Uchawi wa kulogewa kibyongo, busha

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,084
Ukifuatilia kwa karibu haya mambo kuna mahali inafika unabaki na mshangao
Mtu anaanza kuugua from no where..!anajikunja kama ana kibyongo au kabeba kitu kizito hasa au anatembea utadhani ana busha na kuna wakati amevimba kabisa sehemu husika

Kwa usomi wa kimagharibi na kushika dini za kuletewa mnakuwa hamuamini katika nguvu za giza hivyo mnampeleka mgonjwa hospitali....anafanyiwa vipimo vyote kule lakini hakutwi na ugonjwa wowote, japo anaumwa kweli
Kwa shida sana mwisho wa siku mbakubaliana na ushauri wa baadhi ya ndugu au marafiki, wengine wanasema maombi na wengine wanasema kwa waganga wa kienyeji

Hawa wa mwisho wanashinda na mgonjwa kupelekwa huko kwa mganga husika , mnapokelewa na matibabu yanaanza

Mara mgonjwa anapewa dawa na kuanza kutapika vitu vya ajabu mara nyingi zikiwemo nywele kipande cha kaniki nk nk...mnatajiwa mbaya wenu mnapewa dawa ya kinga mnalipia matibabu na kuondoka

Wengi wamepigwa kwa namna hii...hawa watu waitwao waganga wa kienyeji wengi si waganga hasa bali ni matapeli wanaojua mazingaombwe, na wengi huwa na uwezo wa kumtengenezea mtu ugonjwa ili baadae aje amtibu na kupata sifa na kipato

Waathirika wengi kwenye hili ni wale wapendao sana kwenda kwa waganga kwa ajili ya kupata bahati ngekewa na kupendwa..ukifika pale atakusoma na kukufahamu mtazamo wako hivyo atakutengenezea phantom la kuja kukudhuru mbeleni
 
Duuuh! Mkuu,je kama asingeenda kwa mganga aliyempandikiza ugonjwa huo kupata matibabu,asingepona!?
 
Duuuh! Mkuu,je kama asingeenda kwa mganga aliyempandikiza ugonjwa huo kupata matibabu,asingepona!?
Mara nyingi huwa na connection ya ndugu rafiki au hata mhanga mwenyewe, yani kati ya hao au hata wewe mwenyewe mmoja atatoa ushuhuda wenye nguvu kuwa fulani ndio kiboko wa hayo matatizo
 
Lakini pia watu wa pwani ni hatari sana hasa linapokuja swala la mke wa mtu....kaa mbali mno na huyo binadamu
Mabusha ni aina fulani ya ugonjwa wa matendo unaoambukizwa na aina fulani ya mbu, lakini kule pwani unaweza kulipata busha overnight ukijifanya inasimama sana...mitaa ya kule kushushwa mshipa ni kitu cha dakika
 
Kuna watu flan flan hawajaamka, wakiamka wataamka Na wewe, maana wanataka kukupangia cha kupost huku
 
Huwa naamini kama umetoka kweye familia ambayo hukuwahi kumwona baba ako au mama wanaenda kwa mganga na hawajawahi kukupeleka kwa mganga ni ngumu sana mtoto uje kuwa na tabia hiyo...Wafuasi wengi wengi wa waganga walifundishwa toka utotoni wakiwa na wazazi wao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…