UDA waandika historia Dar

UDA waandika historia Dar

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
JUMATATU, AUGUST 25 2014

Uongozi wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na wamiliki wa daladala mkoani humo, wamesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano ili kushinda zabuni ya kuendesha Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART).

Utiaji saini huo ulifanyika Dar es Salaam juzi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ukishuhudiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia pamoja na na Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Said Meck Sadiki.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bi. Ghasia alisema uamuzi uliochukuliwa na UDA pamoja na wamiliki wa daladala ni mfano wa kuigwa nchini.

Alisema kuungana kwao pamoja, kutawajengea mazingira bora ya kuaminika zaidi na kutoa ushindani madhubuti dhidi ya kampuni za nje ambazo zitajitokeza kuomba kuendesha mradi wa DART.

Alimpongeza Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Saimon Group, Bw. Robert Kisena na viongozi wa vyama vya wamiliki wa daladala mkoani humo kwa uamuzi huo wenye tija kwa Taifa kwani utaongeza ajira na kupunguza umaskini.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya mkutano uliokuwa na mafanikio makubwa uliofanyika jijini humo hivi karibuni katika Ukumbi wa Karimjee ulioandaliwa na Kamati Teule ya Wamiliki wa Daladala.

Kwa upande wake, Bw. Sadiki alisema kuunganisha nguvu kwa wadau hao kutatoa fursa kwa Serikali kuwaunga mkono katika jitihada zake za kuboresha hali ya usafiri katika jiji hilo.

"Serikali inatambua jitihada zinazofanywa na wazawa kwani haiwezi kutumia mabilioni ya fedha kujenga barabara hizo halafu mtu wa kuziendesha atoke nje, hii itakuwa aibu na dharau.
"Kuungana kwenu, kutaishawishi Serikali baada ya kutangazwa zabuni, ianze kuwafikiria nyinyi kwa kuwapa kipaumbele kwani hii ni ishara kwamba, mmedhamiria kupambana katika zabuni," alisema Bw.Sadiki.

Naye Bw. Kisena, alisema watafungua milango kwa wamiliki hao kununua hisa ambazo zitamwezesha mtu yeyote kuwa Mkurugenzi.
"Tunatoa wito kwa wananchi mbalimbali, wajitokeze kununua hisa kwa wingi zaidi ili kuhakikisha tunaboresha huduma ya usafiri katika jiji hili," alisema Bw. Kisena.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Daladala mkoani humo (DARCOBOA), Sabri Mabrouk, alisema UDA ni kampuni yenye uwezo hivyo kuna haja ya kuunganisha nguvu ili kuhakikisha zabuni inapotangazwa hakuna kampuni kutoka nje itakayoshinda.
"Hakuna sababu ya kumwachia mtu kutoka nje aje kuendesha mradi huu, tukikusanya mitaji tukaungana na UDA, tutaweza kuendesha mradi huu kwani hauhitaji fedha nyingi sana, tukiamua tunaweza," alisema.

CHANZO: Majira
 
Hawa UDA ni mkoloni mweusi, watuambie kwanza hilo shirika wamelipataje kama siyo njia za kiujanjanja. tunataka mawazo mapya UDA hawana lolote, magari yao yanajaza kupita kiasi, madereva very rough harafu tuwape na DART. Hii napinga tunataka mwekezaji kutoka nje.
 
Maneno mengi lakini sijaelewa vizuri wameungana kwa lipi??
 
Mmh wendawazimu wameunda chama tunalo tusio na usafiri wanadengua hao wakiona folen ubungo ruti inahamia mbagala au kwingineko
 
Huyu KISENA R, si aligombea Ubunge Maswa akashindwa.Hamkumbuki haka ka bwana kalimpiga na kujeluhi vibaya OCD,matokeo yake ocd alipata adhabu ya kuhamishwa na kushushwa cheo.
 
Wamiliki wa daladala wanauzana wao kwa wao.
Wameingia choo cha kike.We basi gani za Uda hazina Ruti maalum.
Hata Ulaya gari zote zina Ruti maalum na haibadiliki.
Ila Uda wao wanafanya wanavyotaka kwa amri ya dereva na utingo tu.Halafu eti wanasema wanafuata mifumo ya wenzetu.
UDA + DECI = Familia moja
 
Hawa UDA ni mkoloni mweusi, watuambie kwanza hilo shirika wamelipataje kama siyo njia za kiujanjanja. tunataka mawazo mapya UDA hawana lolote, magari yao yanajaza kupita kiasi, madereva very rough harafu tuwape na DART. Hii napinga tunataka mwekezaji kutoka nje.
Ili kupata jibu la hili swali nenda magogoni.
 
Uda cha kwanza wana kesi juu ya mmiliki Ni nani. Uda miaka yote Ni ya serikali kupitia DDC. Sasa imefikaje kwa mtu binafsi mpaka sasa Ni kitendawili! Wajibu watanzania wamemiliki vipi Uda kwanza ndipo waendelee Na michakato Yao!
 
Kumbe mabasi yaendayo kasi yatakua ndio haya haya ya UDA yalioko mitaani Tanzania bwana duh.!!!
 
MAMLAKA ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imesema Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), kipindi hiki linawapa wakati mgumu kutokana na kushindwa kutii taratibu zilizowekwa barabarani.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mfawidhi Sumatra Kanda ya Mashariki, Conrad Shio, alisema hadi sasa kuna mabasi ya UDA 150 ambayo yanafanya safari bila kusajiliwa na mengine ambayo yamesajiliwa, bado hayajapakwa rangi na kuwekwa vibao vinavyoonyesha yanakotoka na yanakokwenda.

Alisema mwitikio wa UDA kuweka rangi na vibao hivyo haupo huku makondakta nao wakikaidi kuvaa sare, sambamba na kukatisha njia.

"Bado tunasisitiza UDA zipakwe rangi na pia ziwekwe vibao ambavyo vinaonyesha sehemu zinakotoka na zinakokwenda, tunaomba UDA kufanya utaratibu unaofanywa na daladala ili kuweza kwenda sawa," alisisitiza Shio.

Aliongeza kuwa kwa sasa wana vikao vya mara kwa mara na UDA na siku za usoni muafaka utapatikana.

Alibainisha kuwa kwa wastani wamekuwa wakizikamata UDA tatu kwa siku na huzipiga faini kati ya sh. 150,000 na 250,000 kulingana na makosa husika.

Shio, alitoa wito kwa abiria kuendelea kutoa taarifa pale magari hayo yanapokatisha njia ama kupandisha nauli.

Alipotafutwa Msemaji wa UDA, George Maziku, alisema kwamba si kweli kuwa kuna mabasi yao 150 hayajasajiliwa na akahoji kama yapo kwanini washindwe kuyakamata.

Kuhusu sare, alisema madereva na makondakta wao wote wamepewa, ila kama ni suala la kutozivaa ni ukaidi wao wenyewe.

Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kutokana na jinsi UDA inavyofanya kazi zake, ikiwamo njia zake kutoeleweka, kukatisha njia na kutoza nauli kubwa.
 
Dar es Salaam
Mabasi mengine 25 ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), yamekamatwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Baharini (Sumatra), kutokana na kuendelea kukaidi amri ya kuwataka wafuate sheria za usafirishaji wa abiria jijini.Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mfawidhi wa Sumatra, Conrad Shio alisema mpaka sasa wameshayakamata mabasi 40, kati ya hayo, 15 yalikamatwa wiki iliyopita.

Madereva wa mabasi hayo wanadaiwa kufanya makosa tofauti ikiwa ni pamoja na kutokuwa na leseni ya uchukuzi wa abiria jijini Dar es Salaam, inayotolewa na mamlaka hiyo, stika na vibao vya kuonyesha njia wanazokwenda.

Shio alisema walipoyakamata awali na kuyaachia, uongozi uliahidi kutekeleza maagizo waliyopewa na Sumatra lakini hawajayatekeleza mpaka sasa.

Alisema pia wamesitisha kwa muda kazi ya kuyakamata na sasa wanaendelea na mazungumzo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema baada ya mazungumzo hayo, atakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kuzungumzia hatua zaidi ambazo watachukua au kile ambacho watakuwa wameafikiana kwa vyombo vya habari.

"Tumeona tusitishe operesheni hii ya kuyakamata mabasi haya ili kutoa nafasi ya mazungumzo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa na iwapo mwafaka usipofikiwa tutajua cha kufanya" alisema Shio.

Kulingana na makosa ambayo yamekutwa katika mabasi hayo, kila basi litalazimika kulipiwa Sh250,000 na kwa mabasi 40, Uda watalazimika kulipia Sh10 milioni. Wiki iliyopita, Sumatra ilianzisha operesheni ya kuyakamata mabasi ya Uda kutokana na malalamiko ya wananchi kuwa yamekuwa yakivunja sheria na hayana stika wala vibao vinavyoonyesha njia wanazopita.




Mwananchi
 
Hizo daladala zisizoenda kasi wameshindwa hayo yaendayo kasi watawezaje!
Wanakatisha ruti hao wahuni wa UDA.
 
Hizo daladala zisizoenda kasi wameshindwa hayo yaendayo kasi watawezaje!
Wanakatisha ruti hao wahuni wa UDA.

Kuna thread humu ilisema SUMATRA wametangaza kurudisha usafiri wa Kivukoni mwezi wa saba mwishoni kuondokana na unyonyaji wa UDA kwa ruti ya M/mmoja-Kivukoni. Tunaelekea September now, wako kimya na jamaa wa UDA bado wanajineemesha, sijui nini kimewapata hawa jamaa...
 
Back
Top Bottom