Uchawi na muujiza ni mapacha

Mosi,,,,
Nimesema ndugu na sijasema marafiki,,,, katika hali ya kawaida marafiki wanagomba na kushindana ndio seuze kwa ndugu?

Nina mifano mingi ya ndugu wamekuwa hawapatani kabisa, mfano Yakobo na Esahu, walianza kupigana tangu wakiwa tumboni mwa mama yao.

Kwa hivyo ni sawa kabisa Uchawi na muujiza ndugu pamoja na kwamba ni maadui. Kwanini nasema ndugu????

Nasema ndugu sababu uchawi haukujiumba, alikadhalika muujiza pia haukujiumba, bali vyote viwili vimeumbwa na Mungu mwenyewe.

Kuna baadhi ya watu wanataka kutuaminisha kuwa shetani kaumba uchawi, si kweli, shetani uchawi kaukuta, anachofanya shetani ni kuutumia tu.

Katika mada yangu ya msingi nimetaja aya kadhaa za kutoka katika biblia na quran zikionesha Mungu ni muumba wa kila kitu(uchawi moja kati ya vitu hivyo)

Ndio maana Mfalme Suleiman amesema katika methali zake kuwa "Bwana amefanya kila kwa kusudi lake, hata ubaya kwa siku ya ubaya"

rejea mithali 16:4

Pili.
Si kweli kuwa nimeshindwa kutoa ushahidi wa vitendo jinsi watu walivyokuwa wanafanya uchawi kwa mujibu wa biblia, naomba soma vizuri mada yangu unaweza kuona.

Nimeeleza jinsi Farao alivyotumia waganga kufanya uchawi kupambana na Mussa, Watu wa Farao walifanya uchawi ili kugeuza fimbo zao kuwa nyoka.

Kwa kuongezea hapo, Sauli baada ya kukataliwa na Mungu, na baada ya kukosa neno la unabii juu ya nini anatakiwa kufanya na nini asifanye, alienda kwa mganga wa kienyeji, ambaye alikuwa anatumia pepo wa utambuzi (jini mpiga ramli), ili aweze kuwasiliana na Samweli ambaye tayari ameshakufa, ili sasa Samweli amweleze nini anatakiwa kufanya.

Yule mganga aliweza kuitafuta roho ya Samweli kwa kutumia uchawi, na akaiona na kaongea naye, na hapo Sauli akajua nini atakiwa kufanya.

Rejea 1 Samweli 28:3-14

Hata hivyo, huenda hoja yako ni kuwa, biblia haijaonesha ni mambo gani ya kiuchawi walifanya watu Farao katika kugeuza fimbo kuwa Nyoka au mambo gani ya kichawi alifanya yule mwanamke mwenye pepo la utambuzi hata akaweza kuongea na roho ya Samweli.

Kama ndio hoja yako.

A. Elewa biblia na quran hazijaacha kitu juu ya ulimwengu, ila vitabu hivi havijaandika kila kitu kwa kina, na kama kitabu kimoja kingeandika kwa kina kila kitu, ukubwa kitabu hicho ungeizidi si dunia yetu tu lakini mfumo mzima wa jua(solar System)

Mathalani, "Mungu akasema iwe nuru"

Hivi ni kweli kuwa Mungu aliposema iwe nuru na nuru ikawa? Hakuna jambo lolote lilofanyika zaidi ya hiyo kauli? Kuna mambo yalifanyika na hapa nataka nikupe ushahidi.

HAPA KUNA NAMNA MBILI
NAMANA YA KWANZA.

Kwa mujibu wa biblia tunaweza kusema kuwa mungu alitumia siku moja kuumba NURU.

Lakini kwa mujibu wa biblia pia siku moja kwa mungu kwetu ni miaka elfu moja. Kama ndivyo tunaweza kusema kuwa Mungu alitumia miaka eflu moja kuumba NURU, hivi kwa miaka yote hii eflu moja Mungu alikaa tu au kuna mambo alokuwa anayafanya kuhakikisha NURU inakuwa? jawabu ndio, na uumbaji wa mungu ni zaidi ya "kuwa" kisha ikawa.

NAMNA YA PILI.

huenda kweli pia kuwa Mungu aliumba NURU kwa kitendo cha kufumba na kufumbua, yaani, "kuwa" kisha ikawa.

Lakini kwa nikirejea kuwa siku moja kwa mungu kwetu sawa na miaka elfu, na jaalie kitendo cha kufumba na kufumbua ni sawa na kitendo cha sekunde moja, kwa hivyo hapo ni sawa na kujiuliza sekunde moja kwa mungu kwetu ni sawa muda gani? ukikokotoa mahesabu utapata sekunde moja kwa mungu kwetu sawa siku 4 na masaa yake matatu.

Kwahivyo naweza kusema kufumba nakufumbua kwa mungu kwetu ni sawa na siku 4. Hivi kwa kusiku nne zote Mungu alitumia kutamka "kuwa nuru" alitamka alafu kukawa hakuna mambo mengine yanafanyika? Jawabu kuna mambo yalikuwa yanafanyika kinyume chake hakuhitaji siku nne.



ZINGATIA: kila kitu kipo ndani ya quran, lakini quran haijaandika kila kitu. Hata biblia pia.

B.
Mungu hapendi tuujue au tuufanye uchawi, ndio maana katika vitabu vyake amefafanua zaidi jinsi muujiza unavyofanyika na kuushinda uchawi lakini haoneshi jinsi uchawi unavyofanyika.

Mathalan wakati Mungu anataka kuwakomboa wana Israeli kutoka Misri alipata ushindani mkubwa sana kutoka kwa uchawi, lakini ule uchawi ulio kuwa unashinda na muujiza hatukuoneshwa bali tulioneshwa muujiza tu kupitia mapigo kumi na mbili.

Pigo la mwisho wana wa Israeli walitakiwa wachinje kondoo au mbuzi, wale wakiwa wamesimama, na mboga za uchungu, damu wapake katika miimo ya milango. Lakini wakati wana wa Israeli wanafanya hivi wachawi wa Farao kuna yao wakuwa wanayafanya si biblia wala si quran ilo onesha kinagaubaga nini Wachawi wa Farao walikuwa wanafanya.

Vitabu hivi vinaonesha kushindwa kwa Farao baada ya kila mzaliwa ea kwanza wa Misri kufa.

ILA UJUE.
Yale walio kuwa wanayafanya wamisri waliya rekodi katika vitabu vyao na mengi waliyaandikia vitabu maalum vya uchawi vya ngazi(hatua au milango) mbalimbali.

Mfano kuna kitabu cha uchawi, book of spells kinaitwa "Book of Dead" kilianza kutumika na wamisri kwenye mwaka 1550BC na baadhi ya spells zilianza kutumika na wamisri wenyewe zaidi ya miaka 1500 kabla hata ya kuandikwa kitabu hicho.

Ikiwa Mussa alizaliwa mwaka 1400 BC utagundua kitabu kilikuwako kabla hata ya Mussa kuzaliwa. Yaliyo andikwa katika kitabu hichi hayakuandikwa kitika biblia wala quran. Na kwa kupitia kitabu hiki ndipo pakapatikana vitabu vingi vya uchawi na ramli mfano satal habar.

Ngoja niishie hapa, sababu nachelea kuingilia sehem ya pili ya mada yangu, ambayo hivi karibuni nitaanza kuandika.
 

Kuna makanisa 37,000 ya kikristo! Kwa kuwa hayapatani katika mafundisho yao huenda kila kanisa lina mungu wake maana Biblia inasema Mungu si wa machafuko.Ndiyo maana wengine husema Yesu ndiye Mungu,Wengine Roho mtakatifu ,wengine Mungu baba,wengine Utatu mtakatifu.Jibu la Biblia ni Yehova ndiye Mungu wa kweli Muumba wa Mbingu na Dunia.Zaburi 83:18,Kutoka 6:2
 
kwanza nipende kumpongeza kipekee mtoa mada kwa kufikiri sana na kuibuka na andiko hili refu sana lenye mrengo wa kidini ambao kwa kweli amekiri ndio msingi wa andiko lake hili kwanza ameweka msawazo kwenye uwanja wa hoja kwa kuainisha nguvu mbili zinazosukuma mambo duniani yaani UCHAWI na MIUJIZA,sina shaka kukukubaliana na maana alizodadavu kuhusu Dhana hizi mbili na ya kwamba ni nani wapo nyuma wakipull strings ili yatokee yanayoitwa MIUJIZA na UCHAWI pia nakubaliana kimsingi kabisa na hoja ya UCHAWI kama ni udenguzi ama ukiushi wa kaida zinazoongoza mambo yatokee katika maumbile ya kawaida lakini yakisimamiwa na mkuu wa nguvu za giza lakini umejichanganya ulipokuwa ukijibu hoja za ndugu tofyo
ukasema mwazilishi wa uchawi sio shetani kwa maana ameukuta uchawi na hivyo akautumia kuenda kinyume na Maumbile halisi ambayo Mungu aliyaumba
excuse me!!!!
Biblia inamtaja shetani kama muasisi wa dhambi(uchawi)maana dhambi ni uasi wa sheria na sheria ndio msingi wa maisha ya binadamu
mkuu wa Miujiza ambaye ameshikilia Sheria zinazoongoza maisha ya sayari na ulimwengu wote yaani Mungu ndiye hasa wa kuinuliwa juu ya muujiza wowote ule unaotendeka kwa jina la Yesu.
Shetani alichofanya ni kuleta Bandia miujiza bandia,Neno bandia theology bandia na sheria bandia ili tu kutaka kujitwalia kiti cha Mungu pambano kubwa sana ambalo Binadamu anagombaniwa hapa lilianzia mbinguni chanzo kikuu ni Ibada shetani akitumia mtindo wake wa kwanza ushawishi.
Akatupwa toka huko Mbinguni wala mahali pake hapakuonekana huko mbinguni.
Kwahivyo swala la uchawi ni swala la shetani kikwelikweli kabisa hapakuwahi kuwa na mauzauza mahali pengine kabla shetani hajaasi mbinguni
ikumbukwe alikuwa malaika wa nuru hivyo nguvu na uwezo wake havikutwaliwa toka mikononi mwake.
pambano na Uchawi na miujiza linaenda likishabihiana kabisa na Dhana ya WEMA na UOVU/UBAYA hili ndio pambano kubwa hasa la leo tunapoelekea mwisho wa wakati
Swali la kujiuliza ni je Umepata nguvu ya kimungu ili ubainishe bayana dhana hizi mbili maana wapo waalimu wengi humu duniani wenye mfano wa Utakatifu lakini wakizikana nguvu za Mungu
Hitimisho!
katika muujiza wowote jiulize?
Waende sawasawa na sheria(torrah) na Shuhuda(yale ambayo manabii wa haki wa MwenyeziMungu wameyaandika)kama hawasemi sawasawa kwao hapana asubuhi!
 
Cjamaliza kusoma Inaboa sana. All I can say Acheni Uchawi kama mnataka kujifunza. Mungu ni mmoja tu.
 
Mtoa mada yupo vizuri anajua anachokisema kwakweli..hateterki mana kapigwa swali hapo kajibu mpaka nacheka mwenyewe...vitu vyenye mantiki kabisa..inatakiwa kufikiri zaidi na zaidi..asantr sana mtoa mada
 
Kama Mungu hakuumba uchawi basi pia ukubali Mungu hakuumba kila kitu, pamoja na hayo una ushahidi wowote kuonesha kuwa Ibilis kaumba uchawi?
 
Mtoa mada nashukuru kwa jibu lako zuri.lakini kusudio "A" la swali langu linaowana na dhamira "B" ya swali langu.
Rejea kauli hii"mchawi au miujiza anatakiwa ajue anataka kufanya nini,wapi na vitugani vinavyotakiwa kuchanganya"ambayo umeiweka hapo juu.
sasa katika muktadha huo umeelezea yesu alivyochanganya tope,kisha ukaonyesha ya Ezekieli na kunyoa kwa panga na kufanya alivyofanya.Lakini hii ni upande mmoja wa miujiza.sasa ilituweze kufanya comperative ya Udugu au Umapacha kama ulivyosema,naomba unionyeshe na mchanganyo na vitu vinavyotumika kwenye uchawi.
Katika hoja hii ni kwamba Mungu kaumba kilakitu lakini suala la udugu au mapacha ni mpaka hivyo vitu viwe vinanasaba iliosawa.Kwasababu Tui la nazi linafanana na maziwa kwani vitu hivyo ni ndugu????lakini nini nasaba zao???
Ninachokitaka mimi unionyeshe udugu wao.na sinashaka kwamba nguvu hizi zinatoka kwa mmoja.Lakini kama miujiza ilikuja kama hoja ya kupinga uchawi since kwamba uchawi unatumiwa kama hoja kupotosha watu .wapi uduguwao?
 
Uchawi, miujiza, mazingaombwe, kiini macho.... Vyote hivi ni kitu kimoja. Ni kama vile unakuta mtu ana jina la utani, Jina la ubatizo, jina la mtaani nk
 
nitakuja inshallah
 
Hivi wewe unajua maana ya ALLAH?? WAKRISTO WA MASHARIKI YA KATI UNAJUA KUSEMA MUNGU WANASEMAJE?? Kwa taarifa yako tamko Allah kwa kiswahili maana yake ni Mwenyezi MUNGU na wakristo wanaotumia lugha ya kiarabu husema Allah wakimaanisha Mwenyezi MUNGU. Jifunze utaelewa. Ulichoeleza hapo ni kama vile kusema Almighty GOD na Mwenyezi MUNGU ni vitu tofauti kumbe ni kitu kimoja tofauti ni lugha. Mwenyezi MUNGU jina lake limejipambanua kwa sifa zake. Huwezi kusema MUNGU wangu ni mbuzi muumba wa mbingu na ardhi, wenzako watamchinja yule mbuzi wamle nyama halafu watakuuliza mungu wako tumemla utampata wapi mungu mwingine!! Kama Ibrahimu alivopasua masanamu akaacha limoja, walivomuuliza nani kafanya hivyo?, akasema, liulizeni lile kubwa lao kama lenyewe ni MUNGU na lisema nani kawavunja wenzake; wakashikwa na aibu kubwa maana halikuweza kuongea wala kuwatetea wala kuwadhuru! Kwa mantiki hiyo nadiriki kusema Mwenyezi MUNGU kajipambanua kwa sifa zake sio kwa jina, ukitaka kumwita jina lake wala usipate taabu, unawezatumia sifa zake kwa kusema tu "Ee Muumba wa Mbingu na ardhi..." aliyeumba mbingu na ardhi atakuitikia sawasawa na imani yako juu yake.
Ni vyema ifahamike kuwa Quran haijawahi kukataa ukristo wala uyahudi na wala usilamu si dini mpya bali ni dini ileile ya Ibarahim na Ismail na Is haka na Yakobo na mitume na manabii. Wala Quran si neno jipya bali linasadikisha yaliyokuwepo kabla yake na ni ukumbusho kwa wachamungu waliopotoka. Ukumbuke wachamungu walikuwepo kabla hata ya kuja muhammad na neno la Mwenyezi MUNGU lilikuwepo tangu zama za Nuhu, lkn wengi katika wachamungu walikuwa kwa nyakati fulani wanaanza kwenda kinyume na maandiko au wanashindwa kutafsiri maandiko, huvyo Mwenyezi MUNGU alikuwa akiwaleta mitume kwa nyakati tofauti kulikumbushia neno lake lililokuwepo tangu awali na kuwaelekeza mengine mapya. Labda nikukumbushe kuwa mitume wote walitamka neno moja tu "Mcheni Mwenyezi MUNGU na nitiini mimi" Hapana mtume ama nabii yeyote aliyewahi sema "nicheni mimi" ama "muabuduni asiyekuwa Mwenyezi MUNGU". Ipo wazi kabisa kuwa MUNGU wa wachawi na wasio na dini na wenye dini na wema na waovu ni MUNGU mmoja tu, yeye ameumba kila kitu na kwake tutarejeshwa sote.
Quran ipo wazi kabisa kuwa kabla yake vilikuwepo vitabu vya Injiri, torati, na zaburi na vingine vilivyoshuka kwa manabii wengi waonyaji. Kifupi wakristo na waislamu tofauti zetu zimejikita kwenye namna ya kumfikia huyu muumba na kamwe hatuna muumba tofauti na Mwenyezi MUNGU aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo.
Aidha, quran haijanukuu vifungu vya biblia hata kimoja ila imenukuu baadhi ya matamko ya manabii moja kwa moja waliyoyatamka kuwaambia watu wao. Ikumbukwe kuna manabii wametajwa kwenye quran lkn biblia haijawahi kutamka na kuna matendo ya manabii yametajwa kwenye quran lkn biblia hajawahi kutamka; mfano Yesu kuumba ndege ipo kwenye quran lkn biblia ipo silent; yesu kuzungumza katika uchanga wake ipo kwenye quran lkn biblia haijawahi kutamka. Ni kukosa uelewa kusema quran imenukuu biblia.
 
Mhhh hapa inabidi mtu akimbie.
Maswali mengine magumu hadi mtu anazikataa aya za kitabu kitakatifu kinachosema Mwenyezi MUNGU kaumba kila kitu including wema na ubaya. Mimi naamini Mwenyezi MUNGU kaumba kila kitu hadi uchawi. Na uchawi hauna mamlaka ya kufanya kazi popote ila hadi yeye aridhie. Hebu tupate nukuu kutoka kwenye Quran;
"Hakika shetani hana nguvu (mamlaka) juu ya walioamini na wanaomtegemea Mola wao" (quran 16: 99)
"Wala mchawi hafaulu popote afikapo" ( Quran 20: 69).
"Mwenyezi MUNGU ndiye muumba wa kila kitu na Yeye ndiye mlinzi wa kila kitu" (Quran 39: 62).
Kwa waliomwasi Mwenyezi MUNGU ridhaa ya wao kukumbwa na uchawi ipo wazi kwa maana wao hawamtegemei Mola wao hivo shetani ana nguvu juu ya nafsi zao. Adha, hata wanao mchamungu uchawi unaweza kuwapata kama mtihani kwao mfano ni Nabii Ayubu alilogeka, Mwenyezi MUNGU aliruhusu nguvu za shetani zifanye kazi kwake na alifaulu mtihani huu hatimaye Mwenyezi MUNGU alimponya na kumuinua zaidi.
 
Hebu jiongeze kidogo nawewe mkuu. Udugu wao ni kuwa aliyeumba hivyo ni mmoja ambaye ni Mwenyezi MUNGU. Tofauti yao ni kuwa watumiaji ndio wako tofauti, waliomwasi Mwenyezi MUNGU hutumia uchawi na wanaomtii Mwenyezi MUNGU hutumia muujiza. Anayewahadaa wanadamu watumie uchawi si yeye muumba bali ni yule mwovu mdanganyifu shetani
 
Mtoa mada upo vzuri sana. Hongera kwa taaluma hii. Umeshuka vitu hadi akili inakubali.
 
Muendelezo afu mbona whatsap haupo?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…