Udini sio mpya tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udini sio mpya tz

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chayowa1981, Oct 20, 2012.

 1. c

  chayowa1981 JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 218
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Moderator Naomba usiiondoe hii post
  Ama kweli watanzania tu wepesi wa kusahau, vurugu hizi zinazotokea leo ndo twasema kuwa ndo udini unatunymele?
  Tujikumbushe kidogo, Mwaka 1993, Vurugu zilitokea dar hadi kuvunjwa kwa mabanda ya nguruwe
  Kati ya Mwaka 1995 - 2000, vurugu nyingi sana za kidini zilijitokeza ikiwemo, maandamano yaliyopelekea kuuawa kwa mtu au watu Mwembechai.

  Mi nadhani kubwa linalowafanya watu kudhani kuwa udini unanyemelea TZ ni kutokana kuwa 2005 Watu wengi bila kuzingatia Dini, Kabila, kanda, rangi n.k walimuunga mkono J.K na hivyo kupelekea kuondoa kutokuaminia kati ya makundi hayo.

  Mwaka 2010 Viongozi wa kanisa katoliki walitoa Ilani na waraka wa kichungaji, ambao pamoja na kuwa maudhui yake yalikuwa mema ila ilionekana waziwazi kuwa utekelzaji wake ungegubikwa na udini, kwa mfano katika waraka sehemu mojawapo ilitoa mwongozo kuwa waamini wake wafikishiwe ujumbe kupitia jumuiya ya kikatoliki, KUMBUKA kuwa katika jumuiya hizo hakuna mtu mwingine ispokuwa wakatoliki ambao huwa huhudhuria. Kwa bahati mbaya sana ni watu wachache mno walionya kuhusu hilo akiwemo mzee Kingunge ambaye aliitwa kwa kila aina ya majina ya kifisadi (si nia yangu kukanusha kama yeye si fisadi, bali alichokuwa amekitahadharisha kilikuwa na mantiki). Mambo yalianza kuwaka moto pale baadhi ya waislamu walipoamua kutoa nao waraka na ilani yao ambayo ilionekana ni kujibu mapigo ya ule wa wakatoliki. (Tayari joto la udini likaanza)
  Kama ilivyokuwa imetabiriwa na wengi akatokea mgombea wa Chama Cha Upinzani (CHADEMA) akiwa anajinasibihisha na maneno yaliyoandikwa kwenye waraka ule, hivyo chama hicho kuonekana kina udini. Katika mitandao mbalimbali ambayo watu walikuwa wakijadiliana ilionekana wazi kuwa waislamu walikuwa wakiunga mkono CCM, na wakristu wakiunga mkono CHADEMA. Baada ya uchaguzi tu hivi, Kikwete alitahadharisha, kuhusu udini uliojitokeza, matokeo yake akashutmiwa kuwa anaongea kitu ambacho hakipo. Kwahiyo mambo yameenda hivyo hadi hapa tulipofikishwa.

  Nigusie Kidogo jambo lingine, Waislamu wamekuwa wakimshutumu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere kuwa hakuwatendea haki. Wakati huo huo Kanisa katoliki wakawa wameamua kutumia haki yao ya kiimani kulingana na mafudisho na Kanuni za Kanisa hilo kuanzisha mchakato wa kumfanya kuwa Mtakatifu. Kwa wale wasiofahamu kuhusu kuwapa utakatifu walei wanaona kuwa Mwalimu Nyerere ameanza Hekaheka za kisiasa akiwa na miaka takribani 30, na kuwa waziri mkuu akiwa na miaka 39, na raisi akiwa na miaka 40, sasa ni lini alipata nafasi ya kulitumikia kanisa?
  Conclusion yao inakuwa moja Alikuwa MDINI.

  Kwa leo naomba niishie hapo natumai tutakuwa na Mjadala mzuri wa kujenga.
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hivi, mbona mara nyingi mnapoongelea ukristo mnaongelea wakatoliki? hivi warumi waliwafanya nini ninyi watu wakati wa vita vya crusades huko mashariki ya kati, mnajua kuwa wakatoliki sasaivi ni wakristo wachache kuliko waprotestant? waprotestant mnawaweka kwenye eneo gani sasa manake tafsiri ya waislam kuhusu ukristo ni ukatoliki. kilaini au pengo akiongea wanasema wameongea wakristo wote, yaani misikiti hii inafundisha mambo ya ajabu sana, manake watu wake naona hawaeleweki.
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mdini ni JK aliyeweka mahakama ya kadhi na OIC kwenye ilani ya CCM 2005. Pia aliwaahidi Waislam upendeleo maalum kwenye ajira na elimu. Kwa kifupi, udini wa leo ni matunda ya JK.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Sasa UNAJUA kuna DINI nyingine zaidi ya U-Catholic Tanzania? Sasa Hizo DINI ZINGINE za KIKRISTO ziliachwa NJE kama Waislamu wote si SAWA???

  Sasa ni Sasasawa na Waislamu wa DINI ya SUNNI ambao ndio wengi Tanzania kwenda MSIKITINI IJUMAA na kuashiriana KUANDAMANA baada ya SWALA ya IJUMAA...

  Sasa DINI Nyingine za KIISLAMU Tanganyika kama VILE SHIITE; WAHABIS;KHARIJITES; SUFIS; GULATS na ZAIDI? Wao Wanapata wapi hayo Mahubiri???

  KUWENI Wajuaji na Mnavyovisema ROHO zenu zitakuwa safi na UPENDO wa Kila MWANADAMU hapa Tanganyika
   
 5. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,803
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  wakatoliki Ndio lenye kubeba waumini wengi wa kikiristo na silo wengine..
   
 6. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Hakuna jipya zaidi ya kujaza server tu. Tatizo la uislamu ni kuwa mafundisho yake yanakinai, hivyo ili yanoge ni lazima kuhubiri kwa kutunia biblia. Ndio maana biblia inashikilia rekodi ya kuwa kitabu kinachosomwa zaidi kwenye mihadhara ya kiislamu. Waislamu wengi wanaelewa aya lukuki za biblia lakini wakristu hata muda hawana wa kusoma kurani. Why? Kwa sababu huwezi kuvuna machungwa kwenye miiba!
   
 7. mnyanyaswaji

  mnyanyaswaji JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 469
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unalosema ni kweli kabisa waislamu wanaijua vizuri Biblia kuliko hata wakristo wanaoibeba kwenda nayo kanisani kuuzia sura lakin kwa siku hata page 3 hawezi kusoma akiwa nyumbani+kanisani pia. Nasikitika wewe hujui dini hata kidogo na kwa taarifa yako hakuna Muislamu atakayeitwa Muislamu bila ya kuvikubali vitabu vifuatavyo:-
  1.ZABURI(ya Daudi)
  2.TAURATI(Mussa)
  3.INJILI(Yesu)
  4.Qur an(Muhammad S.A.W)
  Hivyo vitabu juu vilikuja wakati wa Mitume waliokuwa mentioned kny mabano.
  Sasa kosa lilopo hizi Biblia zenu za sasa mnaZoEdit Dodoma kila baada ya muda nani atazielewa? Eti agano jipya sijui kaja nayo nani? Hapo ndo mnapochemka. Mkibadili maneno yale ya zaman yawekeni kny mabano watu waone origin yake. So kwa hoja yako ni kweli tunasoma Biblia sna kuliko nyie kwasababu pia tumeambiwa kuiamini ila tu sio Biblia inayochakachuliwa kila mwaka kama zenu.
   
 8. k

  kisilo Senior Member

  #8
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakuungamkono maana jk ndiye katufikisha hapatulipo.
  na misafara yake ya ng'ambo isiyoisha anatafuta pakukihifadhi.
   
 9. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hapaa mkuu, kwa sasa, wakatoliki na waprotestant wanaweza kuwa sawa kwa sawa. inakadiriwa kuwa wakatoliki tz wanafikia milioni kumi tu, ile milioni 35 inayobaki ni madhehebu na dini zingine ikiwepo na upagani huko umasaini na usukumani. pia wakatoliki wengi sana wanaacha siku izi kujiunga na makanisa haya ya kisasa, amini usiamini, wanapungua kila wakati. labda ungesema tu kuwa, waislam wana bifu na wakatoliki tangia enzi za crusaders huko middle east walipokuwa wanagombania jerusalem, bifu hilo ni sawa na bifu walilonalo na wayahudu, ukatoliki na uyahudi ni adui yao mkubwa hapa duniani.....nenda kwenye mihadhara yao utaona wanavyoweka mikanda ya dola ya kirumi na kutia chuki kwa warumi/waroma.
   
 10. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hivi tusipowazungumzia Wakatoliki unafikiri tutazungumzia walutheri au Anglican ambao wananjaa kali halafu hawajajipanga ni sawa kudiscuss majimaji wakati yenye Nguvu ni simba au yanga
   
Loading...