Wamiliki wa daladala wanauzana wao kwa wao.
Wameingia choo cha kike.We basi gani za Uda hazina Ruti maalum.
Hata Ulaya gari zote zina Ruti maalum na haibadiliki.
Ila Uda wao wanafanya wanavyotaka kwa amri ya dereva na utingo tu.Halafu eti wanasema wanafuata mifumo ya wenzetu.
UDA + DECI = Familia moja
Yote uliyosema ni mazuri, ila naomba sana msipende kulinganisha na Ulaya. Hapa sio Ulaya na wala hakuna sababu ya kufuata ya Ulaya tunapofanya ya kikwetu. Taja adhari za mfumo ili tuchangie kurekebisha kama zipo. Natumai ni vema kuangalia mazingira na mazingara ya mambo yenyewe ndipo tuone ni yapi yanalinganishwa na Ulaya na yapi ni ya kikwetu kwetu. Ulaya nao kabla ya kufikia hapa walikuwa na taabu taabu zao. Walivyozitatua ni kuangalia hali zao wakafikiria suluhisho, hawakujiuliza kwa mbona Afrika au Asia au marekani wanafanyaga hivi?