Udhalilishaji huu utaendelea mpaka lini?

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,987
1,209
Hodi katika jamvi ni matumaini yangu ku mmeamka salama jana usiku katika wilaya Makete Mkoa wa Njombe. Askari walikuwa wakipita katika nyumba za kulala wageni na kukamata wageni waliokuwa wamelala katika nyumba hizo.

Sababu iliyotolewa ni kuwa hawakujiandikisha kwenye daftari la wageni na hivyo kulazimika watu wengi walikamatwa na kulazimika kulala ndani hata kama walikuwa na vielelezo.

Ndugu zangu kwa kweli mambo haya ni udhalilishaji mkubwa na kusababisha chuki kati jeshi la na wananchi. Sipingi kufanya ukaguzi katika nyumba za kulala wageni lakini ni muhimu haki za binadamu zikazingatiwa

Naomba vyombo husika vikaliangalia jambo hili kwa jicho la busara na ubinadamu kwa mjibu wa wakazi wa Makete zoezi hili la kamata kamata limekuwa likifanyika mara kwa mara.
 
Mkuu pole sana? Vipi ndo wamekuachia sasahivi nini?
Na baridi ya njombe sipati picha usiku wakuchomoe room na mchepuko alafu ukalazwe selo.

Hao policcc labda walikua wameutwika ulanzi.
 
Wapuuzi Sana!
Na hakuna kulala wawili jinsia moja mnakamatwa yaani nimlaze mdogo wangu chumba kingine wakimbaka je?
Hilo liko mikoa mingi tu
Huu utaratibu sijui wameuokota wapi hawa watu
Ni haki kuamsha watu saa 8 usiku kuwakagua kweli??
 
Mkuu pole sana? Vipi ndo wamekuachia sasahivi nini?
Na baridi ya njombe sipati picha usiku wakuchomoe room na mchepuko alafu ukalazwe selo.

Hao policcc labda walikua wameutwika ulanzi.
Hapana mkuu kuna kijana wetu alikuwa huko na mpaka sasa bado hawajamuachia
 
pole sana , Lakini kwa nini usijiandikishe kwenye daftari la wageni?

1. jeukipatwa na stroke ukafia humo utajulikanaje?
2. je ukivamiwa na kuibiwa utalipwaje ? no records
3. hata mchana tu maofisini mbona tunajiandikisha na kuvalishwa badge?
Hapo sasa wapenda chepukos ndio manumia poleni sana
 
Sina mda Wa kumshangaa mkuu Wa mkoa ninakawaida ya kumshangaa aliyemteua na ujinga huo hakuna kauli
Mkuu inasikitisha sana hii ndiyo hupelekea wananchi kuwa na chuki na jeshi lao kutokana na baadhi ya viongozi kuwa na tamaa ya maslahi binafu
 
Wapuuzi Sana!
Na hakuna kulala wawili jinsia moja mnakamatwa yaani nimlaze mdogo wangu chumba kingine wakimbaka je?
Hilo liko mikoa mingi tu
Huu utaratibu sijui wameuokota wapi hawa watu
Ni haki kuamsha watu saa 8 usiku kuwakagua kweli??
Kwa kweli mkuu inasikitisha sana
 
Sheria ndio inasema ni lazima ujiandikishe kwenye daftari la wageni. Next time usivunje sheria
Mkuu kujiandikisha ni kila siku au mara moja?kwa maana kwamba ukikaa siku tatu unatakiwa kila siku ijiaandikishe na ni sheria ipi inayozungumzia kujisajili katika daftari la wageni
 
Unajua watanzania tumekuwa na ujinga kiwango kikubwa san
Mkuu inasikitisha maana afisa anayekabidhiwa dhamana ya kulinda raia ndiye anageuka na kuwa mkandamizaji na mdhalilishaji wa wanachi anaotakiwa kuwalinda
 
Wapuuzi Sana!
Na hakuna kulala wawili jinsia moja mnakamatwa yaani nimlaze mdogo wangu chumba kingine wakimbaka je?
Hilo liko mikoa mingi tu
Huu utaratibu sijui wameuokota wapi hawa watu
Ni haki kuamsha watu saa 8 usiku kuwakagua kweli??
Huo utaratibu niliuona Tanga. Wanawake wanaruhusiwa ila wanaume hawaruhusiwi.
 
Huo utaratibu niliuona Tanga. Wanawake wanaruhusiwa ila wanaume hawaruhusiwi.
Kuna vyumba vina twin bed maalum kulala watu wawili jinsia moja chumba kimoja. Tatizo kuna watu wanafanyakazi kama robot
 
Wapuuzi Sana!
Na hakuna kulala wawili jinsia moja mnakamatwa yaani nimlaze mdogo wangu chumba kingine wakimbaka je?
Hilo liko mikoa mingi tu
Huu utaratibu sijui wameuokota wapi hawa watu
Ni haki kuamsha watu saa 8 usiku kuwakagua kweli??
Kwa wanawake ni rahis kuliko wanaume kulala chumba kimoja..
 
Duh nawe mpka leo unaingia gest house bila kujiandikisha mkuu,,aseeh usijaribu maana kuna matatizo yanaweza kukutokea ukashindwa kujitetea.. Faida za kujiandikisha ni nyingi kuliko kutojiandikisha,,ila umejifunza sasa
 
Huo utaratibu niliuona Tanga. Wanawake wanaruhusiwa ila wanaume hawaruhusiwi.

Ohooooo... Iringa, dodoma mwanza yalinikuta haya mambo kila chumba mtu mmoja labda muwe jinsia mbili
 
Back
Top Bottom