Watanzania wengi bado tukiwa hatuelewi ni sababu zipi hasa zilizopelekea kutokea kwa machafuko ambayo hayakupishana muda na siku .wengi bado tuko gizani ni madai gani hasa ya msingi yanayotakiwa yafanyiwe kazi kwa pande zote mbili .tunashauku ya kujua kutoka zanzibar hadi bara .nawakilisha.
Mkuu
Kuujuwa ukweli unahitaji hekima busara na maono
Inahitaji upendo na imani ya kweli kutoka moyoni sio imani ya makanisani au misikitini.
Inahitaji usiwe mnafiki wala mkurupukaji, bali uongozwe na hekima na zaidi utanzania
Tatizo ni kubwa na source zipo wazi.
UCHOCHEZI- chuki zimepandikizwa na kukomaa sasa ni wakati wa mavuno
CCM & Kikwete - Uchochezi
Cuf & Uamusho - Uchochezi
Ponda na redio Imani - Uchochezi.
Udhaifu wa Rais - Hana maamuzi, hana vision wala hofu ya mungu (Ufisadi, mfumko wa bei, ukandamizaji wa demokrasia nk)
Mambo ya msingi na faida kwa watanzania kama elimu bora, afya bora, miundombinu bora, katika kuliletea heshima taifa
letu la Tanzania kama watanzania bila kujali itikadi zetu tumeviweka pembeni kabisa.
Mambo ya kipuuzi na yasiyo na tija kwa ustawi wa taifa la watanzania, ndiyo kigezo cha fujo na vurugu zote Tanganyika
mpaka visiwani.
CCM na kikwete - Siasa za maji taka Udini, Ukanda, ukabila nk lengo kuwagawa watanzania ili wabakie ikulu.....
CUF & Uamsho - Hawa wanatumia kila njia salama ama najisi kuhakikisha wanaipata zanziba kama taifa nje ya muungano
Ponda na Redio imani - Kila siku ni udini Nyerere, Udini - Necta, Udin - mgawanyo wa madaraka, Udini - huduma za kijamii MoU.
Unapokuwa na kiongozi anaefurahia kukuwa kwa pengo kati ya walionacho na wasionacho(masikini), asie chukuwa hatua
dhidi ya mafisadi, mfumko wa bei, huduma duni za afya, elimu na miundombinu inajenga chuki na hasira miongoni mwa
watanzania masikini. Chuki na hasira hizi huelekezwa popote palipo na sababu ilimraji jipu hupasuka popote pale.
Haya makundi manne yamejenga tofauti za kimtazamo ndani ya vichwa vya watanzania na kuwafanya kuchukiana bila sababu. Kwa sasa imekuwa kutafutwa sababu ya aina yoyote ile na watu kutoa hasira zao kutokana na UCHOCHEZI na mahubili yahayo makundi manne.
Hata hapa katika kuchangia, kila mtu atakuja na mtazamo wake na hakika mitazamo mingi itaegamia udini na kuacha
ukweli, na kwasababu watanzania hatutaki kuukubali ukweli basi lazima tuingie machafukoni, tukimwaga damu kama ilivyo
kwa wasomali nk labda mungu anaweza kuturudia.
Mungu ibariki TANZANIA.