haki na usawa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 485
- 138
naomba kuuliza je kuna nini katika uchimbaji wa uranium katika nchi hii
maana hata dhahabu uzingatiaji wa afya za wananchi hakuna lakini tunataka kuchokoza madini hatari yaliyokaa chini na uwezo wa kuchimba hatuna ila kuweka wakezezaji tena sababu eti umeme mimi nalia kwa uchungu na nashindwa kuelewa je nchi hii ina nini? na wanataka nini kitokee ndipo watu washituke tunapokwenda? na je viongozi wetu madini mengine yameisha? au kuna mgawanyo wa madini fulani ni fulani kokote yapopatikani nchini ni lazima kamisheni ale yeye? naomba wachangiaji wanielimishe nashindwa kujua sababu ya nchi masikini kuamuru/kutaka kuchimba madini hatari kwa kutegeme wawekezaji na je kweli tutafika salama? Dsm hawana habari lakini maji ya uranium watakunywa wapende wasipende je wananchi wanajua ecolojia? au umeme ni kila kitu kwetu? hata anayelazimisha ajue ndugu zake wataumia tu wapende wasipende maana madhara yana mlolongo mrefu." NAOMBA TUSHIRIKI KUWAELEZA WATOA MAAMUZI NA BILA HIVYO TUSUBIRI MAAFA NA NI MAKUBWA KULIKO YA NORTH MARA YA KIMAZINGIRA" wazoefu waeleze madhara yake wazi na bila hivyo twajirushia bomu wenyewe na hakuna wa kutulipa wenzetu Japani walipigwa mpaka sasa wanalipwa fidia na waliyewapiga." UCHUNGU KUHALALISHA MADHARA KWA WANYONGE NA WANYONGE WAFE ILI MTU APATE ASILIMIA YA KAMISHENI" HAKUNA KIONGOZI MWENYE MACHUNGU NA WANYONGE KAMA UONGO ANGALIA MAENEO YA MIGODI NA SEHEMU WALIKO WAWEKEZAJI. NAOMBA JE TUFANYEJE TUNAKOKWENDA SI KUZURI KILA ZURI LA MWEKEZAJE BILA KUJALI TUNAPATA NINI HATA KIBAYA SAWA KWA NCHI YAKO MAANA WEWE UMEPATA FUNGU LAKOLISILO NA MADHARA NA JE MAREKANI HAYAPO? JE WAMEYACHIMBA? KWANINI HAWATAKI KUCHIMBA? NA KAMA KWANINI KWETU NA SI KWAO? NA JE WATU WAO WATAINGIA KUCHIMBA AU WATANZANIA? JE WAMEJIANDAA KUKABILI MADHARA NA NEMC YA NORTH MARA? KUPEWA TIKEKI NA UNAYEENDA KUMWANGALIA KAAMUZAJE WATU WAKO? KUKODISHA NDEGE KWA WABUNGE ILI WASAIDIE KUFUNGA MJADALA WA MADHARA? kumbuka siasa ni mpito maamuzi yako leo yatakuumiza na wewe pia kesho maana hutakuwa na siku zote."KILA NAFSI ITAPITA ILA JEMA/BAYA LA NAFSI LITABAKI MILELE"
Ndugu yangu Elimu ya watu wetu katika uwanja wa urani peke yake, hata kabla hayajaanza kuchimbwa ni janga la kiaifa! Watanzania tumewashuhudia wakichimba na kuhujumu mkongo wa Taifa hata ule wa Tanesco unaopita juu ya nyaya zao za umeme kwa kudhani ni coper wakauze kwenye chuma chakavu! pamoja na uhamasishaji na elimu kuwa ile optic fibre ni hatari kwa maisha ya binadamu! Hudhani kwamba yale mabaki ambayo hufukiwa ardhini kwenye makasha maalumu ili kuzuia mnunurisho hayataibuliwa na watu kuanza kuchakura humo?Cha maana ni uangalifu katika suala zima la uchimbaji uranium na mchakato wote unaohusiana na madini haya. Madini haya si hatari kama kuna uangalifu wa kutosha na utaalam unazingatiwa. Pia tuzingatie kwamba nchi yetu inahitaji sana nishati na pia kujihadhari na maadui wa baadaye. Nguvu ya kiuchumi inahitajika sambamba na usalama wa nchi. Usipoonesha nguvu yako duniani kiuchumi na maguvu ya kiusalama hata Israel itakudharau tu maana wewe ni sawa na "kitu kisikuwepo duniani" . Hao unaowataja (wajapan nk.) wanajua sana uzembe waliokuwa nao hadi maafa ya kinuklia yakawakuta. Mtanzania ni sharti ajiamini...asidhani kuwa kwa kuwa walioendelea walishindwa kuzuia maafa ya kinukia basi hata sisi tutashindwa. Wao ni wao na sisi ni sisi. Hatuwategemei wao maana busara tulizojaliwa na mola wetu zipo na zinatutosha....Lakini baada ya kusema hayo, nasema hivi: tupige vita ufisadi, ubinafsi, uzembe, na mambo mengine hatari kama hayo.
Nafikiri Uranium ndo gharama wanazolipwa Wamarekani kwa kumficha Balali huko kwao. Sidhani kama walikubaliana na uongo wa serikali yetu kwa bure tu.
Sambi sao wenyewe!
Duh watanzania kwa woga hata kunguru wa Zenji cha mtoto. Tunaogopa hata EAC kana kwamba mayo inatoa radiation, alafu kibaya tuna ujuzi wakuandika yote yanayo support woga wetu. Tumeivalia njuga urani kana kwamba sisi ni nchi ya kwanza Africa kuchimba urani. Congo na Malawi vimekuwa vikichimba miaka sasa, na hizo ni nchi ambazo haziko politically stable kuliko Tz. Tuna tabia za ajabu sana.
Alafu tuko mstari wa mbele kushutumu bila kujifunza na kuelewa tunachokiongelea. Na ajabu ni kwamba wanaojuwa ndio wanaongoza katika kupotosha umma. Bado wengi wetu tunazani mchanga unaotoa miozi tulionao kusini mwa Tz ndio sawa na nyuklia iliyomwagika Japan. Nadhani ifike wakati Tz ijitoe kwenye fikra za ujima na ujamaa zinazotufanya tushindwe kupata faida za rasilimali kwa woga.
Duh watanzania kwa woga hata kunguru wa Zenji cha mtoto. Tunaogopa hata EAC kana kwamba mayo inatoa radiation, alafu kibaya tuna ujuzi wakuandika yote yanayo support woga wetu. Tumeivalia njuga urani kana kwamba sisi ni nchi ya kwanza Africa kuchimba urani. Congo na Malawi vimekuwa vikichimba miaka sasa, na hizo ni nchi ambazo haziko politically stable kuliko Tz. Tuna tabia za ajabu sana.
Alafu tuko mstari wa mbele kushutumu bila kujifunza na kuelewa tunachokiongelea. Na ajabu ni kwamba wanaojuwa ndio wanaongoza katika kupotosha umma. Bado wengi wetu tunazani mchanga unaotoa miozi tulionao kusini mwa Tz ndio sawa na nyuklia iliyomwagika Japan. Nadhani ifike wakati Tz ijitoe kwenye fikra za ujima na ujamaa zinazotufanya tushindwe kupata faida za rasilimali kwa woga.
Jambo moja ambalo nataka kukufahamisha kuhusu Uranium ni kwamba, ule mchanga wa njano ulio kule kusini ni hatari sana. Mimi binafsi niliwahi kuhusika wakati wa utafutaji wa Urani, lakini kitu ambacho tulikuwa tunaambiwa ni kwamba haipaswi kudondosha hata punje ya mchanga ardhini au hata ukigusa kwa mkono ilipaswa unawe sana mikono kwa sabuni. Sababu ni kwamba kama hata kiasi kidogo ulichogusa mkononi ukishika kitu ukala kwa mikono hiyo utaumwa sana tumbo! Sasa jaribu kufikiri kama mvua ikinyesha na kuchukua sehemu ya mchanga huo hadi mtoni hali itakuwaje?
Tatizo kubwa ni pale
tunapopenda kuangalia kila jambo kisiasa. Humu mwetu Tanzania ukiangalia kila kitu kwa mtazamo wa kisiasa hufiki popote. Utajenga conspiracy theories weee hadi mwisho wa dunia ufike. Tutumie umakini zaidi katika kuyaangalia mambo. Tunataka kuendelea sana sisi ktk nyanja zote ikiwa ni pamoja na nyanja ya madini. Jambo la msingi tunalotakiwa kufanya ni kuchanganua jinsi uchimbaji huo unavyotakiwa kufanywa, Namna ya kuongeza wataalam wetu ktk nyanja hii, namna ya kuepuka hatari zinazoweza kuambatana na uchimbaji huo, namna ya kudhibiti mapato yatokanayo na shughuli hiyo, namna ya kunufaika na mapato yatokanayo na uchimbaji huo, nk. Hayo ndiyo tuyafikirie na kuyafungia mkanda kweli kweli. Tukumbuke kwamba nia yetu sisi waTz ni kuwa na uchumi mkubwa na kuiweka Tz iwe miongoni mwa nchi zinazojitegemea na ambazo zinategemewa na mataifa mengine kiuchumi...tunataka tufike huko haraka iwezekanavyo.