Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka, Yakafuata Mashirika, Sasa ni Zamu ya Media Ina-suffer

Wataalamu walisema mkuu aliingia na "shock therapy" kunyoosha nchi na waliokuwa wakilia kuumizwa kiuchumi ni wapiga dili. Sasa inawezekana kwenye media kuna wapiga dili wengi na sasa ni zamu yao nao kunyooshwa. Hivyo ndugu Pascali tuendelee kumuombea mkuu akamilishe zoezi la kuinyoosha nchi kwani yajayo yanafurahisha.
 
Na bado kucha kuchwa kwa Musiba, Bashite mara waziri nani. Ina maana msipoenda hamli? Waachieni TBC, musiba tv, na ndugu zao wote nyie fanya yenu.
 
Ili tusibishane hebu fafanua, kampuni kama ya Mayalla ilikua ina corrupt nini and how? Kampuni kama Benchmark production na yenyewe ilikua ina corrupt nini and how!? Sioni tofauti ya hiki wanacho lalamikia kina Mayalla na suala la ununuzi wa Korosho kule kusini, lengo linaweza kua zuri na matokeo ya sasa au mwaka hu yakawa mazuri but matokeo ya mbeleni yakawa mabaya, ukitazama mfumo tunao kwenda nao sasa hivi ni kama tunafata mfumo wa UJAMAA na kujitegemea, mfumo ambao ulishindwa vibaya Enzi za Nyerere na of course umeshindwa everywhere in the world. Time is the best teacher, let us wait brother.
Hizo kampuni unazo ziita kua ni zakitapeli ndio zilikua walau zina AJIRI baadhi ya wahitimu, by now serikali haiajiri na bado imezuia channels za pesa halali kwenye sekta binafsi (jambo ambalo linaweza kua zuri kwa upande mmoja) na sekta binafsi is either zinapunguza wafanyakazi au kufungwa kabisa, matokeo yake tunaongeza WAZURULAJI mitani and hence possibility ya kuongezeka VIBAKA mtaani ni kubwa!
 
Sasa mtu kama wewe Mayalla ilibidi umwambie ukweli kiongozi na wala usisifie tu, hata kama una maslahi yako binafsi. Nchi inakwenda kubaya.
Mkuu Sijali, natumaini umenielewa na kwa bahati nzuri sana, sina maslahi yangu binafsi yoyote.
P
 
Leo kumepatikana habari njema kwa Baba la Baba ametumbukiza mkono Channel Ten na kuinusuru sasa rasmi Channel Ten iko chini ya serikali kwa mgongo wa CCM, maana tusemezane la ukweli, CCM kama CCM haiwezi.

Hongera Channel Ten kupata bail out. Sasa bado Star TV.
P
 
Kijana wa Mayalla haya uliyoyatabiria kwa channel 10 leo yamepata dawa! sasa swali ni je tasnia ya habari nyote sasa mkafugie njiwa huko na mtumie vidumu kuchota maji huko?
Bado kuna kazi na sasa Exim zamu yao imefika afatae nani?
 
Mayala mimi naandika kitabu kinacho husu ujasiliamali namna ya kuanzisha na kuendeleza biashara najua watu wengi wameandika vitabu vya aina hiyo nitachangia kidogo kutoka Kwenye kitabu changu kuna topic inaitwa ''An Entrepreneur and his enviroment '' Mjasilamali na mambo yanayo mzunguka.hili huanzia kwenye Familia hadi Kimataifa ina husu mambo ambayo yanaweza athiri biashara mfano: ukifungua tu biashara unakuta TRA hao wakitoka tu watu wa Liseni hao wakitoka wa osha n.k Serikali ni chanzo kikuu kutokana na sera zake. Serikali ina majukumu matatu muhuhimu The Government has three roles 1. Regulatory role 2. Supporting role .3.Participating role Majukumu ya serikali kwa sekta binafsi ni matatu 1.Kusimamia mfano TRA 2.Kushiriki katika mipango ya kukuza biashara 3.kushiriki moja kwa moja mfano ujenzi wa ukuta wa melelani
Tatizo ninaloliona mimi nikwamba Serikali imejisahau kushiriki kwenye mipango ya kukuza biashara ''supporting role'' Serikali kuwa mkopaji mkubwa kwenye mabenki ya ndani ni tatizo na kuto lipa Madeni ya ndani kwa wakati nitatizo kubwa pia Lengo la ''topic'' ya an entrepreneur and his environment
(mjasiamali na mambo yanayo mzunguka) ni kuweza kujua nini lakufanya kuweza kukabiliana na yanayo kuzunguka kuweza kufanikwa kwenye biashara zetu. Swali fikirishi je unaweza kukabiliana na serikali km maridhiano hakuna ?
 
KUNA kampuni moja ya tours, kubwa sana nayo ni ya ccm, nitawajuza na makampunin mengine 39 makubwa ya ccm, hii nchi ioneni tu kama ilivyo
 
KUNA kampuni moja ya tours, kubwa sana nayo ni ya ccm, nitawajuza na makampunin mengine 39 makubwa ya ccm, hii nchi ioneni tu kama ilivyo
Lazima ni ile iliyoko Arusha. ILe inayoongoza kwa kuwapunja wafanyakazi na kule Kilimanjaro inaongoza kwa vifo vya porters
 
Paskali umenena vyema! Kwetu sekta ya uchapishaji (publishing) ndio balaa, kampuni zimeshindwa kulipa mishahara, pango na kodi ya serikali kisa hakuna zabuni ya vitabu bora vya shule toka serikalini, ilihali watoto na walimu wana hali mbaya ya ukosefu wa vitabu. Ndg tuombe mungu si mchezo, tumuombee pia mh rais mungu amuwezeshe aangalie na huku kwenye elimu. Asiwaamini kwa kuwasikiliza watendaji wa wizara, atumie vyombo vyake kuchunguza ukweli kuokoa taifa la kesho kielimu, vitabu bora shuleni hakunaaaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…