Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,999
Mwanakijiji! mzee wetu Mohamed Said ameianza nakala yake kwa kuturudisha nyuma kidogo na habari ya yule Sheikh aliyerudishwa "kwao" Zanzibar halafu akaendelea kutupeleka mwaka 1964 wakati masheikh wengi waliwekwa kizuizini, hakutuacha hapo bali alitukumbusha mwaka 1993 ambapo kulizuka tafrani kati ya askari na Waislamu akamalizia tukio la Sheikh Kishki juzijuzi na Mufti wa Yemen halafu akaunganisha na lilomkuta yeye.
Huu ni mlolongo wa matukio baada ya matukio haiwezekani ulifananishe na tukio moja la Ulimboka au na jingine kama la Ulimboka pale na hapa......mwisho kauli yako imenishangaza sana kwani inaonekana kuihukumu Serikali kuwa na hatia ya utekwaji wa Ulimboka!
Mohamed said ametuletea udhalilishwaji wa Waislamu unaofanywa na vyombo vya dola, wakati ya Ulimboka ndio kwanza uchunguzi unaendelea!
Ndugu mbona wewe mtata sana? Hulengi chochote zaidi yakupandikiza udini!
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Je, unataka tum cross-examine shahidi wako ambaye ni historia ya darasa la tano?Hili nalo linahitaji uthibitisho? Ina maana wewe historia ya darasa la tano hukusoma? Mbona liko wazi kwamba walioendesha biashara ya utumwa Tanganyika ni waarabu, na kama ni waarabu, definitely ni Waislamu, sasa unataka ushahidi gani tena?
TudokoleeHili la Utumwa zuri sana lakini kwanza itabidi tuanze na Transatlantic Slave Trade. Una ubavu tuanze kazi? Unajua kulikuwa na meli inayobeba watumwa kupeleka Marekani ikiitwa Jesus?
Pole sana Mohamed Said kama umejikuta matatani kutokana na utendaji mbovu wa vyombo vyetu vya usalama. Lakini inaonyesha vyombo vya usalama vimekua vinakufuatilia nyendo zako. Na inawezekana hata mwaliko wa Ibadan ilikua ni ktk kukuchunguza mambo yako ya udini! Inaonyesha ulimwaga nyongo ktk vikao rasmi na visivyo rasimi ukidhani wale jamaa ni wenzako!!! Mwisho ni kwanini umeleta hii stori ktk kipindi wafadhili wako Iran wakituhumiwa kupeperusha bendera yetu kukwepa vikwazo vya Marekani na EU?!
Wakijiji sasa unazeeka vibaya! husikii siku zote kuwa ni MFUMO na wale wa Waislamu wapo pale kuutekeleza watake wasitake?Vyombo vya dola mwaka 2006 kama ilivyo leo vinaongozwa na Waislamu. Kwanini wasiseme ni waislamu serikalini wanawadhalilisha Waislamu wenzao? Mwaka 1964 waliowekwa kizuizini hawakuwa waislamu peke yao.
Wakijiji sasa unazeeka vibaya! husikii siku zote kuwa ni MFUMO na wale wa Waislamu wapo pale kuutekeleza watake wasitake?
Men lie, women lie numbers don't lie
Wee jamaa unaonekana ni mtu mzima na msomi lakini hoja zako ni za kitoto ile mbaya! Hivi wakati wa kipindi cha Nyerere ni watu wangapi waliokuwa detained kutokana na sababu mbalimbali? Au walioondoshwa na kurudishwa kwao; wazungu kwa waafrica? Tukianza kuwa na akili na mawazo mgando kama haya, basi hata wakinga watakuja na kichwa cha habari kinachosema udhalilishaji dhidi ya wakinga kwa kuwa tu Tuntemeke Sanga alinyanyaswa na Nyerere. Au wale watu wa Ukerewe watakuja na hoja kama hizo hizo kwa kuwa wengi wa walioko kule walipelekwa kama adhabu. Ni ufinyu wa fikra, kutolea mfano wa shehe aliyerudishwa Zanzibar kama mfano wa unyanyasaji dhidi ya uislamu.
Ninapata shida sana kukuelewa wewe binafsi na pia uwezo wako wa kuchambua mambo. Ni watu wangapi wamekatwa, achilia mbali uwanja wa ndege na kusingiziwa hizo kesi za madawa ya kulevya na hata mauaji? Ni kwa vipi kukamatwa kwako ukuhusishe na Uislamu? Nyie waislamu kama mtaendelea kuwa na akili finyu hivi hivi, mtaipeleka nchi vitani hii. Yaani wasomi wa elimu dunia kama wewe ambaye tulidhani muwe mmestaarabika, na nyie mnaendekeza ujinga uleule wa mafundisho ya madrasa. Kama na wakristo wangekuja na mafundisho ya kanisani na kutaka yaongoze nchi mnadhani kungekalika? Acheni fikra mbovu na finyu ya kuwazia udini kila wakati!
Mkuu, waarabu na wazungu wote walitumia dini kutufanya watumwa,so kama na wewe ni mwafrika utakuwa umenielewa.Hili la Utumwa zuri sana lakini kwanza itabidi tuanze na Transatlantic Slave Trade. Una ubavu tuanze kazi? Unajua kulikuwa na meli inayobeba watumwa kupeleka Marekani ikiitwa Jesus?
Tudokolee
Mzee M. Said:
a. Wale waliokukamata uwanja wa ndege walihoji nini kuhusu Uislamu wake na harakati zako kama mtetezi wa haki za Waislamu?
b. Wale waliokukamata katika kukuhoji walihoji jambo lolote ulilolesema kwenye ule mkutano wa Iran?
c. Kuna yeyote aliyetoea kauli ya aina yoyote kuhusu shughulii zako kama Muislamu na alisema nini ambacho kilikukwaza?
Hawakuwa watu wenye uwezo wa kunihoji.
Kilichokuwa kinatafutwa na kuwaridhisha Waamerika kuwaeleza kuwa "tunashughulika."