Madaktari wanaonewa sana.Tusipoiambia serikali ukweli tutaangamia bila maarifa.
Tunaambiwa kwamba udaktari ni wito hivyo madaktari wawe kwenye moody hiyo. Lakini hao wanaoambiwa wafanye kazi kwa mode ya wito wanakamuliwa na serikali inayopaswa kuwaatamiza na kuwalinda ili wahudumie wito wao.
Angalia/soma hii screenshot uangalie namna serikali yetu inavyojiendesha kwa UKANDAMIZAJI
View attachment 2921951
Daktari analipia leseni yake kama Wakili anavyolipia leseni. Serikali inafanya biashara na kuvuna kutoka kwenye taaluma ya udaktari. Hata usome vipi udaktari hauwezi kuruhusiwa kufanyakazi nchini bila kulipia Kibali na Kodi ya kupata kibali hiko. Pili utalazimika kulipia leseni kila mwaka. Haya yote ya nini kwa serikali inayojali afya za watu wake?
Haya ni matatizo yatokanayo na kuacha mfumo ulioshindwa kuendelea kushika hatamu za nchi. Sanduku la kura liheshimiwe
Wizara ya Afya Tanzania nawakaribisha mtueleweshe haya mambo yana mantiki gani kisekta? Mnawakamua kisha mnawaambia ni wito. Kwa nini wito huo usianzie serikalini kama mfano?
Ina uma sana hasa walimu wanavyo onewa hadi unasema hivi nani alie turoga,,,,, kada ya afya na elimu ni lulu, serikali inajukumu mama la kuziangalia kwa jicho la pekee sana.Hii ni Kweli sana
Ni wakati wa MabadilikoIna uma sana hasa walimu wanavyo onewa hadi unasema hivi nani alie turoga,,,,, kada ya afya na elimu ni lulu, serikali inajukumu mama la kuziangalia kwa jicho la pekee sana.
Unafikiri tutafanyajeBongo ni mwendo wa kulalamika TU lkn tunatiii Kila Kitu
Wafanyabiashara wa kariaakoo walifanyaje kuwaondoa task force?Unafikiri tutafanyaje
Hii ni tofauti sana mkuu..Wafanyabiashara wa kariaakoo walifanyaje kuwaondoa task force?
Daktari ni kada yenye uelewa sana. Inahitajika akili ya kisomi kubadili mfumo huu kandamizi.Hii ni tofauti sana mkuu..
Mfanyabishara ukimfukuza anaweza kwenda sehemu nyimgine kuanzisha biashara..
Ila serkali ikifungia lesseni yako unabaki na jina tu la daktari ila hauwezi kugusa mgonjwa....
Unakuwa kama Kigwangala tu
Na bado mkuu Tukiwa Tunafanya kazi tunaonekana tuna akili sana na Think tank wa Taifa kwa maswala ya afya lakini ghafla tukistaafu wanasema watutunzie Pesa kwa kuwa hatuna akili katika matumizi ya pesa..Daktari ni kada yenye uelewa sana. Inahitajika akili ya kisomi kubadili mfumo huu kandamizi.
Mtu anakamuliwa kwenye leseni na Kibali kisha anaambiwa haya nenda kafanyekazi ya wito.
Sijawahi kuona popote kazi ya wito imlipishe gharama anayejitolea