Watoto wa hasidi Mohamed Said wameamua kumuokoa mzee wao kwenye kibano. Walipoona kabanwa na ile longolongo ya balozi wa Marekani kuhutubia bunge, hawakuwa na jingine zaidi ya kuupotosha mjadala!Naona mnakasha umeshageuka kutoka wazee wa Gerezani hadi mapinduzi ya Zanzibar.
Duh! sasa hizo ndio hofu za kishirikina. Unasababu gani wewe kujiita Great Thinker kwa ushirikina huu?Cha kudebate tena hakuna kwani uovu wa Nyerere hata Mungu muumba wa mbingu na ardhi ametuonesha.
Halafu nasikia kaburi lake lilikuwa likitoa sauti za vitisho vya ajabu.Walinzi wa kaburi ile wiki ya mwanzo walitimua mbio kwa sauti mbaya sana kama ya mbwa
Woooooooooooooooooh!,Woooooooooooooooh!
Barubaru, mbona hujibu swali uliloulizwa na Jasusi? umeulizwa "mlitaka kumwambia nini Nyerere?"Jasusi.
Waarabu tuna usemi mmoja IN ORDER TO BUILD SOMETHING STRONG, IT HELPS TO START WITH BEST AND POSSIBLE MATERIALS. Na waswahli wanasema kila kitu ni msingi. kama umeweka msingi mbovu hata ufanyeje huwezii jenga kitu imara.
Sasa wa TZ ndio mupo hapo msingi mboovu mliojengewa na JKN ndio huo unaowasibu mpaka leo.
Kuhusu mzee Bomani naona tusiongee mengi kwani namfahamu vizuri sana sana sitaongea mengi bali mpe salam zangu atakwambia mengi kuhusu Mimi. Muulize tu Hamza Yousuf (alizoea kuniita Mwarabu au Mznz) kisha utanieleza.
Pole ndugu yangu
Ritz, wacha uongo, Mohamed Said hashambuliwi kwa sababu ya dini yake, bali anakosolewa hapa jamvin kwa mambo makubwa mawili, moja ni kutumia uislam kupotosha historia ya Tanganyika, ya pili ni kuandika uwongo kwa malengo ya uchochezi. Yote mawili yameoneshwa waziwazi hapa. Kwamba balozi wa Marekani alihutubia bunge ni uongo! kwamba Nyerere alikuwa adui wa waislam huo ni uongo na uchochezi!Nyie mbona mmeungana kumshambulia Mohamed Said kutoka na dini yake. Umeishajiuliza kwa nini mmeungana Wakiristo wote na watu wa Musoma kumtetea Nyerere.
Huu ni utetezi dhaifu sana katika nyanja za kisomi! "historical facts" zinabakia kuwa "fact" bila kujali zimesemwa au kuandikwa na nani, mzungu au mweusi. Kinachobadirika ni uchambuzi wa "facts" hizo. Kwamba Nyerere na watanganyika wenzake waliunda TANU na kudai uhuru ni "historical fact" iandikwe na Mohamed au Illife itabakia kuwa historical fact. Lakini kwamba katika mapambano hayo ya uhuru waislam ndio waliomsaidia zaidi Nyerere kuliko watu wengine na hivyo wanasitahili sifa na heshima kuliko watanganyika wengine, hiyo ni "Opinion" ambayo Mohamed na Illife watatofautiana. Na ni hapo ndipo Mohamed hatakubali kushindwa na Illife kwa sababu yeye ni muislam na Illife sio muislam!Jasusi,
Wewe umepokea kwa Judith Listowel.
Mimi nimekaa na Sheikh Haidar Mwinyimvua.
Sheikh Haidar Mwinyimvua ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wazee.
Wazungu waijue historia ya TANU kunishinda mie mjukuu wa mashujaa hawa?
Huo ni muhali.
Si Listowel wala Iliffe anaweza kuwajua watu hawa kunishinda.
Mie nimeishi na wazee hawa toka udogo wangu hadi hawa wazee walipoondoka duniani.
Walinipa mengi kuhusu TANU na Nyerere.
Sahihisho kwa Lady Listowel.
Mwaka 1965 Sheikh Takadir alikuwa hayupo duniani.
Unajuaje kama yalikuwa mageni kwetu?Kwani wewe ndio mumiliki wa taaluma ya historia?Wickama,
Ahsante nimefahamu.
Mimi huingia katika mjadala kusoma na ikibidi nisomeshe.
Sheikh wangu kaniusia anasema,"Ingia katika mnakasha usome
au usomeshe. Usiingie kutafuta ubishi kwani ilm ya ubishi haina
baraka."
Mie simo humu kutafuta ushindi.
Nataka nikupeni yale yaliyokuwa mageni kwenu.
Bado unajiita Great Thinker!Tutajie ni nani au yupi aliejitambulisha kwa iman ya uislam kwenye huu mnakasha anaempinga Mohamed Said,na yupi aliejitambulisha kwa imani ya kigalatia pia anaemsapoti na kukubaliana na Moh Said??
Tutajie,kama wewe ni miongoni mwa wale wasemao kweli basi..
Mufilisi...
Kwani hujui kwamba watu wamejificha kwenye majina ambayo sio halisi? Kwani Ritz ni jina lako halisi? kwa hiyo ulitegemea watu watataja kilahisi imani zao? kama wapo ni mimi na wewe tu.Tuna miezi minne kwenye huu mnakasha ukimtoa Mkandara ambaye anajulikuna jamvini alivyokuwa na mahaba na Nyerere hebu nitajie Muislam yeyote kwenye huu uzi ambaye anakubaliana na "nyie" kama siyo huyo jamaa wa Musoma ambaye anamuona Nyerere ni nabii.
gombesugu, Ami, Zali la Mentali, Kadogoo, THE BIG SHOW,
Childish!Umeishajiuliza kwa nini nyie Wakiristo wote mnampinga Mohamed Said na kumtetea Nyerere kama mtakatifu wenu.
Bravo mkuu.Wickama, katika bandiko lako#13364 umeandika mengi muhimu sana, nakushukuru sana.
Hoja ambayo Mohamed hajaweza kuiongelea ni kuwa endapo EAMWS ilipigwa marufuku huko kwingine ilizuiliwa na nani?
Kuna hoja ya sheikh kupewa wadhaifa na kuukataa, kwa upande wa kumuonyesha Nyerere alivyo mbaya Mohamed anadai wazee wote walitupwa na vyeo kupewa wakristo. Sasa hili lipo wazi na amekaa kimya kwa kutambua kuwa kuligusa kutazua mambo mengine.
Katika mgogoro wa Issilamiya fil Tanganyika washiriki wake ndio wale waliounda AMNUT.
Hoja ambayo Mohamed hajathubutu kuiongelea ni kwanini katika chaguzi AMNUT ilishindwa.
Kuna tatizo moja kubwa sana ambalo wengi hawapendi kulisikia lakini ni vema kulisema.
Leo BAKWATA ikizikwa kabisa bado kutakuwa na migogoro ndani ya chombo kingine.
Hii inatokana na ukweli kuwa waislam wa Tanzania hasa wasomi wa kiislam wameacha mambo yanayowahusu kwa ima wasio na ufahamu au half baked kama tunaoona hapa.
Narudia tena wasomi na watu wenye weledi wamechukua back seat.
Endapo kungekuwa na wasomi walio mbele basi wangeshampiga break Mohamed na wafuasi wake kwa kumwambia aseme na awaambie watu ukweli wa matatizo yao na wala si kueneza usengenyaji, uongo na chuki.
Kwa bahati mbaya wanaogopa pengine kufanya hivyo ni kukufur.
Ujenzi wa hoja wa kundi hili la Mohamed ni wa kiwango cha kusikitisha ndugu Wickama.
Hili wanalomlaumu Nyerere kuhusu Mapinduzi utashangaa kuwa lina sura tatu.
Kundi la kwanza ni hili la Mohamed linalomuandama Nyerere. Kundi la pili ni lile linalosema Mapinduzi daima na kundi la tatu ni la wale wasiokubali kuhusu Nyerere na wasiokubaliana na kundi la pili.
Hoja inajiua hata kabla haijajadiliwa. Pengine utafunguliwa uzi tujadili
Kwahiyo kuna tatizo la kiuongozi na hili linatokana na kukosekana kwa wasomi. Wasomi nina maana watu wenye weledi uwe wa dini au elimu nyingine. Imekuwa proved kuwa Ponda ambaye ni swahiba yake Mohamed hana elimu ya dini wala ya kawaida(dunia). Lakini ndiye yupo katika steering wheel.
Watu wanaonekana kuwa na weledi ndio hawa ambao mstari mmoja unaua hoja nzima. Hapo hamuoni tatizo.
Hawafikiri kwa upana zaidi ya kujifungia na kutunga hadithi! Hao ndio wasengenyaji wakubwa, wenye farki na chuki na ni hao hao wanaoongelea dhulma kana kwamba kuna kadhambi kadogo na dhambi kuubwa!
Pumba Pumba Pumba...!
Tulia Zali la Mentali akulambishe dawaa...
Ni kweli bwana mkubwa hata wewe inawezekana umevaa ngozi ya kondoo kumbe ni chui,wewe ni "ATHIEST KUMBE NI PADRI" Ha ha haa... mkuki kwa nguruwe.Kwani hujui kwamba watu wamejificha kwenye majina ambayo sio halisi? Kwani Ritz ni jina lako halisi? kwa hiyo ulitegemea watu watataja kilahisi imani zao? kama wapo ni mimi na wewe tu.
Jasusi,
Hapana tabu.
Nakuongezea kitu.
Judith Listowel alikuja Tanganyika 1962 kuja kufanya utafiti wake.
Aliyempokea ni Ally Sykes kwa kuelekezwa na Peter Colmore.
Nimesoma barua za ''aerogram'' ambazo Listowel alikuwa akimuandikia
Ally Sykes kutoka London katika nyaraka za Sykes.
Hizi zipo pamoja na barua za Chief Thomas Marealle na Rashid Kawawa.
Barua hizi zina mengi.
Jasusi najua ungependa kujua vipi Chief Thomas Marealle alivyokuwa
akimchukulia Nyerere.
Zipo habari za Nyerere katika moja ya barua hizi ambapo Chief Marealle
alimtakidi Ally Sykes kuwa rafiki kipenzi wa Nyerere.
Hii ilikuwa miaka michache kabla ya uhuru.
Katika barua hii alimwambia Ally Sykes kuwa ipo siku tukipata uhuru aitataka
aje azunguze habari zile.
Historia ya TANU ina wachezaji wengi, ina visa vingi vya dhahir na vingine
vilivyojificha.
Mzungu hawezi akavipata na ndiyo maana unaona Iliffe na Listowel wana
mambo hawakuweza kuyajua.
Kuna rafiki yangu hapa anataka kunibeza ati siwezi kujua habari za wazee
wangu hata kama niliishinao.
Ati mimi nimemuiga Iliffe.
Mie nimuige Iliffe...
Ama akutukanae...
Namshauri asome kisa cha Abdulwahid Sykes na Dockworkers Union nilichoandika
mimi kisha asome kisa hicho hicho kama alivyokiandika Iliffe aone tulivyoghitilafiana.
Iliffe kamtoa Abdulwahid katika kisa kile.
Mimi nimemrudisha tena kwa taarifa nyingi sana.
Kile kisomo cha Shamba kwa Mohamed Abeid kapuruzia mie nimeeleza hadi
maana kwa nini Waislam wakati wa harakati dhidi ya ukoloni walikuwa hawafanyi
jambo sharti watawasul.
Isomwe Qur'an kwanza ndipo waingie vitani.
Mimi nimemueleza Hamilton jinsi alivyokuwa ndumila kuwili yeye hilo hakulipata.
Yote haya kanihadithia mzee wangu Islam Barakat aliyekuwa bega kwa bega na
Abdu Sykes katika ''labour movement'' kuanzia 1948 hadi 1950 na kashuhudia
migomo yote.
Wanajamvi kisa hicho nimekiweka chote hapa jamvini.
Kisomeni.
Ninayo mengi.
Si kitu Ritz kanishauri nijaribu kuandika riwaya za mapenzi.
Naufikiria ushauri wake kwa bidii sana.
Naanza kupitia vitabu vya Barbara Cartland kwa kuanzia huenda nikapata
vitu vya kunisaidia.
Boko, ni lini utaipa akili yako nafasi kufanya kazi japo kidogo tu? Padri atakuwaje Atheist? au hujui Atheism ni kitu gani! hakika Mohamed Said hasidi mkubwa atakuua roho na akili mtoto wewe.Ni kweli bwana mkubwa hata wewe inawezekana umevaa ngozi ya kondoo kumbe ni chui,wewe ni "ATHIEST KUMBE NI PADRI" Ha ha haa... mkuki kwa nguruwe.
Tatizo lako ukisoma post zangu unazisoma kwa ushabiki wewe umesema watu wameingia jf kwa majina ambayo sio halisi kwahiyo huwezi kujua imani yake na mimi nikakwambia hata wewe inawezekana unajifanya ni ATHIEST kumbe ni PADRI hebu jitahidi kuwa muungwana kuwa mstaarabu hivyo ufanyavyo sivyo :nono::nono::nono:Boko, ni lini utaipa akili yako nafasi kufanya kazi japo kidogo tu? Padri atakuwaje Atheist? au hujui Atheism ni kitu gani! hakika Mohamed Said hasidi mkubwa atakuua roho na akili mtoto wewe.