Uchawi: Dawa za kujiepusha na ajali

Uchawi: Dawa za kujiepusha na ajali

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,349
Reaction score
36,303
Nianze kwa kutoa pole zangu kwa watu wote walio poteza ndugu zao kwenye ajali mfululizo zilizo tokea hivi karibuni.Hakika hakuna msiba unao uma kama msiba wa ajali, maana mtu mnakuwa nae leo halafu from no where unasikia fulani hayupo tena duniani! Inasikitisha sana.

Pamoja na yote hayo,lakini je wajua kuwa zipo dawa za kichawi, zinazo weza kukuepusha na ajali ? Kama ulikuwa haujui basi mbaroko ndo nakujulisha. Follow my lead !

UCHAWI : DAWA ZA KUJIEPUSHA NA AJALI.


Zipo dawa mbalimbali za kujiepusha na ajali. Ziwe ni ajali zitokanazo na uzembe wa madereva au zile za kutengeneza ( Ajali za kichawi ).

Nitazitaja chache kati yazo na moja wapo nitaielezea kidogo coz ni rahisi, na haihitaji tunguli.

1. ZINDIKO MAALUMU LA KUKUEPUSHA NA AJALI ZA AINA ZOTE :

Yapo mazindiko maalumu yanayo fanyika kwa ajili ya kuwaepusha watu na ajali. Katika mazindiko ya kuwakinga na kuwaepusha watu na ajali, zindiko linalotajwa kuwa na nguvu kuliko yote ni zindiko kutoka katika KABILA MOJA LINALOPATIKANA KUSINI MWA TANZANIA. Ukifanyiwa zindiko hili, huwezi kufa kwa ajali, kwa mkono wa mtu wala kwa hila ya aina yoyote ile.

2. Zipo dawa maalumu za kichawi maalumu kwa kuwaepusha watu na ajali.Utapewa dawa na tunguli za kichawi. Kuna mambo ambayo utakuwa unafanya kabla ya kusafiri safari yoyote ile ya mbali. Tunguli hiyo itakuonyesha kama safari hiyo ni ya heri au la.

3. JINI AU MZIMU MAALUMU KUKUKINGA NA AJALI: Utapewa mzimu au jini litakalo kuwa linafanya kazi ya kukukinga na ajali yoyote ile. Utakuwa unaoteshwa siku kabla kuhusu usalama wa safari yako.


4. CHALE MAALUMU ZA KUKUEPUSHA NA AJALI : Ulishawahi kusikia mtu anasema ' MACHALE YAMENICHEZA?" Basi chanzo chake ni hapa. Utachanjwa chale na kupakwa dawa maalumu.Kama kutakuwa na jambo lolote baya kwenye safari yako,basi kitatokea kitu fulani ambacho kitakuzuia kusafiri. Siku zote utasafiri safari salama.


HIZO HAPO JUU NI BAADHI YA NJIA ZINAZO WEZA KUTUMIKA KUMKINGA MTU NA AJALI ZA AINA ZOTE.


Hii hapa chini ni njia ambayo inaweza kutumiwa hata na wale wasio amini masuala ya tunguli. Unachotakiwa ni kufanya mambo yafuatayo:

Ukipanda kwenye gari au chombo chochote cha usafiri. Chukua simu yako au saa yako. Tafuta tarehe yoyote ya nyuma ambayo wewe ulikuwa hai, Badilisha tarehe ya kwenye saa yako ya siku hiyo na kuiweka kuwa tarehe ya siku hiyo ya nyuma ulio ichagua. Kama unakumbuka tarehe yoyote ya nyuma ambayo wewe ulisafiri kwenye chombo chochote cha usafiri (safari ya mbali ) na ukafika salama,unaweza kuifanya kuwa ndio tarehe yako ya siku hiyo.

UKIFANYA HIVYO, SAFARI YAKO UTAFIKA SALAMA NA HAUTO HUSIKA KATIKA AJALI YOYOTE SIKU HIYO.

 
ahahahahahaahaaaaaaaaaaaaaaaa....shikamooooooooooooooo
 
duh!!! mkuu huu ndo mrejesho wa ile kozi uloendaga?

Nimekuja kuzungumzia suala linalo ikabili jamii ,so nimetumia knowledge yangu ya masuala haya kuwaelimisha watanzania wenzangu
 
Huyo ndo LIKUD, nenda kachukue Jini lako la kukuepusha na ajali, halafu kakate tiketi ya basi usafiri, ukirudi salama njo uandike hapa
 
dunia ina mambo, yapo ya mchana yapo ya usiku. haya wadau wa safari
 
Nimepanda daladala Mbagara-Makumbusho
safari yangu ilikua inaishia mwisho wa safari
lakini nimeamua kuteremkia Karume.

amepanda mama mmoja kapiga Ninja ni kwamba
haonekani chochote hadi mikono kavaa gloves
anaongea na sim tangu anapanda hadi nateremka
alafu Inshallah nyingi kiufupi ni anaongea kiarabu
tupu!

nilichoambulia ni kimoja tu Kul nafs
dhaikatur maut nikaona isiwe tabu! Nimeshuka
mie nina watoto wadogo!
 
Hebu leta dawa ya uchawi itakayobadilisha morogoro road kuwa double road kutoka dar hadi moro
 
Huyo ndo LIKUD, nenda kachukue Jini lako la kukuepusha na ajali, halafu kakate tiketi ya basi usafiri, ukirudi salama njo uandike hapa

Nimetoka Lindi leo
 
Nimepanda daladala Mbagara-Makumbusho
safari yangu ilikua inaishia mwisho wa safari
lakini nimeamua kuteremkia Karume.

amepanda mama mmoja kapiga Ninja ni kwamba
haonekani chochote hadi mikono kavaa gloves
anaongea na sim tangu anapanda hadi nateremka
alafu Inshallah nyingi kiufupi ni anaongea kiarabu
tupu!

nilichoambulia ni kimoja tu Kul nafs
dhaikatur maut nikaona isiwe tabu! Nimeshuka
mie nina watoto wadogo!
uko afghanistan and siria? tangu muda huo mpaka sasa kashashuka anapika kwake.
 
lukud tell us the side effects za mbinu yako ya kuepusha ajali hasa ukitilia maanani majini, mapepo na wachawi wanategemea ajali ili wapate damu
 
Last edited by a moderator:
Tupe takwimu, evidence based practice . Au ndo unataka uanze kukusanya data?
 
lukud tell us the side effects za mbinu yako ya kuepusha ajali hasa ukitilia maanani majini, mapepo na wachawi wanategemea ajali ili wapate damu

Aliyekwambia majini na mapepo wanahitaji damu nani?
 
Tupe takwimu, evidence based practice . Au ndo unataka uanze kukusanya data?


Unaumwa au ? Kuna uhusiano gani kati ya komenti yako na uzi wangu?
 
iyo nayo imekaa kichawi zaidi njia bora ni ile ambayo everybody anakuwa warned in case of any danger most of us used to ignore it as a result you suffer to the consequences!
 
Ktk Harakati Hzo Hzo Jana Kuna Jirani Yangu Kaenda Kwa Fundi Welding Kutengeneza Nguo Kwa Kutumia Mabati Magumu Na Helmet Za Bati Gumu Angalau Kupunguza Kasi Ya Kuumia Au Kufa Kabisa Alivyojaribisha Wanaonekana Kama Maroboti Lkn Inaweza Saidia Au Wadau Mnasemaje?
 
Back
Top Bottom