Udhibiti Wa Sumukuvu unahitaji wadau kushirikiana

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1592932991109.png

WADAU wa usalama wa chakula nchini wametakiwa kuisaidia serikali kutekeleza mradi mkubwa wa miaka mitano wenye lengo la kudhibiti tatizo la sumu kuvu ili ili kuboresha afya ya jamii kwa kuhakikisha taifa linazalisha na kuuza chakula salama na chenye kiwango cha ubora unaotakiwa kitaifa na kimataifa. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati akifungua kikao cha pili cha kamati ya kusimamia mradi wa kudhibiti sumukuvu nchini (TANIPAC) kilichofanyika leo mkoani Morogoro. Kikao hicho kinashirikisha pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali zinazotekeleza mradi pia wamo Makatibu Wakuu wanne kutoka wizara za Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Katibu Mkuu huyo alisema usalama wa chakula hapa nchini unategemea Kilimo kwa kiasi kikubwa, na kuongeza:” sote tunafahamu hakuna Taifa linalokuwa salama bila usalama wa chakula. Kwa kuzingatia umuhimu huo, tunalo jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba tunaendelea kukipa Kilimo uzito unaostahili kwa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza wakati wowote.”

Sekta ya Kilimo ndiyo inayoajiri zaidi ya asilimia 65 ya nguvu kazi na inachangia asilimia 30 ya pato la Taifa (GDP), huku ikichangia takriban asilimia 65 ya malighafi za viwandani na takribani asilimia 100 ya chakula kinachotumika ndani ya nchi.

“ Napenda kumshukuru Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dk.John Pombe Joseph Magufuli, kwa uongozi wake mahiri katika kipindi hiki cha miaka mitano ambapo nchi imeendelea kuwa na utoshelevu wa chakula.” Alisema Katibu Mkuu Kusaya na kuongeza kuwa sasa ni wajibu wa wadau mbalimbali kuhakikisha chakula hicho ni salama. Alisema watanzania wanapozungumza usalama wa chakula wanagusa sekta ya Kilimo ambao ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na jamii. Alisema mojawapo ya changamoto hizo ni sumukuvu tatizo ambalo limekuwa likijirudia nchini Tanzania na hivyo kuifanyha serikali kuungana na wadau wengine kudhibiti hali hiyo.
 
Back
Top Bottom