Udhaifu wa Chadema sio Uimara wa CCM!

Udhaifu wa Chadema sio Uimara wa CCM!

TWisheshagi

Member
Joined
May 2, 2020
Posts
14
Reaction score
209
Nimeona mjadala mkali na wa kuvutia ukiendelea kuhusu uhai wa vyama vya upinzani hususan Chadema kuelekea 2020.

Nikiri mapema kuwa, hatuna vyama vya siasa Bali tuna vikundi vinavyopambana na dola. Hata CCM yenyewe ilikwisha acha siku nyingi kuwa Chama cha siasa badala yake uhai wake unategemea uwepo wa dola.
CCM hakifanyi tena kazi ya siasa ndani ya umma na badala yake kinafanya kazi ya dola ndani ya umma.

Zipo tetesi kuwa, dola ipo kazini, na kazi kubwa ni kusimika utawala mpya wa NCCR MAGEUZI, kama mbadala wa Chadema kuelekea 2020.

Nimeshindwa kuzipuuza "tetesi" hizo kwa sababu mbili kubwa: Mosi, tetesi hizi zimeanza kusemwa na viongozi wakubwa wa CCM. Pili, tetesi hizi zinaeleza tabia halisi ya James Mbatia kuhusu mageuzi. Huyu haaminiki na ni vigumu kumpa dhamana ya kutetea maslahi ya mageuzi nchini.

Lakini lipo jambo linalotia fora. Ushiriki wa CCM kuihujumu Chadema. Juhudi hizi zinaongozwa na CCM. Nimeongea na baadhi ya viongozi wa Chama chetu waliobaki walau na chembechembe za uzalendo na hofu ya MUNGU, jambo hili linawakera Sana.

Kwanza ni "Upuuzi" kudhani kuwa, Udhaifu wa Chadema(kama upo kweli) ni uimara wa CCM. Ni ujinga zaidi kudhani kuwa, kuiua Chadema bila juhudi za kuimarisha CCM.

Unaweza kweli kuua upinzani kwa kutumia ubabe. Maana hata siku hizi ubabe umegeuzwa kuwa ujasiri! Lakini ukashindwa kuuwa hisia za upinzani na mageuzi.

Mwaka1965, Watawala wa kipindi hicho, waliunga mkono kuondoshwa kwa vyama vingi nchini. Walichofanikiwa pekee ni kufuta majina ya vyama kwenye makabrasha ya serikali, lakini walishindwa kuua mageuzi na fikra zake.

Hata mwasisi wa Chama chetu Kuna nyakati alituasa kwamba huwezi kuifagia shilingi, tena akasema, hoja hazipigwi rungu.

Pamoja na ukweli kuwa Mwalimu Nyerere, aliongoza zama za kiza za Chama kimoja, lakini alihakikisha kuwa anazungukwa na watu makini na wenye ueledi na ujasiri wa kumpinga hata hoja zake.

Mwalimu alizungukwa na watu kama vile: George Opiyo, Emilio Mzena, Rashid Kawawa, Kingunge Ngombale Mwiru, Mzee Mwakawago nk. Hawa walikuwa kama vyama vya upinzani kwa utawala wa Mwalimu Nyerere. Walimpinga kwa hoja, na wakati mwingine ililazimu Mwalimu kubadili mawazo yake, pamoja na ukweli kuwa aliongoza taifa kwa nguvu ya maono na si kwa nguvu za miti shamba!

Bunge la Chama kimoja lilikuwa bunge lenye hoja kuliko hili linalopangiwa namna ya ulipaji posho na mhimili mwingine.

Chama chetu kiliongozwa na falsafa ya kuchukia makosa na kupenda wakosoaji. Na NGUVU ya Chama ilikuwa kubwa dhidi ya serikali.

Leo Chama chetu kinaogopa wakosoaji. Kimejificha kwenye koti la dola. Hatufanyi siasa, tunafanyiwa na dola. Tunaongoza harakati za hila za kufuta Chadema pasipo kuimarisha Chama chetu! Kwa leo nikomee hapa, bado ni mgeni kwenye jukwaa hii la tafakuri!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom