Mkuu Mwanasheria nguli mbobezi Petiro, kuona hoja ni ipi pia kunahitaji kiwango fulani cha level ya uelewa kuweza kuona hoja ya uzi huu ni ipi, ukiwa uko below level ya uelewa huo, hutaona hoja ni ipi!.
Tuhuma zimetolewa kuhusu uongo na uzushi mitandaoni na japo haikusemwa ila mlengwa pia ni jf.
Hoja ni kila zikitolewa shutuma za uongo au uzushi, dawa ni kwa shutuma hizo zijibiwe kwa ukweli na facts.
Nikatolea mfano uzushi wa udikiteta na uvunjaji wa katiba, ulipoibuliwa na Chadema na katika UKUTA, nikasema kama katiba imetoa hakiya kuandamana na kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa popote then rais akapiga marufuku mikutano hiyo mpaka 2020, ili kuufuta uzushi wa udikiteta, msemaji wa serikali alipaswa kusema tuu ukweli kuwa rais sio dikiteta bali amepiga marufuku mikutano ya kisiasa hadi 2020 kwa mamlaka gani chini ya kifungu gani au sheria gani inayompa mamlaka rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa amri inayopingana na katiba, then hoja ya udikiteta na uvunjifu wa katiba inakufa natural death.
Uzushi na uongo unakanushwaje? , unakanushwa kwa kusema ukweli, na sio kuacha tuu kwa vile ni uongo na uzushi, hivyo unaamua kuupuuza tuu huo uongo huku uongo huo ukiendelea kusemwa na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hivyo hugeuka kuwa ni ukweli na sasa uongo huo umeingizwa hadi UN!.
Ufafanuzi huu ni wa level ya sekondari ila
kama bado hujaelewa naweza kukufafanulia kwa low level zaidi ya watoto wa primary.
Pasco.