Juzi tarehe 30/10/2017 usiku route ya Kivukoni -Kimara hali ilikuwa mbaya sana.
Kulikuwa na mabasi machache, nayo pia yalikuwa yana tumia muda mrefu kugeuza yakifika Kivukoni, yakirudi yamejaza kiasi cha kuhatarisha kuvunjwa mlango.
Tatizo la kukosa huduma ya kuongeza salio ktk kadi limekuwa sugu hasa vituo vya Kibo, Ubungo Maji lango la kutokea Kimara, Posta ya Zamani lango la kutokea Azania Waterfront, na vituo vingine vingi hasa vya katikati.
Watu tunabanana mno, rahisi kuambukizana Herpetitis, TB, Uti wa mgongo na magonjwa mengine ya ngozi. Na joto la sasa watu mnapakazana jasho ambalo ni hatari tupu kwa afya.