Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,267
Je unajua kinachoitafuna Mbeya City hadi kushangaza wengi?
nitarudi hapa na habari za kiuchunguzi
nitarudi hapa na habari za kiuchunguzi
Mbeya City ambayo iliwika sana msimu wa 2013/14 imeshindwa kukidhi matakwa ya wengi msimu huu baada ya kuambulia vichapo nyumbani na ugenini hali ambayo si ya kawaida kabisa. Why?
Mbeya City ilianza vizuri sana kwa kuungwa mkono na wakazi lukuki wa Mbeya iliwemo Halmashauri yenyewe na wafanyabiashara nguli
Upepo ulibadilika ghafla baada ya wanasiasa kupenyeza ajenda zao ambazo zilionekana kuungwa mkono na wanazi wa Mbeya City na hivyo kudhoofisha waliokua na nia njema kabisa ya kuisaidia timu hiyo bila kuegemea mrengo wa siasa.
Moja ya kundi lililoiathiri sana Mbeya City ni kundi la wafanyabiashara wakubwa ambao walihanikizwa kutoiunga mkono tena timu hiyo baada ya kuonekana kuwa na mtengo wa kushoto kisiasa na athari moja kubwa ilikua ni pale wafanyabiashara hao waliojitolea kuiweka timu hiyo kwenye hoteli moja iliyo chini ya usharika fulani wa kidini lakini ghafla wakajitoa baada ya kuona mwelekeo wa kushoto matokeo yake timu ikawa kwenye deni kubwa..hata ahadi kadhaa kama vile kununuliwa basi na kusaidiwa kujenga uwanja zimetoweka ghafla na tunakoelekea hata washabiki waandamizi huenda wakakosa udhamini kabisa kwani mechi ya Mgambo zilikwenda Coaster mbili tu na huenda ya Stand hakuna kabisa iliyoenda.
Sasa timu hiyo imebaki ukiwa na haina a very strong financial support ambayo ilifanya kucheza kwa kujituma muda wote, wachezaji wengi wamekopwa usajili .(ama ilivyo kwa Simba) hamkani si shwari tena.
Nitakuja tena na upande mwingine wa story