Udikteta wa Rais Magufuli uko wapi?

Udikteta wa Rais Magufuli uko wapi?

Wakati wa mchakato wa kutengeneza katiba mpya, tuliona jinsi utawala wa Kikwete ulivyokatisha ndoto kubwa ya watanzania wengi wenye uelewa kupata Katiba ya Warioba iliyokuwa na maudhui mengi yaliyokuwa yakipendelewa sana na ''ma-elites'' nchi nzima. Hata hivyo, wengi walifurahia sana baada ya mchakato wa kuipigia kura katiba hiyo pendekezwa uliposhindikana.

Hata hivyo ukichunguza kwa makini kampeni za vyama vya upinzani katika kipindi kile cha kuhamasisha umma cha 2014, utagundua kuwa masuala mengi ambayo vyama vya upinzani hasa CHADEMA, vilivyokuwa vikiyapigania, yameanza kushughulikiwa na Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambayo si mimi, wala mwana-CCM ama mpinzani aliyetarajia huyu jamaa angeyafanya yote hayo na ndani ya kipindi kifupi sana.
Kwa ajili ya kupanua mjadala, tushirikiane tuyajadili vyema ili tumhukumu kwa haki Rais huyu.

Hivi tunaifahamu vyema nchi yetu, je ni haki tumhukumu Rais wetu kwa sababu hataki bunge liwe live, au kwa sababu sukari imepanda bei? Uwezo wetu wa kufikiri ndio umeishia hapo ama?

Nikiri wazi mi ni mpenzi mkubwa sana wa plurality katika siasa ambapo hakuna Chama kinacho-dominate vyama vingine. Mwenye uelewa mzuri wa Comparative Politics atakiri kuwa, kati ya CCM na CHADEMA/UKAWA, anayepaswa kushangilia kwa anayoyafanya Rais Magufuli ni CHADEMA/UKAWA kwa sababu anawasomesha namba vibaya sana wana-CCM, huku akitekeleza yale ambayo wapinzani waliyataka.

Nani atasumbuka kuangalia bunge live wakati Rais anaonekana moja kwa moja akitekeleza watu wanayoyataka na hivyo kupelekea bunge kupitisha kila kitu.
Jamani wapinzani nyie ndio mlio win kuliko wana-CCM, fikirieni mara mbili mbili.

Duu!!! VERY PATHETIC.
 
Sawa hata mimi ninaamini suala la siasa aliache liendelee bila kubughudhiwa. Ni vizuri vyama viwe huru kufanya siasa lakini ninavyomuona ni kwamba anasumbuka kutokana na kuzunhukwa na watu wengi wasio waaminifu huku wengi wao wakiwa na majeraha ya mirija ya madili yao kukata ghafula.

Ndiyo maana naomba tumsaidie Rais huyu maana ukichambua kwa makini utagundua kuwa ni bahati sana kuwa na Rais wa aina yake - yaani mtu ametokea ndani ya Chama tawala halafu akafanya mageuzi makubwa kiasi hicho? Tujiulize alikuwa na shida hiyo ya kujipendekeza kiasi hicho kiasi cha kutishia nafasi yake ya uenyekiti ndani ya Chama chake.

Hivi kwani vipaumbele vyetu kama taifa ni nini, kwa nini tusimhukumu kwa kuangalia jinsi anavyotumia rasilimali za umma? kuna kigezo kikubwa zaidi ya hicho?

Ukimuita Magufuli dikteta kwani nani anaweza kutudanganya kuwa demokrasia ni nzuri
muda wote? Kati ya Benevolent Dictator na laissez-faire democrat nani mzuri katika nchi za dunia ya tatu?

Jamani wote tunatamani abadilisha baadhi ya masuala kama la uhuru wa kisiasa lakini huyu jamaa bado ni mzuri ile mbaya. Tusisahau kuwa katika jamii za kiafrika, furaha ya wengi (japokuwa hawana ufahamu mzuri) ni zaidi ya furaha ya wachache, na hiyo ndiyo demokrasia.
Benevolent Dictator??? Sheeeesh! more like a malignant lingering dictator
Naona unaungana naye kuwa ni almighty,omnipotent,great sage,all wise Budhaa ni mjuvi wa kila kitu hakosei hivyo hastaili kukosolewa
Trump alikuwa sawa Watz kama wewe hamstahili kuwa huru
 
Ni aibu na Wendawazimu kumpinga JPM kama Rais, kwani yote anayoyafanya ndiyo ambayo yanamanufaa kwetu Watz, lakini ukimuona mtu tena Mtanzania anampinga Rais ujue kuna mawili; aidha ni Mgonjwa wa akili kama Lisu au ni mmoja wa ndugu wa Mafisadi ya Kaskazini ambayo hayataki kuona viongozi wa juu hususan Rais akitokea Kanda ya ziwa. Kuna ka SACCOS kamoja kamekuwa kakitafuta viongozi wake ambao lazima waoe kwa Muasisi wa SACCOS hiyo, Muasisi mwenyewe ni yule aliyewahi kumtaka Baba wa Taifa kufanya jambo kipumbavu la kushusha thamani ya shilingi ili kukidhi matakwa ya mabepari yaliyokuwa yamempa HONGO muasisi wa SACCOS hiyo.
Kakojoe ulale uliyoyaandika haps ni fedheha kwa JF wewe kuwa member wake
idiot
 
Wakati wa mchakato wa kutengeneza katiba mpya, tuliona jinsi utawala wa Kikwete ulivyokatisha ndoto kubwa ya watanzania wengi wenye uelewa kupata Katiba ya Warioba iliyokuwa na maudhui mengi yaliyokuwa yakipendelewa sana na ''ma-elites'' nchi nzima. Hata hivyo, wengi walifurahia sana baada ya mchakato wa kuipigia kura katiba hiyo pendekezwa uliposhindikana.

Hata hivyo ukichunguza kwa makini kampeni za vyama vya upinzani katika kipindi kile cha kuhamasisha umma cha 2014, utagundua kuwa masuala mengi ambayo vyama vya upinzani hasa CHADEMA, vilivyokuwa vikiyapigania, yameanza kushughulikiwa na Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambayo si mimi, wala mwana-CCM ama mpinzani aliyetarajia huyu jamaa angeyafanya yote hayo na ndani ya kipindi kifupi sana.
Kwa ajili ya kupanua mjadala, tushirikiane tuyajadili vyema ili tumhukumu kwa haki Rais huyu.

Hivi tunaifahamu vyema nchi yetu, je ni haki tumhukumu Rais wetu kwa sababu hataki bunge liwe live, au kwa sababu sukari imepanda bei? Uwezo wetu wa kufikiri ndio umeishia hapo ama?

Nikiri wazi mi ni mpenzi mkubwa sana wa plurality katika siasa ambapo hakuna Chama kinacho-dominate vyama vingine. Mwenye uelewa mzuri wa Comparative Politics atakiri kuwa, kati ya CCM na CHADEMA/UKAWA, anayepaswa kushangilia kwa anayoyafanya Rais Magufuli ni CHADEMA/UKAWA kwa sababu anawasomesha namba vibaya sana wana-CCM, huku akitekeleza yale ambayo wapinzani waliyataka.

Nani atasumbuka kuangalia bunge live wakati Rais anaonekana moja kwa moja akitekeleza watu wanayoyataka na hivyo kupelekea bunge kupitisha kila kitu.
Jamani wapinzani nyie ndio mlio win kuliko wana-CCM, fikirieni mara mbili mbili.
Kama mnakubalika na kuungwa mkono na watu wengi kabisa mnahofu ya nini juu ya watu kiduchu ambao hawawaungi mkono!!!? si muwaache tu wajitembelee zao kwa miguu umbali wanaotaka wakichoka wajiendee majumbani kwao kujilalia zao??!
KAMA SII KUCHANGANYIKIWA NI NINI BASI???!
 
Nani atasumbuka kuangalia bunge live wakati Rais anaonekana moja kwa moja akitekeleza watu wanayoyataka na hivyo kupelekea bunge kupitisha kila kitu.
Jamani wapinzani nyie ndio mlio win kuliko wana-CCM, fikirieni mara mbili mbili.

Ndio think tank huko kwenu
 
Mtoa hoja umeeleweka vizuri sana. Hata kwa maoni yangu mimi nadhani Mheshimiwa rais Magufuli hata baada ya miaka michache tu ya yeye kuwa rais, atatuletea mabadiliko chanya makubwa sana katika nyanja mbalimbali. Kwa kadri walivyo watanzania hasa wa mijini na vijiweni, bila bakora za maana nchi yetu itachelewa sana kupiga hatua za maendeleo. Naomba kumshauri mheshimiwa rais Magufuli kuwa, huu ni wakati wa yeye kuwa mkali zaidi. Bila rais Magufuli kuwa m'babe, tutaishia tu kupiga marktime katika maendeleo.
 
Hata suala kuhamia Dodoma kwa wenye uelewa watakubali siyo gumu kihivyo endapo kuna ''will''. Mwaka 1998, wakati Chancellor wa Ujerumani Gerhard Schroeder ameapishwa madarakani aliharakisha pia kwa namna ya ajabu Makao Makuu kutoka Bonn kwenda Berlin ndani ya muda mfupi (usiseme kuwa ni nchi tajiri) japokuwa Helmut Kohl aliyeiunganisha Ujerumani 1990, alikaa miaka nane zaidi (1990 - 97) bila kuhamishia huko - why? Kwa nini wajerumani walikubali kupeleka Makao Makuu katika eneo masikini nchini humo?
Tunakimbilia kudai mji wa Dodoma hauna miundombinu ya kutosha, sijui nini, wala hiki lakini angalia hizi ni changamoto zilizokumba nchi zote walikohamisha miji mikuu yao - Brazil (Rio to Brasilia), Australia (Sydney to Canberra), India (Delhi to New Delhi), Nigeria (Lagos to Abuja) na mingine mingi.
Hivyo kwenye changamoto na utatuzi wake ndio kipimo kizuri cha kumpima Rais huyu na kum-rank kwa usahihi nafasi yake miongoni mwa marais waliopata kuiongoza nchi yetu.
Nina hamu tu kusikia kauli yetu akitamka kuwa tutaanza upya mchakato wa Katiba mpya. Otherwise hadi sasa mambo yanaenda vizuri tena vizuri sana.

Marekebisho Helmut kohl alikuwa chancellor kwa niaka16 sio8 mji mkuu wa India uhamishwa toka culcata kwenda New Delhi sio delhi to new Delhi

Sio kweli kuwa Berlin ni eneo maskini.ujureumani mji mkuu urudishwa Berlin baada ya ujerumani kuungana Berlin is not a poor city
 
Back
Top Bottom