Udambwidambwi wa Urusi unaujua?

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,552
UNAJUA UDAMBWIDAMBWI WA URUSI WORLD CUP 2018?

Si Cristiano Ronaldo aliyeanza kwa mkwara na chama lake la Ureno, kwa kuipiga hat trick Hispania, mwisho ngoma ikawa sare 3-3. Ronaldo aliishia 16 Bora tu.

Si Lionel Messi aliyefurushwa na Argentina yake baada ya kuchapwa na Ufaransa hatua ya 16 Bora.

Hongera kwa Ufaransa kuchukua kombe baada ya kuibutua Croatia michomo 4-2. Mbape alitisha sana, Modric alifunika mbaya. Hata hivyo hao ni udambwidamwi wa dimbani Kombe la Dunia. Kuna udambwidambwi wa Urusi yote Kombe la Dunia. Unamjua?

Ngoja kwanza; Kombe la Dunia 2014 lililofanyika Brazil, aliyekuwa Rais wa Uruguay, Jose Mujica, ndiye alikuwa udambwidambwi, maana habari zake zilikuwa kivutio wakati wote michuano ilipokuwa ikiendelea.

Mujica alikuwa kivutio kwa namna alivyotangazwa kama Rais maskini kuliko wote duniani. Akiendesha gari aina Beetle Volkswagen (mgongo wa chura), akiendesha mwenyewe bila dereva. Alikuwa akiishi shamba, huku akitoa asilimia 90 ya mshahara wake kwa jamii isiyojiweza.

Mshahara wake kama Rais ulikuwa dola 12,000 (Sh27.3 milioni), lakini alikuwa anatoa msaada na kubakiwa na dola 774 (Sh1.76 milioni) kila mwezi. Yaani katika 27 milioni, unabaki na milioni 1 na laki 7. Mujica ni mtu wa Mungu sana. Na alibamba kwelikweli Brazil.

Basi World Cup 2018, achana na kila kilichotokea uwanjani, udambwidambwi Urusi yote kipindi cha World Cup 2018 ni Madame President Kolinda Grabar Kitarovic ambaye ni Rais wa Croatia. Mama aliteka mioyo ya wapenda soka ulimwenguni.

Nje ya uwanja, Kolinda alikuwa liwazo la wapenda soka. Picha zake za kawaida na zile za kuogelea ambazo zinafanya maungo yake ya sirini yaonekane dhahiri, zilisambaa sana. Si ajabu Croatia ilipofika fainali ikawa na mashabiki wengi ulimwenguni kuliko Ufaransa. Mama aliipamba sana timu yake.

Kolinda alikuwa kivutio aliposafiri kwa ndege daraja la makabwela, yaani economy. Alisafiri na watu wa kawaida kabisa. Mechi kati ya Croatia na Denmark, aliishuhudia jukwaa la mashabiki wa kawaida. Mechi zilizofuata aliwekewa utaratibu wa kukaa jukwaa la viongozi.

Baada ya mechi ya Croatia na Denmark, Kolinda aliingia chumba cha kubadilishia nguo na kukuta wachezaji wakiwa wameloa jasho baada mchezo, wengine vifua wazi na boxer tu, Kolinda bila kinyaa wala nini, alimkumbatia mmoja baada ya mwingine.

Kolinda ndiye hasa udambwidambwi wa World Cup 2018. Tutammiss sana Kolinda. Wengi wangetamani World Cup 2022 ifanyike Croatia badala ya Qatar.

Ndimi Luqman MALOTO

FB_IMG_1531796057824.jpg
 
Back
Top Bottom