Uchomaji wa silaha za wakimbizi

Mwanitu

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,036
592
Gazeti la leo la Mwananchi lina picha mbele ikionyesha jeshi la polisi likijitayarisha kuchoma lundo la silaha zilizoingizwa nchini na wakimbizi.
Baadhi ya silaha hizo zikiionekana katika hali ya upya.Swali kwa wataalam nauliza kwa nini silaha hizo zisikaguliwe na kutumiwa majeshini kwetu badala ya kuzichoma?Au kuna sheria za kimataifa zinakataza hilo.Sioni sababu tuchome silaha za bure na kesho tukanunue silaha.Kama ni kudhibiti si tayari ziko kwenye mikono salama?wataalam tafadhali?
 
Kuna sheria za kimataifa zinakataza hilo. Silaha haramu ni silaha haramu tu na haiwezu kubadilishwa na kuingizwa katika mfumo wa uhalali. Hivyo ni lazima iteketezwe
 
Silaha haramu ni haramu mkuu.

Mbaya zaidi zinakuwa silaha za wizi zilizoibiwa kimagumashi kutoka kwenye majeshi ya nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom