Udhaifu wa Spika

Udhaifu wa Spika

sina-ajira

Senior Member
Joined
May 1, 2013
Posts
136
Reaction score
38
Kwa mtazamo wangu naona kiti cha Spika kimeyumba sana katika suala zima la utoaji maamuzi ndani ya Bunge.Ni dhahiri Spika Makinda anasukumwa zaidi na hisia katika maamuzi yake,Hasa hisia za mapenzi dhahiri kwa Chama chake na kujisahau kabisa kwamba kazi yake ya msingi ni kutenda haki kwa Wabunge wote bila kujali Vyama wanavyotoka.Spika amekuwa akiiuwa mijadala mingi Bungeni ambayo ilikuwa mwiba mkali kwa Serikali hasa zile hoja zilizoletwa na Wapinzani lakini iliyokuwa na manufaa kwa Taifa.Alifanya hivyo ili tu kuwafurahisha Mabwana wakubwa wa Chama chake Tawala huku akijua fika kuwa Maamuzi yake hayo ni kama yanahalalisha uzembe na matendo mengine yasiyo ya kimaadili miongoni mwa Watendaji wa Serikali.Zaidi maamuzi yamelenga kulifanya Bunge liwe kama Rubber Stamp kwaajili ya kupitisha Miswada mbali mbali inayowasilishwa na Serikali hata kama imejaa dosari nyingi.Bunge chini ya Makinda limeshindwa kabisa kuisimamia na kuiwajibisha Serikali badala yake limejigeuza kuwa ngao ya Serikali dhidi ya Wakosoaji wake.
 
Back
Top Bottom