Udadisi; "Asiyefanya kazi na asile"

TheMeek

JF-Expert Member
Mar 12, 2016
460
400
Ndugu wana JF,

Salaam!

Napenda kuchukua fursa hii kwa dhati kabisa kushirikiana nanyi kudadisi maana halisi ya sentensi "Asiyefanya kazi na ASILE"

Kwa Uelewa wangu, sentensi hii ni ya kiuongozi (leadership) na ninaweza kuizungumzia kwa namna mbili.

1. ELIMU

Jukumu kubwa la Kiongozi yeyote huwa ni Kuongoza. Kiongozi ni lazima aongoze kwa Hekima (Busara), tena kwa kutumia Elimu na Haki (Usawa wa Binadamu). Hapa Elimu (Maono+Malengo+Fikra) ndio msingi mkuu katika UONGOZI.

Kiongozi anapaswa kuwaelimisha anaowaongoza kwa Upendo na kwa Upole ili waweze kuwa wazalendo, watiifu, wanyenyekevu na wachapakazi (pasipo woga) , kwa ajili ya Ustawi wa Eneo lake.

Mtu yeyote aliyepata Elimu kutoka kwa Kiongozi huyu, akaidharau, akaibeza au kutoitii, basi hatakiwi kuelimishwa tena ( adhabu yake ni kutoipata Elimu hiyo tena , itakayo ambatana na adhabu nyingine zilizipo chini ya Sheria za eneo husika - kwani kukataa Elimu ya Kiongozi Bora ni kuvunja sheria za eneo lake)

Kwahiyo basi, ni lazima MTU aelimishwe kwanza, ndipo aende kuyafanyia Kazi aliyoelimishwa. Na iwapo MTU huyu akielimishwa na akaacha kuyafanyia Kazi aliyoelimishwa, basi hatakiwi kuelimishwa tena. Yaani, Asiyefanya Kazi na ASILE!


2. CHAKULA

Sote tunafahamu kwamba chakula ni Nguzo muhimu sana katika Maendeleo ya mwili wa Mwanadamu. Hivyo basi , ili Mwanadamu aweze kufanya shughuli zake vizuri ni lazima apate chakula Bora kwa ajili ya kumpa yeye Nguvu, Ujasiri na Dhamira njema.

Hapo maana yake ni kwamba, MTU hawezi kufanya Kazi akiwa na njaa- Ni lazima mtu huyo ale chakula kwanza ndipo akafanye kazi. (Sawasawa Ndugu zangu!)

Iwapo MTU huyu akila chakula na akaacha kufanya Kazi , basi hatakiwi kupewa chakula tena. Yaani, Asiyefanya Kazi na ASILE.

Asanteni sana. Na karibuni kwa UDADISI zaidi.

MUNGU IBARIKI AFRIKA , MUNGU IBARIKI TANZANIA

b4f0580331c25e806b462597a9fa1eec.jpg
 
Back
Top Bottom