Udini ukabila na taifa maskini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udini ukabila na taifa maskini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngagarupalu, Oct 13, 2012.

 1. Ngagarupalu

  Ngagarupalu Senior Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Nchi ya Tanzania inakadiliwa kuwa na idadi watu wapatao million 44 ( japo tunasubiri matokeo ya sensa ya 2012 yenye utata). Nchi hii inakadiriwa kuwa na makabila yapatayo 121 au zaidi. Ina madhehebu ya dini yasipungua 50 ( yakigawanywa kwenye makundi makuu matatu, ukristo, uislam, na upagani. Ingawa ndani ya haya makundi kuna madhehebu isiyopungua matano.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Makundi mawaili ya uislam na ukristo yamekuwa kwenye malumbano kwa muda sasa na kujiona kama yapo juu hata ya sheria na kama yenyewe ndo yana mungu wao, yana haki ya kuwambia wengine ubaya wao, uzuri wa mungu wao, kushiriki kutunga sheria za nchi, pengine kuzingatia dini zao na hata kutaka kuchukua dola na kuongoza, na hivyo kusahau kuwepo kwa makundi mengine, na hata kusahau ndani yao kuna madhehebu mengine tena yanayotofautiana.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Pamoja na kuwepo kwa makabila yanayozidi 100, bado ukabila umeshindwa kujipenyeza kwa nguvu zaidi, na hata kutia chuki dhidi ya kabila jingine, japo ukabila nao hauwezi kuachwa nje kama mdudu nyemelezi kwenye taifa changa. Leo nitaongela udini sababu ndo umepanda chart hadi leo kuwa gumzo, na kuleta matukio tofauti ndani ya nchi ambayo wengine waliamini ni kiswa cha amani.

  [/FONT]

  [FONT=&quot]Udini umetoka wapi?[/FONT]

  [FONT=&quot]Kabla ya miaka ya 80, hapakuwepo na udini, ila tulipo anza kusonga mbele tunaona udini unapata kazi, miaka ya tisini, ulianza, pale tuliposema watu waende shule na mavazi tofauti (tukizingatia dini zao) ingawa hilo wengine waliona halina tabu, ila liliwatofatisha wanafunzi na kuwafanya wawe na makundi tofauti, pengine sababu ya mavazi yao. [/FONT]
  [FONT=&quot]
  Pili, idadi ya watu imeongezeka , na fursa kutokuongezeka kuendana na ongezeko la idadi ya watu. Hii imesababisha watu kutafuta upendeleo kwa njia mbadala, na moja ni dini kutimika, na ukabila japo bado upo chini ya dini.[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Tatu, uchumi wan chi haukui na kutoa fursa sawa kwa wote, kwa mfano shule nzuri zimekuwa za gharama sana, kuhitimu chuo kikuu haisaidii au haihakikishi upatikanaji wa kazi, na maisha bora, ajira mpya ni chache, hivyo kuwa nakundi la watu wanelimu ya nchini na kati bila shughuli maalum za kufanya. Hili kundi ni rahisi kulishawishi kwa lugha yoyte ile lugha yoyote kwa gharama nafuu.[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Nne, idadi ya watu kuingia kwenye dini na kuitumia kama ngazi, kufadhili, kudhulumu, etc na kujipatia umaarufu kumbe nia yao ni kwenda kwenye madaraka na kushika dola, kundi hili ni baya sana, kwani hupandikiza chuki dhidi ya kundi la dini nyingine.[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Tano, wanasiasa kujipambanunua kwa kulinda na kutetea kundi flani la dini flani, wakati mwingine kupeleka malalamiko yao na maonyo yao ya kisiasa kwenye majukwaa ya dini.[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Sita, viongosi wa dini kuingilia na kusemea serikali katika kujitanabaisha kuwa iko (haiko) upande wake bila kujadili na kundi jingine la dini/dhebu[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Saba, serikali kushindwa kutoa nafasi kwa viongozi wa dini na madhehebu kukutana kwa pamamoja, ( na kama inafanya hivyo viongozi hawaleti taarifa sahihi kwa waumini wao) Viongozi wa dini wanapaswa kutoa mawazo yao kwa serikali kwa niaba ya waumini wao kwenye vikao maalum, ikiwa ni kukutana na serikali kwa muda mwafaka, na kufanya makubaliano ya pamoja. [/FONT]

  [FONT=&quot]
  Nane, serikali kushindwa kutoa sera na mwongozo kwa makundi madogo (unadvantaged group) haya ni yale ya wasio waislam wala wakristo, ni wapagani, dini za asili na hata wasio abudu. Kundi hili kubwa lenye watu wengi limeachwa nje na hata halina mwakilishi na wala halipewi fursa ya kuwepo, tunaomba litambuliwe, maana mm hujiuliza kama, kiongosi wetu hatokani na uislam na ukristo ataapa kwa kushika nini?, ( mfumo useme na siyo katiba maana hiyo ya wote wenye na wasiyo na dini)[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Tisa, migogoro isiyo isha ndani ya dini hizi. Dini hizi kubwa zenye wafuasi wengi zina migogoro kila siku. Vikundi vya uasi ndani ya dini hizi, vikundi vya wpigania haki ndani ya dini, vikundi vya wana mageuzi huleta migogolo kila kukicha. Migogoro hii isipopata ufumbuzi ndani basi hutoka nje na kuwa kero kwa waumini wenyewe na kwa waumini wa dini zingine. Vikundi hivi, vya wanamaombi, siasa kali, imani kali etc huanza kuongelea siasa kugawa watu na hata kuunganisha mapinduzi ndani na nje ya nyumba za ibada. [/FONT]

  [FONT=&quot]
  Kumi, kuwepo kwa kundi kubwa ambalo linapenda dini, lakini halijapta muda wa kuisoma na kuilewa dini, hili kundi limekuwa ni kama bendera kufuata upepo, kiongozi akisema haliwezi kupambanua hata kidogo. Waumini wengi wamekuwa si wasomi wazuri wa vitabu vya dini bali wasikilizaji, na hivyo kupokea upotoshaji kirahisi zaidi.[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Kumi na moja, baadhi ya viongozi wa dini hawana wito, wanamapinduzi, wamechoshwa na mfumo wa sisa, uchumi, na maendeleo ya nchi. Hili kundi halina mbadala ila kutumia nyumba ya ibada, kutaka kuleta mapinduzi hadi ya kisias, kiuchumi, kisheria n.k wao Rais, IGP, Sheikh, Askofu, Waziri etc siyo muhimu, maneno yao chuki tu, wakichanganya na mahubiri wanapotosha waumini wao, maana wao wamejaa visasi na uhasi.[/FONT]

  [FONT=&quot]
  Hitimisho!! [/FONT]

  [FONT=&quot]Kuwepo na mjadala mkubwa watu wajifunze siyo tu dini bali hata vyanzo vya dini hizi, hivi mkwawa, mirambo, etc walikuwa dini gani? Kabla ya warabu na wazungu, wazee waliomba mvua wapi? Je hizi dini zina husiana na tamani za wketu au wageni waliozileta? Hivi ukiua watu wote wasio dini yako utahubiri nani? Hivi ni bora kuingiza watu kundi mwako au kuwa ua[/FONT]
  [FONT=&quot]Nitakuja na suluhisho la udini kwenye Taifa maskini. Ingawa umaskini ni chanzo kikubwa cha udini, ukabila na machafuko mbalimbali.[/FONT]
   
 2. Z

  Zuwely salufu Senior Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Umegonga sehemu nye-nyeti
   
 3. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,634
  Likes Received: 2,445
  Trophy Points: 280
  Watu weusi wa jabau sana,

  Wanauana kwa ajili ya Mungu Allah na Mungu Jehovah!
   
 4. l

  long'oi Senior Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nchi yetu imekuwa na kipindi kirefu cha kufukuta kupotea kwa Amani ya nchi kwa misingi ya nchi. Wote tutakubaliana hali hii imekuwa zaidi katika kipindi cha awamu ya 4 ya uongozi wa Rais JKikwete.

  Watu wamekuwa wakisema Chadema wamnatishia/ kuvunja Amani na wamekuwa wakishughulikiwa ipasavyo kwa kigezo cha kulinda umoja na mshikamano wa nchi. Sawa. Tujiulizi ni kipi kinahatarisha amani ya nchi kati ya siasa na udini?

  Rais anashindwa kukemea kwa sababu yeye ndio mwasisi wake. ameingia madarakani kwa misingi ya dini, uteuzi wake wa viongozi umekuwa ukiegemea kuwapa nafasi watu wa dini flani hata kamma hawana uwezo klwa kisingizio 'kukuza na kueneza dini kwenye taasisi na vyombo vya umma). Jambo hili linafanyika wazi sana, kma hamuamini kuna mkakati wa kukifanya UDOM kuwa cha misingi ya dini anayolazimishwa kuieneza. Hawezi kemea machafuko haya yanayotokea sasa.

  Majibu ya Rais kwenye swala hili yamekuwa mepesi mno, ni katika kipindi hiki ile mihadhara aliyopambana nayo mzee Ruksa ya kukashfu watu na dini zao inakuwa kwa kasi, na usambazwaji wa CD zake unafanyika peupeeee. Ilianza kidogokidogo tukasema potezea, sijue ieendelee kupotezewa?
   
 5. E

  Earthmover JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 13,531
  Likes Received: 3,723
  Trophy Points: 280
  Tukemee kwa nguvu zote bila kujali Dini zetu ,makabila yetu ,uwezo wetu kiamaisha na hata upagani wetu, swala hili la UDINI!!!

  Nalaani vikali WAPANDAJI WA MBEGU HII YA UDINI wasiojua misingi mikuu ya UTAWALA BORA UTU NA HAKI YA MTANZANIA!! Mmetumia nguvu nyingi kuizuia HAKI YA MYONGE MLIYO IPORA na haya ndiyo matunda ya sumu mliyo pandikiza kwa jamii.
  HAKI inapigania HAKI!! haki ya myonge iliyopotea…. wanainchi wameelewa vizuri HAKI YAO , nyinyi mkaja na hii mbegu ya udini kuwapandikiza hawa wanainchi masikini ili muendeleee kuwanyonya zaidi…nasema mlaaniwe nyinyi pamoja na vizazi vyenu!!!

  Hitimisho: watanzania wote tunawajibu Mmoja tu kwa sasa kuhakikisha haki na utu wetu vinarudishwa mikononi mwetu,Kulinda Amani yetu na KAMWE SI MBEGU HII CHAFU YA UDINI!!!

  Mlipora HAKI NA UTU WETU na kamwe si UDINI …TURUDISHIENI HAKI NA UTU WETU!!

  WATANZANIA TUKIKUBALI KUGAWANYWA KATIKA SAFARI HII YA KUDAI TULICHO PORWA TUMEKWISHA!!  TANZANIA BILA UDINI ILIWEZEKANA INAWEZEKANA NA ITAWEZEKANA!!!

  MUNGU IBARIKI TANZANIA

   
 6. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Watanzania tuna tofauti nyingi sana achana na hii ya dini, lakini licha ya tofauti zote hizi tunaunganishwa na Utanzania. Tofauti hizi zimejigawa katika nyanja mbalimbali ambazo zikitumiwa vibaya zinaweza kuleta machafuko na amani kutoweka.

  KISIASA, hapa watanzania tumejigawa katika vyama mbalimbali vya siasa, kila chama kikiwa na malengo ya kushika dola. katika siasa kuna watawala na wasiowatawala.

  KIJAMII na KIJIOGRAFIA, hapa watanzania tumejigawa katika makabila, na kanda tofauti vilevile dini kama Waislamu, wakristo, wahindu, wabudha, na wasio na dini.

  KIUCHUMI, Hapa watanzania tumejigawa katika matabaka walionacho na wasio nacho, wakulima, wafugaji, wachimba madini n.k

  KIUTAMADUNI, hapa tumejigawa kulingana na upendeleo wetu katika michezo mabali mathalani katika soka wengine ni Simba na Wengine ni Yanga, tukumbuke kuwa hata ushabiki wa soka kule Misri ulifanya watu wafe.

  MAONI YANGU. kuwa watanzania tonatofauti nyingi sana, na kwa tofauti hizi zinaweza kutumika kutugawa kwa maslahi ya wachache wanaotaka kutumia hiyo kama daraja kufikia maslahi yao, kwa namna yeyote.Udini ukishamiri wakristo na waislamu ndani ya dini hizo kuna makundi hasimu, vile ndani ya dini hizo kuna makundi mbalimbali ya watu kutokana na SIASA, UTAMADUNI.KANDA na UCHUMI, hivyo kimoja kinchotakiwa kutuunganisha ni Utanzania.
   
 7. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hayo mengine hayana tabu sana kama la kiuchumi, ili bwana siku likianza kututafuna hatutapata sehemu ya kukimbilia.
   
 8. i

  ibrahim kisili Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashangaa sana tunaposhabikia swala hili humu ndani kwa kuwa naimani watu waliomo humu tunaouwezo wa kujadili maswala mazito, familia zetu leo hii nyingi zimeoleana waislamu na wakristo, sie tumekua hatuoni tofauti kati ya ukristo na uislamu ila watoto wetu wa sasa haya wanayoyaona naimani wanajifunza kitu kibaya kuwahi kutokea hapa tanzania....jamani matusi kwa dini zetu humu ndani hazitasaidia kitu tujadili na tuone tunachangia vipi kulimaliza swala hili.NASHANGAZWA SANA NA KASHFA KUBWA SANA ZINAZOTOLEWA HUMU KWA DINI HIZI MBILI.
   
 9. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Huu ni Udhaifu,
  Vikundi hivi vinavyoleta chokochoko juu ya imani wakati wenywe ni watenda dhambi wakuu sasa vimefikia pabaya kwa kuwa wameona hamna serikali kwani wanaahidi kufanya vurugu na wanazitekeleza bila kizuizi chochote
  Hivi ni kweli idara ya Usalama wa taifa na jeshi la polisi hawakuwa na taarifa na mipango hii? Na hakuna mbinu zozote za kuyadhibiti kabla?

  Viongozi wa misikiti nao katika mawaidha yao ya sala hawakemei hii tabia? Ama nao pia wanahamasisha yatokee?
  Hakika tumefika pabaya iwapo serikali inakaa kusubiri yatokee ndio wakapige mabomu bila ya kujali nani ataathirika na kupata madhra ya kuumia yakiwamo na ya watu kuibiwa na wimbi la vibaka wanaojitokeza nyakati za matukio kama haya(ikumbukwe kariakoo ni business centre)

  hatuwezi kuwa wote waislamu wala wakristu,la msingi ni kujikita katika imani zetu kwa misingi ya kuheshimiana kiimani na yakitokea yanayoamsha hasira yashughulikiwe kibusara

  ikumbukwe tukio la mbagala limefanywa na watoto ambao umri wao unaweza kuwafanya wasijue watendalo na pia labda kutokana na malezi ya familia zao..hili lipo wazi hata kisheria hukumu za watoto zinazingatia hilo
  Tujiulize vurugu hizi zinafanywa na watoto? Kwani wale watoto walitumwa na wazazi wao kuwa wewe kaseme hivi na yule mwingine kutumwa kufanya vile?

  ni sisi watu wazima tusioliona hilo ndio wapumbavu.kama mimi nakiheshimu kitabu kitakatifu siwezi kukupa ukinajisi kwani nitakuwa nimekosea,ila wewe ukikinajisi wakati hukiabudu kwako si kosa ila kwangu ndio nitabidi nijitafakari
  kuna matukio kama ya yule binti aliyekuwa mtoto wa imamu bagamoyo akaingia ukristo,wakamchokonoa na kumpa quran ainajisi naye akainajisi.(nasikia alishtakiwa na kufungwa-Ingawa mimi nalipinga hilo)
  kwa hoja kuwa aliyeona ni kosa hakuangalia upande wa aliyetoa quran inajisiwe naye angelistahili adhabu!Rejea miaka michache iliyopita kuna muumini wa kiislamu aliyefahamika kama Dibagula alihukumiwa huko morogoro kwenda jela kwa kauli yake ya kusema yesu sio Mungu..kwa haraka alionekana kakosa na kufungwa lakini aliachiwa baada ya kuitafakri hukumu kuwa alifungwa kimakosa kwani kwa imani yake hakuwa na kosa ila kinafsi yake inaweza kufeel guiltness ya kuwachefua wakristo na pia nafsi za wakristo kuumizwa na hilo

  ipo mifano mingi lakini hapa hoja ya msingi ni why this things are happening like there is no ruling govt? Huu ni udhaifu,hata wakristu wakipata mawazo kuwa this is happening coz the head of state is muslim mtawazuia?

  hivi majuzi watu walisema watagoma kuhesabiwa,likatolewa tamko kuwa atakayegoma atachukuliwa hatua..kweli wakagoma,wakakamatwa na baadaye kuachwa huru bila adhabu yoyote,watu wale wale kwa kuona hali hiyo si watafanya kingine kwa kuwa wanajia hawafanywi kitu!
  wamechoma biblia
  wamechoma makanisa
  Je hiyo sioyo najisi kwa wakristo? Tena ikifanywa na 18+++??????
  na hao ni watu wazima...baadaye kutafuata nini? Rejea msemo wa kiislam usemao ukimuachia mbwa atakufuata mpaka msikitini
   
 10. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  JK ndiye aliwatuma hawa,ndo maana amekuwa akiwafumbia macho na masikio angalia pia matangazo yanayorushwa na radio imani utaamini wanalelewa kwa lengo best known to himself mwenyekiti wa ccm
   
 11. enhe

  enhe JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 80
  "The cure is to hit them(muslims) hard"-Ariel Sharon
   
 12. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  police waache udhalilishaji juu ya viongozi wa dini ya kiislam huwezi kumkamata kiongozi halafu, vinginevyo fujo hazitaisha
   
 13. a

  afwe JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
   
 14. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  Hebu waislamu watafakari upya...haiingii akilini tendo la watoto wadogo kuwafanya wafanye fujo kama wafanyavyo sasa...there must be something wrong!
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  mkuu tatizo ni ukosefu wa ajira kwa watanzania,hapo hakuna suala la dini!lowasa alishasema hili ni bomu linalolipuka
   
 16. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,323
  Likes Received: 3,117
  Trophy Points: 280
  Usiwalaumu sana waliotenda haya, namna yao ya kufikiri na wale watoto walioanzisha hili ni sawa kabisa; ni sawa na walevi wawili wanaopigana na mlevi kutumwa kutatua tatizo, katika nchi inayoongozwa na mlevi mwingine.
   
 17. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  nchi ambazo zimeleta dini asa uislam wako wanafikiria mambo ya kiuchum zaidi na namna ya kuboresha maisha ya wananchi wake,ikiwemo miundo mbinu,nchi za kiarabu kama united arab emirates zimepiga hatua kubwa kimaendeleo kwa sababu ya kutoleta udini,lakin sisi ambao dini tumeletewa kwa meli tunajifanya kujua zaidi ata kuchoma nyumba za ibada za dini nyingine mambo ambayo hayakuwepo kipindi cha nyumba.
  huu wakati nchi zote dunian ziko katika malengo ya kukuza uchumi na maendeleo na siyo kwenye vurugu ambazo hazina kichwa wala miguu,
  watu wote bila kubagua dini lazima wafate sheria za nchi na wote wakikosea na kuleta uchochezi lazima wapelekwe mahakaman bila kujali dini aliyopo
   
 18. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mkuu...kisu kimegusa mfupa..punguza makali
   
 19. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  HICHI NDICHO KILICHO WAWEKA WAISLAMU LEO BARABARANI(MAANDAMANO)
  Sababu ni Kama Ifuatavyo:

  1. Quran Kukojolewa
  2. Shekhe Ponda Kukamatwa.
  3. Shekhe Faridi ajulikani alipo huko Zanzibar.
  4. Waislam Kuonewa na Kuteswa kwa sababu ya Mbagala
  5. Akina mama Wa Kiislam Kudhalilishwa wakati wa Kichapo Mbagala.
  6. Msikiti Umepigwa Bomu la Machozi mbagala.
  7. Askari wameingia na Viatu Msikitini.
  8. Rais amewapa pole Wakristo.
  9. Maaskofu kuwapongeza Polisi Kuwakamata Waislam na kuwaweka ndani.

  Kumbe Safari ilikuwa ni kwenda Ikulu
   
 20. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Hizi extension za Al qaeda,Janjaweed,Boko Haram na Alshabaab,wameminywa huko sasa wanakuja kwenye nyumba loose..baba mwenye nyumba mtoto anatiwa mimba hadi karibu anajifungua lakini baba hamjui hata mkwewe!
  uzuri wake Raisi,makamu,judge mkuu,uwt,igp mpaka kamanda wa kanda wanaswali nao
   
Loading...