Udikteta wa Rais Magufuli uko wapi?

Udikteta wa Rais Magufuli uko wapi?

Kutoka Gazeti la Mwananchi

By Idd Hamis

Inaelekea kuna ‘bundi’ anainyemelea nchi yetu taratibu na huenda watu wamechoka amani iliyopo.

Kutunishiana misuli kunakoendelea kati ya Chadema na Serikali hakuashirii heri hata kidogo.

Chadema kimetangaza uamuzi wa mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho kwamba Septemba mosi itakuwa siku ya kufanya mikutano na maandamano ya amani kupinga walichokiita “utawala wa kidikteta”.

Kwa sisi tuliosoma shule enzi za chama kimoja cha siasa na kuijua vyema historia ya nchi yetu, siku hiyo ilikuwa siku ya mashujaa kuwaenzi wale wote waliokufa wakipigania uhuru na heshima ya nchi yetu.

Nimetafakari mantiki ya Chadema kuichagua siku hii na kauli zinazotolewa na Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), naona nchi inaelekea kwenye mgongano ambao kama busara hazitotumika damu janga kubwa linaweza kutokea.

Kauli hizo ni kama ile aliyoitoa Rais akiwa mkoani Singida aliposema: “Wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanawatumia wakawaeleze vizuri”.

Maana yake ni kwamba Chadema wanapoazimia kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima wanamjaribu Rais kama atavitumia vyombo vya dola kuwadhibiti na yeye hayuko tayari kujaribiwa. Msimamo huu unapingwa kwa nguvu zote na Chadema kupitia Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salim Mwalimu, siku aliyozungumza na waandishi wa habari na kusema:

“Hatutorudi nyuma, mkakati wetu wa Septemba Mosi uko palepale”. Kwa kweli kwa kauli hizi naona giza kubwa linalinyemelea Taifa letu.

Kwa kuichagua Septemba Mosi, nadhani Chadema wanataka kutuma ujumbe kwamba wao wako tayari kuingia katika orodha ya mashujaa wa nchi hii, kwa maana kuwa wamejiandaa kutekeleza maamuzi yao hata ikibidi kujitoa mhanga.

Marufuku ya shughuli za kisiasa

Rais amepiga marufuku shughuli zozote zile za vyama vya siasa kufanyika nje ya maeneo ya wanasiasa husika. Akisisitiza hili , rais alisema: “siyo mtu unatoka Hai kwenda Kahama kushawishi watu wafanye fujo”.

Yako masuala kadhaa ya kujadili hapa. Kwanza, je katiba ya nchi au niseme sheria inasemaje kuhusu Mtanzania kutoka shemu moja kwenda sehemu nyingine kufanya siasa? Je, mikutano ya hadhara na maandamano ni fujo?

Jibu la swali la kwanza, Katiba ya nchi yetu inamruhusu Mtanzania kufanya shughuli za kisiasa mahali popote ndani ya nchi alimradi havunji sheria.

Ndiyo maana moja ya masharti ya kusajiliwa chama chochote kile cha siasa nchini ni lile la kuwa na wanachama kutoka pande zote mbili za Muungano na chama kisichokidhi matakwa haya ya kisheria kinaweza kufutiwa usajili.

Kwa hiyo kumzuia Mtanzania wa chama chochote kile kufanya shughuli za kisiasa ikiwa ni pamoja na mikutano ya hadhara na hata maandamano ambayo yanatambulika kisheria ni kumnyima haki yake ya kikatiba na ni kuvunja sheria.

Utawala wa sheria dhidi ya sheria za utawala

Sakata linaloendelea kati ya Serikali na Chadema ni kilelezo cha wazi cha kutamalaki kwa sheria za utawala, badala ya utawala wa sheria nchini Tanzania.

Katika nchi ya kidemokrasia, ainisho la utawala wa sheria linasema utawala wa sheria ni hali ya kuweko vizuizi vya kisheria kuzuia maamuzi ya kiimla na udhibiti wa kisheria kwa ajili ya kumlinda mwananchi na kuwepo utaratibu na uwazi wa kisheria.

Katika nchi yenye utawala wa sheria huwezi kukuta mgongano kati ya sheria na maamuzi au matamko ya viongozi.

Kwa mfano, huwezi kukuta sheria inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa, huku viongozi wanaweka mpaka wa mikutano hiyo kwamba ifanyike katika maeneo ya viongozi husika tu au nyakati za uchaguzi pekee.

Viongozi wa vyama vyote vya siasa wako huru kwenda mahali popote pale katika nchi kufanya shughuli za kisiasa iwe ni kukutana na wanachama wao katika mikutano ya ndani au kukutana na wananchi katika mikutano ya hadhara.

Si busara hata kidogo kuwazuia viongozi wa vyama vya siasa wa kitaifa au hata kama si wa kitaifa kwenda sehemu yoyote ya nchi kufanya siasa, kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya viongozi na chama cha siasa.

Utawala wa sheria maana yake ni kuhakikisha kutumika kwa sheria kama zilivyokusudiwa na siyo kuzipa tafsiri waitakayo watawala. Kufanya hivyo ndiko kunakohakikisha kwamba haki za wananchi zinalindwa na haki za watawala pia zinalindwa.

Kinyume cha utawala wa sheria ni kile kiitwacho ‘sheria za utawala’au kwa Kiingereza; ‘Law of rule’. Hali hii hutokea pale ambapo utawala unatoa amri zake kinyume cha sheria hali ambayo hukaribisha upinzani kutoka kwa wananchi.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wa kada mbalimbali kwamba nchi yetu imeanza kubobea kidogo kidogo kwenye sheria za utawala.

Wataalamu wa mambo ya sheria na katiba wanasema kukosekana kwa utawala wa sheria na kutamalaki sheria za utawala, ni hali inayoweza kujitokeza katika nchi zote, zile za kidemokrasia na hata zile za kidikteta.

Ndiyo maana wakaja na msamiati “dictatorial democracy” yaani demokrasia ya kidikteta au ya kiimla kwa lugha nyepesi. Kinachoendelea katika nchi yetu hii ya kidemokrasia ni sheria ya utawala badala ya utawala wa sheria.

Wakati wa mchakato wa kutengeneza katiba mpya, tuliona jinsi utawala wa Kikwete ulivyokatisha ndoto kubwa ya watanzania wengi wenye uelewa kupata Katiba ya Warioba iliyokuwa na maudhui mengi yaliyokuwa yakipendelewa sana na ''ma-elites'' nchi nzima. Hata hivyo, wengi walifurahia sana baada ya mchakato wa kuipigia kura katiba hiyo pendekezwa uliposhindikana.

Hata hivyo ukichunguza kwa makini kampeni za vyama vya upinzani katika kipindi kile cha kuhamasisha umma cha 2014, utagundua kuwa masuala mengi ambayo vyama vya upinzani hasa CHADEMA, vilivyokuwa vikiyapigania, yameanza kushughulikiwa na Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambayo si mimi, wala mwana-CCM ama mpinzani aliyetarajia huyu jamaa angeyafanya yote hayo na ndani ya kipindi kifupi sana.
Kwa ajili ya kupanua mjadala, tushirikiane tuyajadili vyema ili tumhukumu kwa haki Rais huyu.

Hivi tunaifahamu vyema nchi yetu, je ni haki tumhukumu Rais wetu kwa sababu hataki bunge liwe live, au kwa sababu sukari imepanda bei? Uwezo wetu wa kufikiri ndio umeishia hapo ama?

Nikiri wazi mi ni mpenzi mkubwa sana wa plurality katika siasa ambapo hakuna Chama kinacho-dominate vyama vingine. Mwenye uelewa mzuri wa Comparative Politics atakiri kuwa, kati ya CCM na CHADEMA/UKAWA, anayepaswa kushangilia kwa anayoyafanya Rais Magufuli ni CHADEMA/UKAWA kwa sababu anawasomesha namba vibaya sana wana-CCM, huku akitekeleza yale ambayo wapinzani waliyataka.

Nani atasumbuka kuangalia bunge live wakati Rais anaonekana moja kwa moja akitekeleza watu wanayoyataka na hivyo kupelekea bunge kupitisha kila kitu.
Jamani wapinzani nyie ndio mlio win kuliko wana-CCM, fikirieni mara mbili mbili.
 
Mijini watu wengi sana hawitaki Chadema hata kidogo, angalia matokeo ya kura, siyo kweli kwamba ccm ilikuwa inapata sifuri. Na pia siyo kweli kwamba kijijini eti watu hawana uelewa juu ya shida zao, pia ni kuwadhalilisha kuwachukulia wananchi hao kuwa eti vyama vya upinzani eti havijawafikia. Ukweli ni kwamba Vyama vya upinzani vinaendesha siasa za matukio badala ya sera. Hata wewe ndugu yangu unayedai eti havijajieleza vijijini, nikikuuliza Chadema ina sera gani juu ya kuwaletea maji safi na salama Watz? Inasemaje sera yao kuhusu Elimu bora? Wanasemaje kuhusu miundo mbinu bora, Kuhusu Afya wana sera gani, kuhusu watoto, watu wenye ulemavu n.k ukitoa maelezo na hata kupost andiko la sera za Chadema inayosema juu ya hayo, mimi unitumie Namba zako nikuMpesa sasa hivi Tsh 20, 000/=
 
Watanzania tumechoka kusikia kelele zao. Magufuli ndiye mkombozi wa watanzania walio wanyonge. Hata mfanye nini lakini rais Magufuli ataendelea tu kuwa mkombozi wa watanzania.
 
Kuvunja katiba haijawahi kuwa sera ya CHADEMA. Hatukumwambia JPM anyakue sera zetu na sisi atufunge midomo!!! Hata mwanafunzi anayeibia majibu Darasani hawezi kufanya kwa ufanisi kuliko yule anayeibiwa. Angeruhusu akakosolewa angetekeleza vizuri zaidi hizo sera alizoibia.No No NO. I will be the last person to support dictatorship.

Mangikule, ni vizuri tutoe haki panapohitajika. Tusijidanganye kuwa mabadiliko ya serikali yanaleta mabadiliko chanya kwa wananchi muda wote. Uzoefu uliopo hapa Afrika ni kuwa, hakuna nchi yoyote kubwa iliyoboresha maisha ya wananchi wake baada ya kubadilisha Serikali. Hivyo siyo CDM wala CUF ambavyo vitaleta maendeleo kama wananachi wenyewe ndio hao. Fuatilia nchi kubwa za Ethiopia, Kenya, DRC, Nigeria, Sudan, Libya, Zambia, Madagascar nk. Hiyo ni kwa sababu maendeleo hayaletwi na serikali bali wananchi wenyewe. Kazi ya kuunda ''strong institutions'' siyo ya serikali ni ya wananchi kama jamii na ndiyo maana tunafanya makosa makuba sana ku-overlook familia kama institution muhimu kuelekea mabadiliko.
 
Tusipoteze hoja za msingi kwa visingizio vya wajibu wa kiongozi kutenda vizuri ni wajibu wa Rais sasa kama anageuza wajibu wake kwa adhabu ya kuzuia fikra huru toka vyama pinzani basi uzuri wa wajibu wake unapotea kama ni kiongizi mzuri ajue anatakiwa kuacha fikra huru zitamalaki kuanzia bungeni mpaka kwa mwananchi mmoja mmoja afu aone ukawa watamwita dikteta tena? Lakini asikomoe watu kwa kisingizio anatekeleza mawazo ya wapinzani siwezi kuunga mkono udikteta wa hivyo.
Mnamuonea bure Rais kwani ukifuatilia matamko yake, utaona kuwa, hayatoi kwa nia mbaya ya kumuumiza mtu isipokuwa ni njia yake ya kusisitiza jambo. Uwezo wa kuongea (oratory) ni mojawapo ya karama tulizojaliwa na Mungu hivyo siyo wote wenye uwezo huo na ukizingatia Rais alikuwa mwanasayansi.
Ndiyo maana najiuliza sana, hivi ndio uwezo wetu ulipoishia kuona aina ya kiongozi tulinaye? Mimi ninavyozifahamu tabia za viongozi wa kiafrika, hata kama CDM, wangechukua nchi, wasingeweza kuyafanya haya anayofanya Magufuli - zaidi wangeishia kuwaweka ndani watawala waliopita huku wakigawa vyeo vya asante kwa wanachama na manazi wa Chama hicho - halafu wangefikiri wamefanya mabadiliko chanya.

Tunatafuta udhaifu wa Rais, hivi tunataka awe ''an ideal'' kwa kila kitu hivi itawezekana kweli? Alifanya vyema kwenye wizara ya miundombinu tukamfurahia, Kikwete akamdis akampeleka wizara ya kitoweo akasababisha wizara hiyo kuwa maarufu kuliko zingine huku miundombinu ikichechemea hadi akarudishwa, alitutajia hadi idadi ya samaki waliomo ziwa Victoria pamoja na urefu wa mbarabara yetu tukawa tunashangaa, sasa tunataka awe perfect kila kitu. Kwani sisi mbona tuna madhaifu kibao tu?
 
Yanaenda vzr kwa mtizamo wako,Kwan Shroeder alizuia vyama vya siasa kuendesha shugli zao kama jpm anavofanya?
 
Wakati wa mchakato wa kutengeneza katiba mpya, tuliona jinsi utawala wa Kikwete ulivyokatisha ndoto kubwa ya watanzania wengi wenye uelewa kupata Katiba ya Warioba iliyokuwa na maudhui mengi yaliyokuwa yakipendelewa sana na ''ma-elites'' nchi nzima. Hata hivyo, wengi walifurahia sana baada ya mchakato wa kuipigia kura katiba hiyo pendekezwa uliposhindikana.

Hata hivyo ukichunguza kwa makini kampeni za vyama vya upinzani katika kipindi kile cha kuhamasisha umma cha 2014, utagundua kuwa masuala mengi ambayo vyama vya upinzani hasa CHADEMA, vilivyokuwa vikiyapigania, yameanza kushughulikiwa na Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambayo si mimi, wala mwana-CCM ama mpinzani aliyetarajia huyu jamaa angeyafanya yote hayo na ndani ya kipindi kifupi sana.
Kwa ajili ya kupanua mjadala, tushirikiane tuyajadili vyema ili tumhukumu kwa haki Rais huyu.

Hivi tunaifahamu vyema nchi yetu, je ni haki tumhukumu Rais wetu kwa sababu hataki bunge liwe live, au kwa sababu sukari imepanda bei? Uwezo wetu wa kufikiri ndio umeishia hapo ama?

Nikiri wazi mi ni mpenzi mkubwa sana wa plurality katika siasa ambapo hakuna Chama kinacho-dominate vyama vingine. Mwenye uelewa mzuri wa Comparative Politics atakiri kuwa, kati ya CCM na CHADEMA/UKAWA, anayepaswa kushangilia kwa anayoyafanya Rais Magufuli ni CHADEMA/UKAWA kwa sababu anawasomesha namba vibaya sana wana-CCM, huku akitekeleza yale ambayo wapinzani waliyataka.

Nani atasumbuka kuangalia bunge live wakati Rais anaonekana moja kwa moja akitekeleza watu wanayoyataka na hivyo kupelekea bunge kupitisha kila kitu.
Jamani wapinzani nyie ndio mlio win kuliko wana-CCM, fikirieni mara mbili mbili.
hapa issue sio nani kawini issue ni Uhuru wa vyombo vya habari na demokrasia, na katiba bila hayo hakuna utetezi utakaomshawishi MTU mwenye akili huru
 
nchi inaenda kumeguka katika vipande vipande, mh asipokuwa makini, ona ya Zanzibar, hata kukimbilia dodoma ni dalili ya mpasuko, bado anataka siasa zifanywe ki kakinda kikabila. na kivyama, umoja wa kitaifa unayoyoma, kuna siku atajikuta yuko Dodoma peke yake
 
Wakati wa mchakato wa kutengeneza katiba mpya, tuliona jinsi utawala wa Kikwete ulivyokatisha ndoto kubwa ya watanzania wengi wenye uelewa kupata Katiba ya Warioba iliyokuwa na maudhui mengi yaliyokuwa yakipendelewa sana na ''ma-elites'' nchi nzima. Hata hivyo, wengi walifurahia sana baada ya mchakato wa kuipigia kura katiba hiyo pendekezwa uliposhindikana.

Hata hivyo ukichunguza kwa makini kampeni za vyama vya upinzani katika kipindi kile cha kuhamasisha umma cha 2014, utagundua kuwa masuala mengi ambayo vyama vya upinzani hasa CHADEMA, vilivyokuwa vikiyapigania, yameanza kushughulikiwa na Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambayo si mimi, wala mwana-CCM ama mpinzani aliyetarajia huyu jamaa angeyafanya yote hayo na ndani ya kipindi kifupi sana.
Kwa ajili ya kupanua mjadala, tushirikiane tuyajadili vyema ili tumhukumu kwa haki Rais huyu.

Hivi tunaifahamu vyema nchi yetu, je ni haki tumhukumu Rais wetu kwa sababu hataki bunge liwe live, au kwa sababu sukari imepanda bei? Uwezo wetu wa kufikiri ndio umeishia hapo ama?

Nikiri wazi mi ni mpenzi mkubwa sana wa plurality katika siasa ambapo hakuna Chama kinacho-dominate vyama vingine. Mwenye uelewa mzuri wa Comparative Politics atakiri kuwa, kati ya CCM na CHADEMA/UKAWA, anayepaswa kushangilia kwa anayoyafanya Rais Magufuli ni CHADEMA/UKAWA kwa sababu anawasomesha namba vibaya sana wana-CCM, huku akitekeleza yale ambayo wapinzani waliyataka.

Nani atasumbuka kuangalia bunge live wakati Rais anaonekana moja kwa moja akitekeleza watu wanayoyataka na hivyo kupelekea bunge kupitisha kila kitu.
Jamani wapinzani nyie ndio mlio win kuliko wana-CCM, fikirieni mara mbili mbili.
nchi inaenda kumeguka vipande vipande kama siasa zitafanywa kikanda kikabila na kivyama kama mhe. anavyotaka, kura mil 8.za magumashi alizopata hazijustify kwa anaungwa mkono na kila mtu
 
Vyama vya upinzani hasa Chama kikuu CHADEMA, jifunzeni misingi ya kukubalika kwa wananchi siyo kung'ang'ania watu wa mijini ambao ni obvious huwa ni wafuasi wa mageuzi na wala huwa hawasubiri swagga zenu. Nendeni vijijini muanzishe ofisi zinazofanya kazi la sivyo, vyama hivi vitalazimika kusubiri bahati kama ya Kenya kwamba Chama tawala kisambaratike kwanza ndio kipate wafuasi. Watanzania wengi bado wako vijijini, kwa nini vyama hivi visiende kujenga ofisi za wilaya (kwa kuanzia).
Yaani wanaccm, hivi isingekuwa Jecha wa Jecha mngebakia bara ila mlikuwa tayari kumwaga damu ilimradi Shein awe mkulu; na sasa tena bado watu mnawataka eti wakae kimya kisa matamko? kibaya zaidi mmeanza kupenyeza ukabila na ubaguzi mkubwa eti kila mtu afanye siasa kwenye sehemu yake tu!!! 😡😡😎😕 hata kama Mwl. Nyerere angekuwa hai kamwe asingekubaliana na hilo maana mkifanikisha hilo basi kesho mtasema kila kabila wafanye kampeni kivyao.😡 Jk. alikuwa dhaifu lakini mwenyeuelewa mkubwa mno juu ya siasa nini.
 
Kutoka Gazeti la Mwananchi

By Idd Hamis

Inaelekea kuna ‘bundi’ anainyemelea nchi yetu taratibu na huenda watu wamechoka amani iliyopo.

Kutunishiana misuli kunakoendelea kati ya Chadema na Serikali hakuashirii heri hata kidogo.

Chadema kimetangaza uamuzi wa mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho kwamba Septemba mosi itakuwa siku ya kufanya mikutano na maandamano ya amani kupinga walichokiita “utawala wa kidikteta”.

Kwa sisi tuliosoma shule enzi za chama kimoja cha siasa na kuijua vyema historia ya nchi yetu, siku hiyo ilikuwa siku ya mashujaa kuwaenzi wale wote waliokufa wakipigania uhuru na heshima ya nchi yetu.

Nimetafakari mantiki ya Chadema kuichagua siku hii na kauli zinazotolewa na Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), naona nchi inaelekea kwenye mgongano ambao kama busara hazitotumika damu janga kubwa linaweza kutokea.

Kauli hizo ni kama ile aliyoitoa Rais akiwa mkoani Singida aliposema: “Wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanawatumia wakawaeleze vizuri”.

Maana yake ni kwamba Chadema wanapoazimia kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima wanamjaribu Rais kama atavitumia vyombo vya dola kuwadhibiti na yeye hayuko tayari kujaribiwa. Msimamo huu unapingwa kwa nguvu zote na Chadema kupitia Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salim Mwalimu, siku aliyozungumza na waandishi wa habari na kusema:

“Hatutorudi nyuma, mkakati wetu wa Septemba Mosi uko palepale”. Kwa kweli kwa kauli hizi naona giza kubwa linalinyemelea Taifa letu.

Kwa kuichagua Septemba Mosi, nadhani Chadema wanataka kutuma ujumbe kwamba wao wako tayari kuingia katika orodha ya mashujaa wa nchi hii, kwa maana kuwa wamejiandaa kutekeleza maamuzi yao hata ikibidi kujitoa mhanga.

Marufuku ya shughuli za kisiasa

Rais amepiga marufuku shughuli zozote zile za vyama vya siasa kufanyika nje ya maeneo ya wanasiasa husika. Akisisitiza hili , rais alisema: “siyo mtu unatoka Hai kwenda Kahama kushawishi watu wafanye fujo”.

Yako masuala kadhaa ya kujadili hapa. Kwanza, je katiba ya nchi au niseme sheria inasemaje kuhusu Mtanzania kutoka shemu moja kwenda sehemu nyingine kufanya siasa? Je, mikutano ya hadhara na maandamano ni fujo?

Jibu la swali la kwanza, Katiba ya nchi yetu inamruhusu Mtanzania kufanya shughuli za kisiasa mahali popote ndani ya nchi alimradi havunji sheria.

Ndiyo maana moja ya masharti ya kusajiliwa chama chochote kile cha siasa nchini ni lile la kuwa na wanachama kutoka pande zote mbili za Muungano na chama kisichokidhi matakwa haya ya kisheria kinaweza kufutiwa usajili.

Kwa hiyo kumzuia Mtanzania wa chama chochote kile kufanya shughuli za kisiasa ikiwa ni pamoja na mikutano ya hadhara na hata maandamano ambayo yanatambulika kisheria ni kumnyima haki yake ya kikatiba na ni kuvunja sheria.

Utawala wa sheria dhidi ya sheria za utawala

Sakata linaloendelea kati ya Serikali na Chadema ni kilelezo cha wazi cha kutamalaki kwa sheria za utawala, badala ya utawala wa sheria nchini Tanzania.

Katika nchi ya kidemokrasia, ainisho la utawala wa sheria linasema utawala wa sheria ni hali ya kuweko vizuizi vya kisheria kuzuia maamuzi ya kiimla na udhibiti wa kisheria kwa ajili ya kumlinda mwananchi na kuwepo utaratibu na uwazi wa kisheria.

Katika nchi yenye utawala wa sheria huwezi kukuta mgongano kati ya sheria na maamuzi au matamko ya viongozi.

Kwa mfano, huwezi kukuta sheria inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa, huku viongozi wanaweka mpaka wa mikutano hiyo kwamba ifanyike katika maeneo ya viongozi husika tu au nyakati za uchaguzi pekee.

Viongozi wa vyama vyote vya siasa wako huru kwenda mahali popote pale katika nchi kufanya shughuli za kisiasa iwe ni kukutana na wanachama wao katika mikutano ya ndani au kukutana na wananchi katika mikutano ya hadhara.

Si busara hata kidogo kuwazuia viongozi wa vyama vya siasa wa kitaifa au hata kama si wa kitaifa kwenda sehemu yoyote ya nchi kufanya siasa, kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya viongozi na chama cha siasa.

Utawala wa sheria maana yake ni kuhakikisha kutumika kwa sheria kama zilivyokusudiwa na siyo kuzipa tafsiri waitakayo watawala. Kufanya hivyo ndiko kunakohakikisha kwamba haki za wananchi zinalindwa na haki za watawala pia zinalindwa.

Kinyume cha utawala wa sheria ni kile kiitwacho ‘sheria za utawala’au kwa Kiingereza; ‘Law of rule’. Hali hii hutokea pale ambapo utawala unatoa amri zake kinyume cha sheria hali ambayo hukaribisha upinzani kutoka kwa wananchi.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wa kada mbalimbali kwamba nchi yetu imeanza kubobea kidogo kidogo kwenye sheria za utawala.

Wataalamu wa mambo ya sheria na katiba wanasema kukosekana kwa utawala wa sheria na kutamalaki sheria za utawala, ni hali inayoweza kujitokeza katika nchi zote, zile za kidemokrasia na hata zile za kidikteta.

Ndiyo maana wakaja na msamiati “dictatorial democracy” yaani demokrasia ya kidikteta au ya kiimla kwa lugha nyepesi. Kinachoendelea katika nchi yetu hii ya kidemokrasia ni sheria ya utawala badala ya utawala wa sheria.
Bak nachotaka nikukumbushe ni kuwa katiba na yaliyomo si chochote ama lolote mpaka wale inaowaongoza waikubali na kile kilichomo. Sasa jiulize vizuri kama kweli ulishawahi kuisoma vyema Katiba yetu, ni Rais gani ameitendea haki Katiba hiyo kama Sheria mama?
Nani Afrika ameitetea na kuilinda Katiba kwa namna tunavyoielewa?
Ni vyema uelewe kuwa, Katiba yetu kama zilivyo zote za dunia ya tatu, Katiba ni document iliyojaza masuala yanayotoa haki kwa mtu (individual) kwa mtizamo wa kiliberal lakini hapo hapo nchi nyingi za kiafrika zimekuwa zikiingiza vipande vinavyotoa haki kwa jamii (community).
Hapo ndipo Katiba zetu huwa zinaiua haki ya an individual na kutoa kwa wengi (community).
Na tusisahau kuwa, kiasili sisi waafrika haki na wajibu viko kwenye jamii na siyo mtu mmojammoja ndiyo maana ilikuwa rahisi kuingiza elements nyingi za kijamaa katika mifumo ya kiutawala baada ya nchi zetu kupata uhuru. La ajabu ni kuwa mpaka muda huu we are a socialist state (though mostly in theory).
 
Yanaenda vzr kwa mtizamo wako,Kwan Shroeder alizuia vyama vya siasa kuendesha shugli zao kama jpm anavofanya?
Nimetolea mfano wa Gerhard Schroeder kujibu hoja ya member. Jaribu kurefer majibu kwanza la sivyo utanitafasiri vibaya. Mimi nilijenga hija ya kuhamisha Makao Makuu ya nchi na kuonyesha jinsi Chancellor huyo alivyoharakisha suala hilo huko kwao Ujerumani.
Endapo Viongozi wa Vyama vya Upinzani wakiwa wanamkosoa Rais Magufuli kwa kila analofanya hiyo ni sawa kabisa kwa sababu pasipo kutafuta madhaifu yake hawataweza kutatawala. Hata hivyo inaumiza kukuta mwananchi wa kawaida anamshikia bango Rais kwa kila kosa linaloenezwa na Viongozi wa Upinzani lakini ukimuuliza ayataje mazuri ambayo Magufuli ameyafanya hawezi kukutajia kwa sababu hajui chanzo cha matatizo yaliyopo nchini.
Magufuli anayoyafanya ni tiba ya matatizo yetu mengi tuliyorithi kutoka kwa huyo mnayemuona mzuri kwa sasa. Leo wanachuo wanarudishwa nyumbani tunalalamika, watumishi hewa tunalalamika, wabadhirifu wanatumbuliwa tunalalamika, vyuo vinafungiwa tunalalamika - lakini sisi ndio wa kwanza kulaumu maadili yameshuka ama walimu hawana uwezo kufundisha mashuleni.
Ndiyo maana kuna msemo muhimu sana katika Social Sciences ''An Organization normally reflects the society's behaviour'' - kwamba ukiona watu wanamkosoa kwa namna inayoonekana sasa, nk wazi kuwa tatizo siyo Magufuli ama watawala waliowahi kuitawala nchi hii bali ni sisi wananchi ambao ni mburura na hatuifahamu hii organization (nchi) yetu. Kwenye ofisi ukijikuta ni wewe pekee hautaki rushwa kati ya watumishi 10 basi tatizo ni wewe na siyo hao wala rushwa. Ndiyo maana tunawaabudu wezi wakubwa wa rasilimali zetu kwa sababu rushwa ni sisi na pia ni sehemu ya sisi na maisha yetu. Poor me with ma bloved country...!!!
 
Tatizo kubwa lipo ktk kuongoza kwa kufuata katiba. Nadhani akifuata utaratibu huo sidhani kama wapinzani watakuwa na cha kuongea. Mtego ndio upo hapo tena upo wazi kabisa.
 
Pamoja na viraka chungu nzima katiba yetu inabidi iheshimiwe na wote ikiwemo Rais wa nchi ambaye hayuko juu ya katiba.

Huna cha kunikumbusha chochote kile. Kikwete na Mkapa hawakuwadhibiti wapinzani ndani ya Bunge na nje ya Bunge na kupiga marufuku siasa kwa miaka mitano.

Anachokifanya huyu DU si sawa hata kidogo na inabidi kipigwe vita na wapenda amani wote nchini. Anaidharau katiba ya nchi halafu hapo hapo anajibaraguza kuhubiri utulivu nchini. Huwezi kukibubali kimoja halafu ukidharau kingine. Utulivu unaletwa na kuheshimu haki za vyama vya wapinzani bila kuingiliwa na yeyote yule. Vinginevyo ni mwanzo wa kuleta machafuko nchini.

Bak nachotaka nikukumbushe ni kuwa katiba na yaliyomo si chochote ama lolote mpaka wale inaowaongoza waikubali na kile kilichomo. Sasa jiulize vizuri kama kweli ulishawahi kuisoma vyema Katiba yetu, ni Rais gani ameitendea haki Katiba hiyo kama Sheria mama?
Nani Afrika ameitetea na kuilinda Katiba kwa namna tunavyoielewa?
Ni vyema uelewe kuwa, Katiba yetu kama zilivyo zote za dunia ya tatu, Katiba ni document iliyojaza masuala yanayotoa haki kwa mtu (individual) kwa mtizamo wa kiliberal lakini hapo hapo nchi nyingi za kiafrika zimekuwa zikiingiza vipande vinavyotoa haki kwa jamii (community).
Hapo ndipo Katiba zetu huwa zinaiua haki ya an individual na kutoa kwa wengi (community).
Na tusisahau kuwa, kiasili sisi waafrika haki na wajibu viko kwenye jamii na siyo mtu mmojammoja ndiyo maana ilikuwa rahisi kuingiza elements nyingi za kijamaa katika mifumo ya kiutawala baada ya nchi zetu kupata uhuru. La ajabu ni kuwa mpaka muda huu we are a socialist state (though mostly in theory).
 
Pamoja na viraka chungu nzima katiba yetu inabidi iheshimiwe na wote ikiwemo Rais wa nchi ambaye hayuko juu ya katiba.

Huna cha kunikumbusha chochote kile. Kikwete na Mkapa hawakuwadhibiti wapinzani ndani ya Bunge na nje ya Bunge na kupiga marufuku siasa kwa miaka mitano.

Anachokifanya huyu DU si sawa hata kidogo na inabidi kipigwe vita na wapenda amani wote nchini. Anaidharau katiba ya nchi halafu hapo hapo anajibaraguza kuhubiri utulivu nchini. Huwezi kukibubali kimoja halafu ukidharau kingine. Utulivu unaletwa na kuheshimu haki za vyama vya wapinzani bila kuingiliwa na yeyote yule. Vinginevyo ni mwanzo wa kuleta machafuko nchini.
Naungana na ww kabisa ndio maana post yangu ya nyuma nilieleza umuhimu wa Rais kuviruhusu Vyama vyote kuwa huru kuendesha shughuli zao za kisiasa kwa sababi ndio msingi mkuu wa kila Chama kwamba kinapigania kuchukua madaraka. Na nilisisitiza kuwa mi ni muumini mzuri ''plurality'' badala ya Chama kimoja kudominate.
Hata hivyo approach ya watu wengi kwa Rais ni kama ameua mtu kwa jinsi wanavyomuandama.
Hivi ni kweli tuko serious kwamba pamoja na kukataza mikutano ya kisiasa Magufuli ni mbaya kulinganisha na wale watangulizi uliowataja?
Sasa wote tukiwa na mtazamo huo kuna haja tena ya kujiuliza kwa nini sisi ndio masikini sana kuzidi nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki licha ya kujidai tuna rasilimali kibao?
 
Unataka tusubiri mpaka mtu afe ndiyo tupinge katiba ya nchi kutoheshimiwa!? kwanini tusianze kupinga mapema ili kuepusha umwagaji wa damu na hivyo kuhakikisha hakuna Mtanzania atakayepoteza maisha nchini kwa huu udikteta uchwara!?

Magufuli fisadi, Magufuli muongo na pia haiheshimu katiba ya nchi yote haya huyaoni!?

Hao waliomtangulia angalau hawakuvizuia vyama vya upinzani kutofanya siasa kwa miaka 5/10 na hivyo kuviwezesha kupata wanachama wapya wengi na kukusanya michango mbali mbali toka kwa wanachama wao.

Naungana na ww kabisa ndio maana post yangu ya nyuma nilieleza umuhimu wa Rais kuviruhusu Vyama vyote kuwa huru kuendesha shughuli zao za kisiasa kwa sababi ndio msingi mkuu wa kila Chama kwamba kinapigania kuchukua madaraka. Na nilisisitiza kuwa mi ni muumini mzuri ''plurality'' badala ya Chama kimoja kudominate.
Hata hivyo approach ya watu wengi kwa Rais ni kama ameua mtu kwa jinsi wanavyomuandama.
Hivi ni kweli tuko serious kwamba pamoja na kukataza mikutano ya kisiasa Magufuli ni mbaya kulinganisha na wale watangulizi uliowataja?
Sasa wote tukiwa na mtazamo huo kuna haja tena ya kujiuliza kwa nini sisi ndio masikini sana kuzidi nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki licha ya kujidai tuna rasilimali kibao?
 
Wakati wa mchakato wa kutengeneza katiba mpya, tuliona jinsi utawala wa Kikwete ulivyokatisha ndoto kubwa ya watanzania wengi wenye uelewa kupata Katiba ya Warioba iliyokuwa na maudhui mengi yaliyokuwa yakipendelewa sana na ''ma-elites'' nchi nzima. Hata hivyo, wengi walifurahia sana baada ya mchakato wa kuipigia kura katiba hiyo pendekezwa uliposhindikana.

Hata hivyo ukichunguza kwa makini kampeni za vyama vya upinzani katika kipindi kile cha kuhamasisha umma cha 2014, utagundua kuwa masuala mengi ambayo vyama vya upinzani hasa CHADEMA, vilivyokuwa vikiyapigania, yameanza kushughulikiwa na Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambayo si mimi, wala mwana-CCM ama mpinzani aliyetarajia huyu jamaa angeyafanya yote hayo na ndani ya kipindi kifupi sana.
Kwa ajili ya kupanua mjadala, tushirikiane tuyajadili vyema ili tumhukumu kwa haki Rais huyu.

Hivi tunaifahamu vyema nchi yetu, je ni haki tumhukumu Rais wetu kwa sababu hataki bunge liwe live, au kwa sababu sukari imepanda bei? Uwezo wetu wa kufikiri ndio umeishia hapo ama?

Nikiri wazi mi ni mpenzi mkubwa sana wa plurality katika siasa ambapo hakuna Chama kinacho-dominate vyama vingine. Mwenye uelewa mzuri wa Comparative Politics atakiri kuwa, kati ya CCM na CHADEMA/UKAWA, anayepaswa kushangilia kwa anayoyafanya Rais Magufuli ni CHADEMA/UKAWA kwa sababu anawasomesha namba vibaya sana wana-CCM, huku akitekeleza yale ambayo wapinzani waliyataka.

Nani atasumbuka kuangalia bunge live wakati Rais anaonekana moja kwa moja akitekeleza watu wanayoyataka na hivyo kupelekea bunge kupitisha kila kitu.
Jamani wapinzani nyie ndio mlio win kuliko wana-CCM, fikirieni mara mbili mbili.
Screenshot_2016-08-05-20-05-27.png
Screenshot_2016-07-31-12-09-55.png
Screenshot_2016-07-30-17-53-50.png
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nashukuru sana kwa kujaribu kuelezea kiufafanuzi japokua haya masuala ya udikteta kila mtu anayelewa yanamaanisha nini. La muhimu ni kuwa kuongozi kuwa wa kidikteta siyo tatizo isipokuwa kunakuwepo tatizo tu unapolinganisha na aina nyingine ya kiutawala mfano wa kidemokrasia. Suala la kujiuliza ni nchi gani ya kiafrika ambayo ni ya kidemokrasia? Wengi wangeifikiria SA lakini fikiria jinsi jeshi lao lilivyoua mamia ya wachimbaji madini ya dhahabu waliokuwa wakiandamana mitaani kupinga serikali.
Wananchi wenye uelewa wanapenda siasa za ushindani hivyo wangefurahi kuona vyama vya siasa vikiwa huru kufanya siasa. Hata hivyo, ni wazi kuwa wengi kwa sasa hawavutiwi na siasa kihivyo baada ya Vyama vya Upinzani kufanya vibaya tofauti na matarajio ya wengi kuwa vingeweza kuchukua hata nusu ya majimbo ama kiti cha urais. Sasa pamoja na kuwekeza nguvu nyingi 2015, mbona watu hawakuvikubali, havioni kuwa somewhere (vijijini) something (elimu ya uraia) was missing na kwamba ikifaa sasa waweke nguvu kutengeneza mtandao mpana wa wapiga kura na siyo washabiki pekee?
Kitu cha aibu ni kuwa hata maandamano ambayo huwa yanapangwa yanaishia majiji makubwa ama mikoani huku wilayani kukiwa zii. Wenzenu CCM hawana kabisa mvuto kwa watu wenye uelewa wengi lakini wanajua kuwahimiza wafuasi wao kwenda kupiga kura hasa wakitumia mabalozi wao. Jengeni ofisi wilayani bhana watu walete shida zao na hivyo kuwafahamu. Vyama hivi vya upinzani visipohangaika kujenga miundombinu ni rahisi sana kusambaratika. Wenye ufahamu hawapendi kusikia CHADEMA ikisambaratika kama NCCR MAGEUZI, Chama kikali chini ya Mrema kilichoitetemesha sana CCM mwaka 1995 kabla ya jusambaratika na kupelekea juibuka kidogo kwa TLP 1999 ambacho kikifeli kabisa na kukiachia Chama cha CUF usukani wa Chama kikuu cha upinzani nchini 2000 - 2010.
 
Umeandika Maelezo marefu ila sijaelewa point yako!Hapa sijazungumzia fulani kachukua nchi au fulani hajachukua nchi!Kila chama kitajua namna ya kujijenga chenyewe kwa namna yake,mimi hilo halinihusu!Hoja yangu ni kuwe na uwanja sawa wa demokrasia baina ya vyama vya siasa!Viwe dhaifu au viwe na nguvu,wapewe haki!Hayo cjui Mrema,sijui CUF kushindwa kuchukua nchi sio concern yangu na wala sijajenga hoja inayohusu hayo so ni off topic kabisa!
 
Back
Top Bottom