UDADISI: Rushwa Tanzania

TheMeek

JF-Expert Member
Mar 12, 2016
460
400
Ndugu wanajamii,

Salaam!

Tafadhali, napenda kuchukua fursa hii kuandika machache kuhusu Rushwa Tanzania, ili sote kwa pamoja tushirikiane kuidadisi na kuitafutia namna ya kuipunguza kwaajili ya ustawi wa Taifa letu na Bara la Afrika kwa ujumla.

Ninavyoelewa Mimi, Rushwa ni ile hali ya kutumia #Hekima au #Ujuzi bila ya kuwa na #Uelewa. Namaanisha kutumia "Concepts" bila ya kuwa na "Precepts". Au kwa maana nyingine kufanya jambo pasipo kulielewa undani wake. (Kuiga- Kuigilizia- Kuegelezea).


Chanzo kikuu cha Rushwa ni Mahusiano ( Mahusiano Dhaifu) ambayo husabishwa na Elimu dhaifu au Elimu Duni ( Bora Elimu).

#ElimuDuni maana yake ni mapokeo potofu yenye fikra potofu zenye maono potofu na malengo potofu kwa ajili ya kuiba, kuua na kuharibu Taswira ya Taifa, Utu wa Mwanadamu, kuharibu Mazingira na viumbe vilivyomo kwenye Mazingira.


Mahusiano Dhaifu (Elimu Duni) humsababisha MTU kuvunja Sheria , Kanuni na Taratibu za Sehemu husika mfano , katika Taifa lake, Katika eneo lake la Kazi, Nyumbani kwake , n.k na kupelekea MTU huyo kugushi nyaraka, kufanya ngono, kuiba, kuchafua Mazingira, kuuwa , kupiga kelele, kutukana n.k


Yafuatayo ni machache niliyoyabaini kuhusu Rushwa Tanzania.


1. Sheria, Kanuni na Taratibu zikitungwa na wala rushwa, kamwe Taifa letu halitaweza kusonga mbele kimaendeleo wala kuwa na Amani,; Bali migogoro mingi pamoja na kero mbalimbali, mfano Muungano, Magonjwa ya Milipuko n.k zitaongezeka .

2. Rushwa ndio chanzo kikubwa cha Ugaidi, Ufisadi, Uonevu, Uvunjifu wa haki za raia, uvunjifu wa Demokrasia, Uovu wa kijinsia, Ushoga, n.k. Rushwa husabibisha utegemezi na kuwafanya watu wasifikirie sawa sawa.


3. Rushwa ikipanda, Deni la Taifa hupanda, Matumizi hupanda mfano, mfumko wa bei ; Usalama wa Taifa hushuka na kusababisha migogoro mingi zaidi,; mfano ugaidi, migogoro ya ardhi, Vita vya wenyewe kwa wenyewe, Ufisadi, Uonevu na Uovu wa kila aina ( Tamaduni , Mila, Desturi chafu)

Ndugu zangu wanajamii, Ni jukumu letu sote kwa kushirikiana pamoja, kulijenga Taifa letu, Kulilinda, Kulisimamia na Kuliendeleza katika misingi ya Haki, Demokrasia na Maendeleo.

Vita dhidi ya Rushwa ni vita ya kikatiba. Katiba ni Siasa. Siasa ni Uraia. Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunailinda Katiba yetu, tunaiishi, tunaisimamia na kuiendeleza kwa dhati kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu na Bara la Afrika kwa ujumla.

Kila Raia wa Tanzania anajukumu la kuhakikisha anaipiga Vita Rushwa kwa nguvu zake zote na Ujasiri wake wote ili kuhakikisha Taifa letu linabaki kuwa salama wakati wote.


Asanteni sana; Karibuni kuchangia mawazo na kudadisi zaidi.

MUNGU IBARIKI AFRIKA , MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
1. Tanzania kama taifa, tuna sheria za kuzuia/kupinga vitendo vya rushwa?

2. Kama tunazo, nani ana wajibu wa kuhakikisha zinafanya kazi?

3. Kama hakuna, tunasubiri nini kuwa nazo?

4. Wachache wenye nguvu ( fedha/ nyadhifa) wanafaidika kwa uwapo wa rushwa, wengi na wasio na nguvu wala jinsi ya kuipinga rushwa wanaathirika kila siku. Je njia gani itumike, maana sheria zinapindishwa, katiba bado inawapa baadhi mamlaka kupita kiasi, umma hauonekani kuwa na uwezo wa kuwaadabisha walio na nyadhifa mbalimbali.

5. Elimu ya uraia(mwema) itolewe kuanzia shule za awali, msisitizo uwe katika utu wa mtu, uzalendo kwa nchi na kuelewa haki za raia, sheria za nchi na wajibu kwa haki zao na za nchi.

6. Kwa sasa hayo yote yatawezekana kama kuna uongozi unaojali utu na uzalendo wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom