Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 47,207
- 32,705
Ritz,
Katika miaka ya 1960 Abdu Sykes alimpangisha nyumba yake
Issa Nassor Ismaily aliyekuja kuandika kitabu "Kinyang'anyiro
cha Zanzibar."
Siku moja Sheikh Issa alimuuliza Abdu Sykes ilikuwaje hata
yakatokea yalotokea?
Abdu alimsihi Sheikh Issa kuwa wasizungumze habari za Zanzibar
kwani zinaweza kuvunja udugu wao.
Toka siku ile Abdu na Sheikh Issa hawakupata tena kurejea habari
zile hadi Abdu alipokufa na Sheikh Issa si muda mrefu akahamia
Oman.
Ndipo ninaposema kuwa ndugu zetu wanasoma historia sisi tumeishi
ndani ya historia.
Kwa miaka mingi nimefahamiana na Sheikh Issa na nimemtembelea
kwake Mascut.
Mohamed Said,
Unachosema ni kweli kabisa mimi takupa kisa kimoja wala hakina muda mrefu.
Pale Msikiti wa Kichangani Magomeni kulikuwa na mzee mmoja walikuwa wanamuita makoti amefariki mwezi uliyopita makazi yake yalikuwa hapo hapo Msikitini.
Kipindi cha mwisho wakati mgonjwa kuna kauli alikuwa anazitoa anaelezea unyama waliokuwa wanaufanya Zanzibar wakati wa mapinduzi huwezi amini yule mzee watu wengi walimchukia hata wale waliokuwa wanamsaidia.
Yule mzee alikuwa ni Mmakonde walitokea Tanga kwenda Zanzibar.
Bora yule mzee angekaa kimya wala watu wasingejua.
Last edited by a moderator: