Napendaga kujua je ni mimi tu mwenye tabia hii au kuna wenzangu tunaofanana? Au km ndo hatufanani madhaifu yetu bas je wengine wana madhaifu yapi?
Ok,ngoja tuone ...
Me binafsi huwa najikuta hodari kweli wakumsema tu!
Kimsingi hili ni tatizo na unatakiwa ulitafutie ufumbuzi,tabia hii sio nzuri kwa afya ya mahusiano imara,hii tabia inaletwa na ubinafsi,unajiona wewe ndio uko sahihi tu bila kujua kuwa wewe nawe ni binadamu
Anza kujiona wewe ni binadamu kama mwenzako na anza kuona nawe kuna mahali unakosea,wengi wenye tabia hizi ni wale ambao wana tatizo la kuyaona matatizo kwa wenzao hasa yale ambayo wao wanakuwa wanayafanya,kwasababu hii unaweza kumfanya mwenzako kioo cha kujitazama wewe na tabia zako kwani yale ambayo unachukia mwenzako kuyafanya ndio yale ambayo wewe unayafanya
Pia ni rahisi sana kununanuna ovyo!
Kununa ni tabia ya kike lakini ikizidi inakuwa tatizo,mara nyingi hili husababishwa na wivu na msongo wa mawazo,jaribu kujikagua uone kama una matatizo hayo ili ujaribu kuyaondoa ili uhusiano wako uwe imara na wenye afya
Halafu sipend unirekebishe kitu! Nataka nifanye vile nnavyopenda!
Inaonekana pia una tatizo la kutojiamini,na una kiwango kikubwa sana cha umimi,anza kuwaona wenzako kama binadamu wenzako na acha kujiona wewe ni malaika
Viongozi wengi ambao walikuwa ni madikteta walikuwa na tabia kama hii ....
Tena nnapokosea kufanya jambo huwa najua kn nmekosoea so ctak tena mtu anirekebishe huwa nanuna kweli! Hiz tabia huwa kujicontrol cwez!
Unaweza labda tu hutaki au hujui namna ya kuondoka kwenye tabia hizo,namna ya kuondoka nimekueleza kwa baadhi ya njia hapo juu .....
Japo namshukuru Mungu cnaga tamaa, ni mwaminifu hata unipepesa nying nikuhifadhie bas hata niwe na shida cwez chomoa hata senti! Tamaa ya pesa sina kabisaa hata uniekee pipa la pesa ukitegemea unitege bas me hunipati! Na mengineyo! nipen njia niweze kujirekebisha madhaifu yangu na tuambie wewe yako ni yapi?
Hili ni jema kwako,hongera .....!