Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
WANAUKUMBI: Naona kuna mpya imeingia hapa kuhusu udini. Mada hii ni nzuri lakini walioanzisha lazima wawe na ustahamilivu wa kupokea mawazo pingamizi. Ikiwa watakubali hilo basi hapana shaka mjadala utastawi. Kwa kuanza mimi naanza na swali. Je tuko hadhir na historia ya vyama vya siasa kuanzia African Association 1929 hadi TANU 1954 mpaka leo CCM?

Ningependa kuwasikia wanaukumbi katika hilo ili nami Insha Allah nichangie kwa yale ninayoyajua kuhusu somo hili.
 
"If you want to please everybody, you will end up pleasing none"- Haiwezekani kumridhisha kila mtu na matakwa yake kama walivyokwish changia wengine, dini ya mtu haina maana sana na sio vyema ikahusishwa na nafasi yake kwenye chama chochote au serikali, kinachopaswa kuangaliwa hapa ni competence ya mtu kwa nafasi aliyopewa. Tukisema tuanze kuangalia nani wa dini gani yuko wapi hatutafika. Tuna mambo mengi na mazito sisi kama Taifa ya kuzungumza hasa kipindi hiki tunachoelekea kutoa maamuzi mazitpo kabisa juu ya mustakabali wa tanzania yetu kwa miaka mingine mitano! Great Thinkers discuss issues not people!
 

It is now getting interesting.

Hivi pesa ya kujenga UDOM ilitoka wapi?????

Najua Chuo Kikuu Cha Tanzania (UDSM) kilijengwa na Mayahudi. Sasa? Nini lengo hasa la UDOM? Chuo kikubwa kama kile hakiwezi kujengwa within 3 years. Marekani na uwezo wao wote hawajamudu kusimamisha WTC, now 9 years on.

Can you swallow that?

Hapa kuna wanaharakati wana yao jamani.
 
Jamani tuache udini hjaijarishi kama ni nani kwa sasa wanaongoza CCM tunachokaa ni ule ubaradhuri na ghiriba zao walizonazo wao kama binadamu lakini si dini yao

haijalishi hata viongozi wote wa CCM na kiamati zake wangekuwa waislamu, hapa suala sio udini, tuache siasa za udini mi nilidhani kuwa mambo haya Tanzania yalishaisha, watu waingie madarakani iwe kwenye vyama au nchi kwa uwezo wao na si kwa dini zao, kushabikia na kuanza kuulizia ulizia dini za viongozi iwe wa chama au wa nchi ni udini mbaya kuliko kitu chochote..tuache udini jamani, huo ni udini na tuupige vita..acha wawe waislamu, wawe wakristu hapa pointi ni nini wameifanyia Tanzania, na kama wameshindwa kudeliver ni kwa uwezo wao mdogo wa kuongoza na si kwa kuwa ni waislamu au wakristo sipendi udini naukataa na kuupiga vita na sipendi kuushabikia kabisa..ni hayo tuu
 
Tanzania ya leo bado mnaongelea UDINI?Mnaanza ubaguzi bila ya ninyi kujijua na mwisho wake ni mbaya.
 
 

Rev. unakosea kunapokuwa na uwiano wa namna hiyo itatugharimu hasa kwenye maamuzi makubwa ya nchi ikiwa tu uwiano huo utafikia kwenye vyombo kama baraza la mawaziri pamoja na bunge na mahala penginepo! tuliangalie hili kwa umakini wandugu.
 
Mimi nadhani mtoa hoja ni msahaulifu au anajidai hakumbuki hata uongozi wa CCM uliopita. Mwenyekiti Bejamini William Mkapa, Katibu Mkuu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti Bara John Malecela, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Abeid Karume. Sasa hapa tuseme uongozi uliopita ulikuwa na udini(Ukiristo)? Manake Karume pekeyake ndio alikuwa Muislamu. Labda una chuki na waislamu wakishika madaraka kwa vile walipokuwepo wakiristo wengi hakuna aliyesema kuna udini. Usiwe biased, kuwa fair ni michakato tu ikifanyika wanaweza kupatikana waislam au wakiristo. Usitake kutugawa kwa misingi ya dini ni mbaya sana kwa taifa letu.
 
Katika mambo yasiyohitaji mwongozo wa katiba bali busara za viongozi ni masuala ya tofauti zilizopo kimaumbile, kidini, kikabila na kielimu. Mfano hakuna mtu atakuzuia kama Rais ukichagua baraza la mawaziri kisha ukakuta baraza lote la mawaziri ni maprofesa tu. Au wa dini fulani tu au kabila fulani tu au pengine ni wanawake watupu. Lakini lazima malalamiko yatakuwepo.

Kwenye suala la kulalamika tunazidiana. Kuna makabila kwa mfano yamewahi kuweka robo tatu ya wafanyakazi wa ngazi kubwa kwenye shirika moja, na malalamiko hayakuwa makubwa. Na mashirika mengine yapo ambayo si ya kidini lakini asilimia mpaka 99 ni wa dini fulani tu na malalamiko hakuna.

Sasa ikitokea shirika la Umma likawa na wakristo asilimia 90 je ni kwamba waislamu na watu wa dini zingine wenye uwezo na kutaka kufanya kazi hapo hawapo?

Kama ingekuwa wakuu wa wilaya asilimia 100 ni waislamu je ni kwamba watu wa dini zingine wanaofaa hawapo?

Maswali haya yanaturudisha kwenye busara kwamba kwa nchi kama Tanzania ni lazima uchaguzi wa viongozi uende zaidi ya uwezo na vigezo.
Kwanza uwezo na vigezo vizingatiwe, kisha tujue Tanzania hii ina masuala ya bara na visiwani, ina masuala ya dini mbalimbali, madhehebu mbalimbali, makabila mbalimbali, wanawake kwa waume, watu wenye mahitaji maalumu n.k. Hivyo kwenye ngazi mbalimbali ikitumika busara hakutakuwa na matabaka wala maswali wala kudhoofika kwa umoja wa watanzania.

Hivyo si vizuri kuendekeza udini katika nchi kama Tanzania kwa kuwa nchi yetu si ya kidini.

Niko tayari kuongozwa na mtu wa dini yeyote, lakini siko tayari kuongozwa na watu wa dini moja tu ndani ya taifa langu.
 
"Kunya nye kuku akinya bata kaharusha chambilecho wahenga", uko sawa mno ndugu asam.thegunner. Wakati ule wa Mkapa haikuonekana kuwa ni udini kuwa ni viongozi wengi wa dini kutoka imani fulan, lakini sasa imekuwa tatizo.

 
ccm wadini ndiyo maana walikuwa tayari kuweka mahakama ya kadhi kwenye ilani yao wakijua hayo ni mambo ya kiislamu.hii inatokana na kuwa tu viongozi wa juu ni waislamu
 
Kimsingi hapa wengi wa wanaotetea hoja hii ni Chademaniacs, sababu wanazo skendo za udini na uchaga ndiyo maaana wanataka kurudisha haya makombora kwa CCM.
Tafadhali kubalini mapungufu yenu, na mtashikwa pabaya tu hiyo Oktoba, pia mvumilie maumivu.
Nyerere alishautoa UCHAGA katika mambo ya Utawala kwa sababu za nepotism,lakini alitete suala la dini kuwa si tatizo katika utawala.
KWA HIYO MNATAKA KUTUAMBIA CHAMA GANI KIPO 50-50 KTK DINI KAMA SIYO CCM.
CUF=WAISLAM,WAPEMBA.
CHADEMA=WAKRISTO,WACHAGA.
TLP= WAKRISTO, WACHAGA.
NCCR=WAKRISTO,WACHAGA.
CCM= DINI ZOTE , KABILA ZOTE.

SIJUI MNA LIPI LA KUONGEZEA WADAU HAPA.

TUACHE HAYA MAMBO YA UDINI.:hand:
UKIJUA KULA NA UJUE KUNYA PIA.:blah:
 
Nadhani ingekuwa vizuri sana kama Watanzania tukajenga hoja endelevu na ambazo haziwezi kugawa nchi, Suala la Uislam na Ukistro kuhusishwa na vyama vya siasa tena kwa kukumbushia historia halina msingi wowote. Waislamu walishawahi kulalaimika katika Uongozi wa Mkapa (Mkistro) pale Mauaji ya kutisha ya Mwembechai yalipotokea na watu kuuliwa ndani ya msikiti, na kanakwamba haitoshi pia mauji yaliyotokea Zanzibar nayo yalipigiwa kelele. Wakristo walisimama kidete kupinga Kadhi na OIC katika awamu hii hii ya Kikwete (Muislam), hawa wote ni Viongozi wa CCM. Sasa je CCM = Christian Church Movement? Au CCM = Chama cha Mujahidina?

Tuangalieni Mustakabali wa Maendeleo ya nchi na kubadirisha utawala ambao nusu karne imepita maendeleo hakuna. Tusijenge hoja za Udini ambazo pande zote mbili wana ushahidi wa kutetea dini yao.
 
CCM ya leo siyo siri ni wa dini, hata apointments mbalimbali serikalini siku hizi ni dini flani,
that is not health for the country's unit.
 
du noma sasa udini huu balaaa.... We need people of high capasity of COMPITANCE, PERFORMANCE, DELIVERLY etc..... dini si hoja jamani.... percentage wise ingekuwa 50/50... Someone could have gone for ukabila..... uzanzibar/utanganyika etc... let us close this issue of politics based on religions.... i stand to be corrected.....


CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA.......................................
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…