiyo mwaasisi wa Orodha ya aibu na kuna Wakristo wengi tu mule. Tunapochukia Chenge, Yona, Mramba na Lowasa sio kwa Ukristo wake wala Usukuma wake ila ni kwa ukosefu wake wa maadili. Kikwete ndio mhandisi wa mradi huu wa kipuuzi. Inatosha sasa. Ina maana kina Yona, Mramba na Mgonja wameshtakiwa kwa kuwa ni wakristo na Kikwete ni muislamu?
   
 13. mtoto mpole

  mtoto mpole JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 679
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hii hapana kwa kweli yaan sijui kwanini hivi? unajua saa ingine sisi waislam tuamke na tujue inakuaje sio kushabikia tuu sababu shekhe kasema na kupinga kila kitu ambacho mtu yupo sawa ila tuu kwa vile ni mkristo...sio vizuri hata tuamke na kusoma alama za nyakatii....kiukweli Jk nchi imemshinnda so we better unite without looking itikadi za udini.....kwenye haki ukristo na uislam ukae pembeni...afu si waislam sijui tupoje jaman Mungu atusaidie tuone mwishowe itakuaje...
   
 14. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi nafikiri huyu sheikh anaumwa siyo mzima,ana kaugonjwa ka kichaa, hivyo asamehewe tu akipona hatafanya hivyo tena, kwa kuwa atajua tz haina dini na watz wanashirikiana kila siku bila kujali itikadi zao za dini wala siasa.
   
 15. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kweli Tanzania kuna vituko. Siku hizi Amr wa vijana wa Kiislam naye ni sehemu ya dola? Au ndo mkakati wa nchi kuendelea kuongozwa kwa mazingaombwe ya Sheikh Yahya Hussein!!
  TOBA.
   
 16. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kama hilonikweli ninaimani kunavyombo husika nakamamebahatika kuzipatahizo data wapeniwahusika wazifanyiekazi kwahiyopicha hatuna sirikali nyiendosirikali? Kumbuka tz hatuna silikali ya dini munatupereka wapi mungu ni umoja&upendo dini isiwe chanzo chabinadam kufarakana yanayopigiwa kerere yanatugusa wadinizote hata wapagani kwamwenye busara tumshauli raisi wetu azifanyiekazi kelo mheshimiwa jk siwakikundi furani hakuingia ikuru kwanguvu yadini mkiliendekeza hili itaonekana waumini wa dini furani hawafai kushika madaraka ya uraisi waowanageuza ikuru ni yaimaniyao ilosisahihi ninaimani kuipigia silikali kerere sikuupigiya usiramu raisi ni mwisiramu sirikali si yakiisiram
   
 17. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haya ndio matunda ya JK alipotangaza kwamba eti kuna udini na anapambana nao! Wenye akili zilizofunikwa na vibaraghashia wakaidaka ajenda hiyo wakimaanisha kwamba JK kupata anguko la kishindo mpaka ilibidi ajazilize kura za kuchakachua kwenye uchaguzi wa 2010 lilisababishwa na kwamba alipingwa "kwa sababu ya uislamu wake!" Wenye akili zilizofunikwa na vibaraghashia walisahau kwamba hata mwaka 2005 JK alipopata ushindi wa 80% wakati wa uchaguzi mkuu alikuwa bado ni Mwislamu! Sasa uislamu wa Kikwete (Chaguo la Mungu?), 2005 ulikuwa tofauti na 2010?
  Kwa nini kushindwa kwa mtu kunahusishwa na dini yake lakini mafanikio hayahusishwi na dini hiyo? Kwa nini Waislamu hawaangalii ufisadi kwamba ndio sababu hasa ya kushindwa kwa JK, wanakimbilia kumvalisha "gamba la dini" isivyostahili? Kwani Kikwete ni Rais wa Waislamu tu? Kwa nini wengine wasiokuwa Waislamu hawaoni kama uislamu wa Kikwete umemponza? Why, why, why?
  Mbona future ya nchi hii iko mashakani wandugu?
   
 18. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wewe ni "mtoto mpole" ila una akili kuliko sungura mjanja! I am impressed by your analysis.
   
 19. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Tatizo mnang'ang'ania elimu ahera peke yake. Kama mufti mwenyewe ni darasa la saba mnadhani hapo kuna uongozi bora au bora viongozi. Halafu mnajidanganya kuhusu historia ya nchi wakati mnajua fika kuwa maeneo yenye waislam wengi ndio maeneo ya watu waoga na ndiko wengi walishindwa kupambana na waarabu wakakamatwa kuwa watumwa. Je huo uoga umewaishia leo hii mnajifanya kututisha sisi watanzania shupavu ambao kwetu vita ni vita tu, hata ukiibiwa kuku. Mtaweza kweli kupambana au mnafikiri kwa kuwa tumekaa kimya ni wajinga? Tumechoka na vitisho vyenu waislamu. Jibu hoja kwa hoja. Kakobe akiongelea siasa mnamuandama hadi misikitini wakati nyie kila siku mnashiriki katika siasa.
   
 20. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,127
  Likes Received: 3,315
  Trophy Points: 280
  if it's true then hawa jamaa...must be very ignorant and some shit.
   
Loading...