Konda wa bodaboda
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 7,981
- 4,174
Nimefanya uchunguzi kuhusu akina dada walio na umri pungufu ya huo nilioutaja kwenye kichwa cha habari. Katika sehemu nyingi nilizotembea kwa bongo, nimegundua kuwa mabinti warembo walio chini ya miaka 25 wengi wao huwa hawasalimii vijana wenzao wa kiume kwa sababu ambazo bado sijazijua.
Mabinti hao hawaishi kwenye salamu tu, bali hata kumsemesha kijana wa kiume wakiwa kwenye usafiri wa umma au kituo cha usafiri ni kitu kigumu kwao. Hii inatofautiana na vijana wenzao wa kiume ambao kusalimia ama kusemesha chochote ni kawaida kwao. Nimegundua pia, mdada anayethubutu kumsalimia kijana wa kiume ni dalili ya wazi kuwa ni mgeni wa sehemu alipo ama kuna shida ambayo anahitaji msaada wa muda mfupi.
Nikagundua pia kuwa wengi wa wenye tabia hiyo ni wale ambao kwa nje wanajulikana/kujijua kuwa yeye ni wa juu.
Nimejaribu kutazama kwa kulinganisha kwa kutumia saikolijia ya kibinadamu kati ya wenye uzuri wa muonekano wa nje na wale wanaoonekana/kujiona ni wa kawaida kwa wengine nikapata tofauti ya kwamba wale wanaoonekana hawana mvuto kuliko wenye mvuto ndio huwa rahisi kusalimia au kusemesha jambo kwa kijana wa kiume.
Nimejaribu pia kulinganisha wadada wenye uzuri/mvuto wa nje walioolewa na ambao hawajaolewa nimegundua kuwa wengi wao walioolewa wanakuwa na tabia tofauti na ile waliyokuwa nayo kabla hawajaolewa (hii ni kwa wale walioolewa na kufika umri wa miaka 25).
Nikachunguza tena kwenye suala la ndoa, nikaona kuwa wengi wao huchelewa kuolewa na pia huolewa na wanaume waliopishana sana umri. Huku wengine wakiolewa na wanaume wenye mionekano isiyovutia na pia huchelewa kuolewa tofauti na wenzao wasio na mvuto mkali wa nje. Nimegundua kuwa wanaume wengi ma-handsome huoa wanawake wasio na mvuto mkali kwa nje(wa kawaida).
Vipi kwa upande wenu wadau, mnalionaje hili?
NOTE: Mdada usitumie maneno yangu kuongeza tabia ya kupiga kimya wakati sura yenyewe tu mmmmh!