Udini sasa umewatawala wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udini sasa umewatawala wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kipuyo, Jul 17, 2011.

 1. k

  kipuyo JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 1,143
  Likes Received: 511
  Trophy Points: 280
  MAKALA yenye kichwa cha habari “Kikwete sasa awa mzigo kwa CCM” iliyochapishwa katika gazeti hili wiki mbili zilizopita, imeibua mengi ikiwamo maudhi na furaha. Maudhi na furaha nilizozipata zilitokana na mrejesho nilioupata kutoka kwa wasomaji wangu.
  Kitu kimoja nilichojifunza ni kwamba wananchi wengi wanatawaliwa na fikra za kidini katika kujadili mustakabali wa taifa. Kwamba wanasikiliza habari kidini, wanaangalia runinga kidini na hata magazeti wanasoma kidini; kila kinachoonekana, kusomwa na kusikilizwa, hutafsiriwa kwa misingi ya kidini.
  Wengi wao wanajiuliza wakati wa kusikiliza, kusoma na kutazama taarifa za habari, je habari hii imelenga dini gani? Inanufaisha dini ipi na imekula njama kuhakikisha yaliyosomwa, yaliyotangazwa na yanayoonekana kwenye taarifa yanatokea na je serikali iko upande gani katika taarifa hii?
  Utashangaa baadhi ya wananchi wanatumia saa zaidi ya mbili au tatu kusoma matangazo ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga chuo kikuu fulani. Ukichunguza utagundua wanachofanya ni kusoma jina moja baada ya jingine ili kujua majina ya akina Shaaban, Ramadhani na Musa ni mangapi na yale ya akina John, George na Peter nayo ni mangapi!
  Kuthibitisha udini umetawala angalia msimamo wa baadhi ya wasomaji. Wengi wamegawanyika kidini katika habari ile ya “Kikwete kuwa mzigo kwa CCM.”
  Wapo walionipongeza wengi wao wakiwa Wakristu nadhani kwa sababu nimemsema kiongozi mwislamu wanayemwona kuwa anawachukia. Wengine walinibeza na kunitukana wengi wao walionesha dhahiri kutokana na lugha iliyotumika kuwa ni waislamu.
  Hakuna hata mmoja aliyehoji mie ni dini gani ila karibu kila Mkiristu alidhani mie ni Mkristu niliyemsema mbaya wao Wakiristu na karibu kila Mwislamu alidhani mie ni Mkiristu niliyetumwa na Wagalatia wa Kanisa kumsema Mwislamu mwenzao.
  Miongoni mwa walionitumia ujumbe, ni kutoka Na. 0713848489. Ulisema, “Kicheere, nimeipenda makala yako. Lakini unadhani JK (Jakaya Kikwete) mwenyewe anajijua kama ameshakuwa mzigo?
  Mwingine ambaye ujumbe wake wa simu ulitumwa kutoka Na. 0656793898 ameeleza, “Umejieleza vizuri. Ni kweli kwamba rais wetu amewavunjia heshima maaskofu. Pia mimi binafsi ameniudhi sana, lakini kaka hawa maaskofu wetu wamezidi, wanaona fahari kumwalika mtu asiyemwamini Yesu katika mambo yamhusuyo Yesu. Sasa wajifunze.”
  Naye mwenye simu Na. 0769051184 alisema, “…Kwani Kikwete tu? Mbona hata Mkapa (rais mstaafu Benjamin) aliwakosea waislamu kwa kuwaua pale Mwembechai, lakini wandishi mlikaa kimya?”
  Mwingine kutoka Na. 078728238 Ni kweli Kikwete ana makosa yake, lakini ninyi hamumkosoi kwa sababu ya kuipenda nchi bali udini ndio unaowasumbua.”
  Huyu kutoka Na. 0784778612 alinieleza, “…Kama ungekuwa rais hungetawala hata saa moja. Mambo unayotarajia ya kufikirika hayatakufikisha popote. Nimekuwa nikikufuatilia makala zako, ni paparazzi unayependa kulaumu hata kile kizuri kinachofanywa na serikali.
  “Inaelekea pia wewe ni mnafiki, mchochezi na mbinafsi. Hujui unatamba kwa kuwa Kikwete kakupa uhuru wa habari mpaka mnatukana demokrasia eti yeye si ndiye choko mchokoe pweza binadamu humwezi. Haya, ruhusa endelea na utetezi kwa Mapadri usije kukosa sakramenti.”
  Mwenye simu Na. 0713065382 alisema ukweli utabaki palepale. Viongozi wetu wa dini si wasafi, nawe unafahamu hivyo. (Maaskofu) wanautumia udhaifu wa rais wetu kujitakasa na wandishi wetu kutetea. Lakini yupo mwanafalsafa aliyesema “ukisema kwenye shaka na ukawekewa mashaka usilalamike.”
  Mwingine mwenye simu Na. 0777475191 aliandika, kauli ya rais dhidi ya viongozi wa dini juu ya dawa za kulevya ni sahihi. Kumbe awaeleze wapi? Mbona wanapoikosoa serikali hadharani nnakaa kimya! Usiandike makala kwa kusoma vichwa vya habari za magazeti.
  0655120920 Pesa za wala rushwa mafisadi na wazungu wa unga ndizo zimetumika kwenye uchaguzi 2005. Akiwakurupusha Lowassa, Rostam, au Mzee wa Vijisenti ataadhirika. Kama kweli anajua mtu anauza unga hicho kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya kipo kwa manufaa ya nani?
  Huyu mwenye Na. 0715472751 alisema waraka wako nimeupenda sana. Vilevile nimefurahia Kikwete kuwatusi maaskofu wetu kwa sababu kila wanapotaka kusimikana wanamwita mgeni – hata kwenye matamasha makubwa kama vile ni mtakatifu – wakati kuna watu kibao wenye hekima zao, wanabaki kujipendekeza tu. Waache wakome.
  0718321242 Viongozi wa kikristu nao wamezidi kujipendekeza kwa wanasiasa hasa walewanaoshika dola wanawahofu na kuwanyenyekea sana hata kusahau wito wao. Yaujazayo moyo ndiyo yautokayo, sasa siasa na kanisa wapi na wapi kwa hiyo kikwete hana kosa, tangu lini Kanisa likawa ukumbi wa siasa maaskofu ndio wa kulaumiwa.
  0718760663 Yesu aliwapenda watu wote hasa waliojitambua kuwa ni wakosefu na kutubu mbele yake. Maaskofu wamevutiwa nini na Kikwete? Chuki mbaya aliyoipandikiza wakati wa kampeni au nini? Kama si hekima ya Watanzania tungekuwa wapi? Au ameshaomba radhi kwa Wakristu hasa sisi RC?
  Majibu wanayo wao wenyewe. Kikwete katoa hisia zake mwenyewe kwamba hawapendi maaksofu hasa wa Kanisa Katoliki wawe wanauza hayo madawa au hawauzi watajijua wenyewe kwani wameshakipata walichokuwa wanakitaka.
  Alisema viongozi wa dini hawapaswi kuwa wanafiki; ukichukua pesa ya mwizi na unajua ni mwizi nawe ni mwizi. Ubarikiwe kwa waraka mzuri.
  Mwenye simu Na. 0713190195 aliandika, waraka wako umelenga kupotosha. Nani amekwambia 2005 Kikwete alipata asilimia 90? Kwa maaskofu ni mkuki kwa nguruwe. Wao wamekuwa wakimshushua hadharani kama alivyowafanyia.
  Sasa hapo ndipo tulipofika Watanzania, kwamba kiongozi anapokosea asisemwe, na akisemwa yule anayemsema anachukuliwa kuwa anafanya hivyo kwa sababu kiongozi huyo ni muumini wa dini fulani. Yaani watendaji serikalini waibe mali ya umma na wasisemwe kwa sababu ni Wakatoliki, Waislamu, Waanglikana au Walutheri!
  Haya yaliwahi kumtokea Reginald Mengi pale alipolalamikia mfanyabiashara Yusufu Manji kwa kununua majengo kutoka mashirika ya hifadhi ya jamii kwa bei sawa na bure na baadaye kuyauzia mahirika hayo majengo yale yale kwa mabilioni.
  Mengi aliambiwa ni mdini anayeuchukia Uislamu kwa sababu tu Yusufu Manji ni Mwislamu, mashirika yale ya hifadhi ya jamii yanaongozwa na Mwislamu na serikali iliyo madarakani inaongozwa na Mwislamu! Watu waibe tu kwa sababu ni Waislamu na kuwakemea ni kuuchukia Uislamu! Haya hayaingii akilini.
  Kikwete hawakamati wala kuwashitaki watuhumiwa wa wizi katika akaunti ya madeni ya nje ya benki Kuu (EPA) na Watanzania wasiseme kwa sababu kumsema Kikwete kwa kutotekeleza wajibu wake ni kuuchukia Uislamu au eti unamsema tu kwa sababu ni Rais Mwislamu! Huu ni upuuzi mtupu.
  Leo hii kila anayemsema au kumwandika Lowassa anaambiwa ametumwa na Kanisa Katoliki kuhakikisha mtu mwingine asiyekuwa Mkatoliki hakaribii urais bali urais uende kwa Mkatoliki Wilbroad Slaa.
  Aliyoyafanya Lowassa wote tunayafahamu, lakini tunaambiwa tunayemsema tumetumwa au tumelipwa na Kanisa Katoliki kuhakikisha Mlutheri Kikwete hapati urais!
  Wananchi hatuwezi kuacha kuwakemea wakosefu kwa sababu ya dini zao au dini za hao wanaowatetea. Kwa hili Watanzania wengi wana hatia, wasafi ni wapagani tu ambao hawahoji dini ya mtu wala kulalamikia mtu kwa sababu ya dini yake.
  My intake:Watanganyika tunaelekea pabaya.Udini ni bomu linaloweza kulipuka na kutuathiri kuvuruga kabisa vision ya nchi yetu 2025.
   
 2. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Watanzania tulio wengi sana tunazania Raisi mzuri ni yule:anayeimbiwa kwaya nyingi sanaanaye watukana marekani na Uingereza na kuchukia matajirimwenye kupenda kuvunja uhusiano wa kibarozi na nchi inayotuletea pesa ktk utalii na foreign trademwenye maneno mengi sana katika mikutano ya Non alignment na OAUmwenye kupenda kuangalia matatizo ya watu wengine kama vile wapigania uhuru ila wanachi wake hawajaliAisyeenda mpirani na kufurahia soka na wananchi wakeMwenye kutoa hati miliki kwa wanamuziki na kufukuza makocha wa nje ili kila mcheza mpira asiwe profesional wanamuziki wasitajilike na vipaji vyao vya muziki bali kuishia kufa masikini tuu. Ona marijani na ahmad kipande!nchi kutokuwa na heshima yeyote ya sanaa duniani!Vijana kucheza Gwaride na kuimba kwaya masaa 24!wakati wenzao wa Nigeria, zambia na ghana wanacheza pro ulaya! wakuu wa wilaya wote wawe darasa la saba! Marufuku kuwa na chama huru cha wafanyakazi!Sasa sifa hizo Raisi Kikwete kazikataa kabisaa na kila kukicha anawafanyia kazi wananchi. Kuhusu swala la umeme sio lawama kwa kikwete wala serikali yake tuu bali pia hata Hao maraisi waliopita walikuwa wapi kusaka vyanzo vingine vya Umeme? Pesa za kujengea mabwawa makubwa na kutafuta vyanzo vingine ziliishia ktk kuimalisha chama wakati wa enzi za Chama chashika hatamu. Sasa mbona lawama msimbambikizie raisi wa wawakati huo leo hii kila mzigo wa makosa ya nyuma anabambikiziwa Kikwete, kulikoni mwejamen?Ghalama za mkutano wa kizota zilitosha kazisaa kutatua tatizo la umeme na kumega umeme mmwingine kuuza nchi za nje. Jamani oneni haya kwa- nza na ndipo muchambue ubaya wa kikwete! Whoeve has ears ought to hear!mwenye masikio na asikie!
   
 3. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mwenye
  kudhulumu na azidi kudhulumu;
  na mwenye uchafu na azidi
  kuwa mchafu; na mwenye haki
  na azidi kufanya haki; na
  mtakatifu na azidi kutakaswa.
  (Soma Ufunuo wa Yohana
  22:11)
   
 4. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Aksante kwa kutuwekea number za wachangiaji wako hewani. Endelea na moyo huo huo. Teh teh teh teh. Ila sio vizuri Ungefuta japo number mbili za mwisho kwa kila mchangiaji.


  Kuhusu mada ni kweli kabisa. Kuna watu

  • wanashindwa kutoa sifa sababu sifa zile zitamlenga mtu fulani
  • Wanashindwa kukosoa kitu sababu ukosoaji huo utamenga mtu wa kundi lake.
   
 5. f

  fazili JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,192
  Likes Received: 404
  Trophy Points: 180
  matokeo ya udini yataonekana baadaye zaidi na itakuwa kilio na kusaga meno!!!!
   
Loading...